Source : wasafi Media
Gereza la Songwe mkoani hapa linatarajiwa kuvunjwa na kujengwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini adimu duniani ya niobium.
Mbeya. Gereza la Songwe mkoani hapa linatarajiwa kuvunjwa na kujengwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini adimu duniani ya niobium.
Ni baada ya madini hayo kugundulika kuwapo kwenye eneo la gereza hilo.
Taarifa za uhakika zimeonyesha michoro ya ujenzi wa gereza jipya imeandaliwa.
Mhandisi wa Migodi wa Kanda ya Kusini Magharibi, Zephania Nsungi alisema Kampuni ya Panda Hill Niobium Project Tanzania imefanikiwa kupata madini hayo karibu na gereza hilo.
“Madini haya ni adimu duniani na yanapatikana katika nchi chache sana, hivyo yakianza kuchimbwa upo uwezekano wa kuliondoa Gereza la Songwe na kujengwa upya eneo jingine,” alisema.
Mfanyakazi wa kampuni hiyo, Emmanuel Kisasi alisema jana kwamba, viongozi wao wako likizoni Ulaya na wanatarajia kurejea nchini mwezi ujao.
Kisasi ambaye hakutaka kuzungumza kwa kina juu ya madini hayo, alithibitisha kuwapo kwa mpango wa kuanza kwa mgodi eneo hilo na kwamba, unatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 30.
Mkuu wa Magereza mkoani hapa, Julius Sang’udi naye alithibitisha kuwapo kwa mpango huo na kusisitiza kwamba, unasimamiwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza chini ya Kamishna aliyemtaja kwa jina moja la Chamlesile.
“Maofisa wa Serikali na wataalamu wa madini hayo wakitaka kwenda eneo hilo wanatoa taarifa hapa na wanakwenda huko moja kwa moja, hivyo mimi siyo msemaji wa mpango huo,” alisema.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao, madini hayo huchanganywa na metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi wa bomba la kupitishia mafuta.
Vilevile hutumika kama metali kwa injini za ndege na husaidia kuzuia mitambo yake kutopata joto kali.
The Panda Hill Niobium Project is located approximately 26km from the city of Mbeya, in south-western
Panda Hill Project – On Track to Be Africa’s First Niobium Mine
The Project is fairly unique in that it has excellent nearby infrastructure including: TAZARA Rail line (2km away), a dry port located in Mbeya (26km away), the Dar es Salaam – Tunduma Highway (5km away), Songwe Airport (8km away), the La Farge Songwe Cement Factory (6km away) and a major fuel depot in Mbeya.
Access to water and power is also relatively simple with the Songwe River, a major water course, running next to the mining tenements and TANESCO planning a new 400kV power line that will run past the licence area.
The Mbeya region is also a developing mining area with the established Shanta goldmine less than 100km away and Peak Resources developing a rare earths mine nearby.
Mbeya city is a growing city with good educational and medical facilities, including technical colleges that are expected to be a source of personnel for the operations.