Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Jina halijakaa sawa kabisa.kwa Nini isiitwe Arusha stadium.majina ya watu ni kupoteza majina yetu ya asili
 
Jina halijakaa sawa kabisa.kwa Nini isiitwe Arusha stadium.majina ya watu ni kupoteza majina yetu ya asili
 
akili yangu mimi inanituma kuuliza hivii, kama tunao uwanja pale arusha ule wa michezo uliopo sasaivi, kwanini tutumie bilioni zaidi ya 200 kujenga mpya? badala ya kuchukua hata bilioni 50 au 100 tukakarabati uleule na kuujenga uwe bora? kwahiyo arusha watakuwa na viwanja viwili vya ku take care, wataweza? au mimi nawaza vibaya?
Huo uwanja uliopo Ccm wamejimilikisha, bora tujenge tu mwingine wa umma
 
Sio jambo la kawaida serikali kutupiga kamba za za ujenzi wa uwanja wenye kuingiza watu 30000,eti ujenzi wake utumie shilingi Billioni 224 . Wakati uwanja wa Benjamin Mkapa wenye kuingiza watu 60,000 Umetumia billions 64 .Na baadae ukakarabatiwa kwa bilioni zingine 30 na hapo ulipo ni viwango full.
Hili siojambo la kawaida kabisa .
Serikali ije na ufafanuzi wa kueleweka hapa.Nchi hii hazina imeshikwa na watu watata.ushahidi ni mwingi na uko Ikulu kwa miaka mitatu sasa kupitia taarifa za CAG kwa miaka mitatu mfululizo bila hatua stahiki kuchukuliwa.
Madonda ya ubadhirifu wa MV Magogoni bado hayajapona.
Madonda ya DP-WORLD ndio bado yana Bandeji za hospitali.
Ngumi za wizi wa kimfumo serikalini na TAMISEMI hata Rais amezisikia na kuzitamka hivi Punde.
Hivyo tunayo kila sababu ya kuwatilia shaka kwa kila michanganuo yao yenye utata wanayotuletea kila uchao.
Wanamzeesha majaliwa kwa kutembea akibweka bila kujaaluwa kuwadhibiti.

Salaleikh!
Tumswalie Mtume!
Kuiba pesa yamkopo, inafikirisha sana,

Labda sababu hawatolipa wao.
 
Kipindi cha Mwendazake alikuja Mfalme wa Morocco na kuahidi kujenga uwanja Dodoma,lakini hadi sasa nashangaa kimya sijui sababu ni nini
 
Bajeti inaonekana kubwa ukilinganisha na Benjamin mkapa stadium hii kutokan na kushuka kwa thaman ya fedha maan kam uwanja umejengwa kwa 60B na matengenezo tu yamegarim 30B ndipo utajua thaman ya fedha inashuka kila kukicha
 
Serikali imeingia mkataba wa kuanza Ujenzi wa uwanja Mpya Jijini Arusha Maarufu kama Samia Suluhu Hassan Stadium ambao ni Mahsusi Kwa Ajili ya Maandalizi ya AFCON 2027.

Uwanja huo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 286.

Kazi iendelee 👇👇

View: https://youtu.be/q05ytnyfpa0?si=jLrsYa4X_7tKcjKO

============

Serikali kupitia wizara ya Sanaa ,Utamaduni na Michezo leo Machi 19, 2024 imesaini mkabata wa ujenzi wa Uwanja wa Dokta Samia Suluhu Hassani wenyewe thamani ya shilingi bilioni mia mbili na themanini na Sita ambao utatumika katika michuano ya mataifa Afrika AFCON 2027 inayoandaliwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Michezo Dokta Damasi Ndumbaro amesema Lengo la uwanja huo kujengwa mkoani Arusha ni kuchochea maendeleo ya sekta utalii kupitia michezo.
---

BILIONI 286 KUTUMIKA UJENZI WA UWANJA MPYA JIJINI ARUSHA

Serikali imesaini Mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 286 na kampuni ya China Construction Engineering Group (CRCEG) kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa mpira wa miguu Mkoani Arusha.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini Mkataba huo leo Machi 19, 2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 30,000 huku akibainisha kuwa uwanja huo utakuwa wa kisasa zaidi Afrika Mashariki.

Amesema Serikali itahakikisha ujenzi huo unafanywa kwa haraka kwa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 ikiwa ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema uwanja huo utachagiza kwa kiasi kikubwa utalii nchini kwa kuwa uwepo wa uwanja huo utakuwa chachu shughuli mbalimbali tofauti na mpira wa miguu kama vile mchezo wa riadha, biashara zitakazokuwa zinafanyika.

"Uwanja huu utakuwa na ubora wa hali ya juu kwani utakuwa na vyumba vya watu mashuhuri, tumefanya zoezi hili leo ambapo, Rais Samia wetu anatimiza miaka mitatu ya uongozi wake, amesema Dkt. Ndumbaro.

Aidha, ameipongeza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo kwa juhudi ilizofanya za kuhakikisha zoezi hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amemtaka Mkandarasi wa uwanja huo ahakikishe kuwa ujenzi huo unakamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

"Wakandarasi hakikisheni kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025 uwanja uwe umefikia kiwango kinachoridhisha na utekelezaji huo uanze haraka iwezekanavyo ikiwa ni maandalizi kuelekea katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON),"amesema.

Amesema Kamati itatoa ushirikiano kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kama ilivyokusudiwa akibainisha kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaitendea haki sekta ya michezo kama anavyofanya kwenye sekta nyingine akitoa wito kwa wakazi wa Arusha watunze miundombinu ya uwanja huo.



View: https://www.instagram.com/p/C5V5FO6tABm/?igsh=ZnRreDVmNWNrcGFk
 
Back
Top Bottom