Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Sio jambo la kawaida serikali kutupiga kamba za uwizi wa fedha za ujenzi wa uwanja wenye kuingiza watu 30000 elf ujenzi wake utumie shilingi Billioni 224 . Wakati uwanja wenye kuingiza watu 60,000 Umetumia billions 64 . Hili siojambo la kawaida kabisa .
Serikali ije na ufafanuzi wa kueleweka hapa.Nchi hii hazina imeshikwa na watu watata.ushshidi ni mwingi na uko Ikulu kwa miaka mitatu sasa kupitia taarifa za CAG kwa miaka mitatu mfululizo bila hatua stahiki kuchukuliwa.
Mafonda ya MV Magogoni bado hayajapona.
Madonda ya DP-WORLD ndio bafo yana Bandeji za hospitali.
Ngumi za wizi kimfumo serikalini na TAMISEMI hata Rais amezisikia na kuzitamka hivi Punde.
Yes wanapiga wanaweka kwenye Mabenki hulo viswa vya Mbali, then sisi tuko busy na Tanga na Simba, kwa kifupi tunapigwa sio kwa sababu ya viongozi wabovu bali kwa sababu ya Ujinga wa Watanzania
 
Tumeacha nchi ishikiliwe na genge la majizi na vibaraka wa mabeberu! Si mmemsikia Kikwete akisifia Bi kidawa kuwa nchi imetulia! Sasa ndo anakwiba kwa kushirikia na magenge ya kifisadi ya kimataifa!
 
Yes wanapiga wanaweka kwenye Mabenki hulo viswa vya Mbali, then sisi tuko busy na Tanga na Simba, kwa kifupi tunapigwa sio kwa sababu ya viongozi wabovu bali kwa sababu ya Ujinga wa Watanzania
Radio na television za Tanganyika ziko busy na Betting kuliko kutoa elimu na kuhabarisha jamii.
Tuko kwenye "State Capture"
 
Nimeshangaa,,uwanja wa wait elf 30 Kwa estimate za engineering kwa the hnologia za kisasa ni billion 98 inclusive VAT.Bahati mbayahizo pesa zinapelekwa mfuko wa hazina wa CCM kwa ajili ya kampeni
 
Bilioni 64 ya wakati huo; sasa ni kiasi gani?

Udogo wa uwanja haina maana kwamba lazima gharama ziwe chini. Inategemea mambo mengi, ikiwemo viwango.

Gharama za Arusha na Daslama ni tofauti. Arusha ni watu wa madini, Daslama uchumi wao unategemea mwendokasi, Kilimanjaro itokayo Kizimkazi (labda na Siitaksi za bilionea).

Kwani hamuoni kwamba shilingi imeshuka sana thamani?

Usikute hizo bilioni 200 ni kama dola milioni 9 tu!
 
Kuna wizi mkubwa sana. Lkn wizi huu umeruhisiwa na rais mwenyewe, amesema watu wale kwa urefu wa kamba zao.
 
Alafu ndio mnasema Simba na Yanga wajenge uwanja kweli? Watu wanaweza kuona wadhamini wa Simba na Yanga wanaishia kupiga maneno na uwanja hawajengi wakadhani wajinga. More aweze ujenzi wa billion 200??? Sio mchezo.
 
Serikali imeingia mkataba wa kuanza Ujenzi wa uwanja Mpya Jijini Arusha Maarufu kama Samia Suluhu Hassan Stadium ambao ni Mahsusi Kwa Ajili ya Maandalizi ya AFCON 2027.

Uwanja huo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 286.

Kazi iendelee 👇👇

View: https://youtu.be/q05ytnyfpa0?si=jLrsYa4X_7tKcjKO

============

Serikali kupitia wizara ya Sanaa ,Utamaduni na Michezo leo Machi 19, 2024 imesaini mkabata wa ujenzi wa Uwanja wa Dokta Samia Suluhu Hassani wenyewe thamani ya shilingi bilioni mia mbili na themanini na Sita ambao utatumika katika michuano ya mataifa Afrika AFCON 2027 inayoandaliwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Michezo Dokta Damasi Ndumbaro amesema Lengo la uwanja huo kujengwa mkoani Arusha ni kuchochea maendeleo ya sekta utalii kupitia michezo.
---

BILIONI 286 KUTUMIKA UJENZI WA UWANJA MPYA JIJINI ARUSHA

Serikali imesaini Mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 286 na kampuni ya China Construction Engineering Group (CRCEG) kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa mpira wa miguu Mkoani Arusha.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini Mkataba huo leo Machi 19, 2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 30,000 huku akibainisha kuwa uwanja huo utakuwa wa kisasa zaidi Afrika Mashariki.

Amesema Serikali itahakikisha ujenzi huo unafanywa kwa haraka kwa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 ikiwa ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema uwanja huo utachagiza kwa kiasi kikubwa utalii nchini kwa kuwa uwepo wa uwanja huo utakuwa chachu shughuli mbalimbali tofauti na mpira wa miguu kama vile mchezo wa riadha, biashara zitakazokuwa zinafanyika.

"Uwanja huu utakuwa na ubora wa hali ya juu kwani utakuwa na vyumba vya watu mashuhuri, tumefanya zoezi hili leo ambapo, Rais Samia wetu anatimiza miaka mitatu ya uongozi wake, amesema Dkt. Ndumbaro.

Aidha, ameipongeza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo kwa juhudi ilizofanya za kuhakikisha zoezi hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amemtaka Mkandarasi wa uwanja huo ahakikishe kuwa ujenzi huo unakamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

"Wakandarasi hakikisheni kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025 uwanja uwe umefikia kiwango kinachoridhisha na utekelezaji huo uanze haraka iwezekanavyo ikiwa ni maandalizi kuelekea katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON),"amesema.

Amesema Kamati itatoa ushirikiano kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kama ilivyokusudiwa akibainisha kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaitendea haki sekta ya michezo kama anavyofanya kwenye sekta nyingine akitoa wito kwa wakazi wa Arusha watunze miundombinu ya uwanja huo.


Huu ni miradi wa ccm kujipatia fedha kwa ajili ya uchaguzi ujao kilivyo kwa miradi mingi huko nyuma. Mfano ni majengo na miradi mingi ya nssf enzi za Dr Dau, jengo la bunge, UDOM nk. Uwanja wa mpira ukumbi usio na mambo mengi na gharama zake hazipaswi kubwa kubwa kiasi hicho. Uzuri hiyo ni taaluma yangu
 
Tumepigwa sana. Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa takriban 65 billioni na unachukua watu 60,000 na hata kama ulijengwa miaka 20 iliyopita bado gharama hiyo ni kubwa sana. Uwanja unaochukua watu 30,000 unajengwa kwa Tshs.286billioni?. Watueleze vitu vya ziada watakavyoweka na thamani ya shillingi dhidi ya dollar ili tulinganishe na gharama iliyotajwa.
 
Nimesoma na kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Serikali itajenga uwanja wa mpira utakaogharimu Tshs.286 billion kule Arusha.

Uwanja huu utaingiza jumla ya watu 30,000 kinyume na Uwanja wa Mkapa unaoingiza watu 65,000. Binafsi mimi ninapingana na gharama kubwa ya uwanja huu.

Nitoe mfano Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa takriban T.shs.65 billioni na inachukua watu 65,000 vipi leo uwanja unaochukua watu 30,000 kujengwa kwa Tshs.286 billioni?

Nashauri tuelezwe vitu vya ziada vitakavyokuwemo kwenye uwanja huo zaidi ule wa Mkapa. Pamoja na vitu kupanda bei na shillingi ya Tanzania kushuka dhidi ya dola ya Marekani bado naona gharama hiyo ni ya juu sana.
Huna akili
 
Back
Top Bottom