Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
BILIONI 4.6 ZA RAIS SAMIA ZAONDOA CHANGAMOTO YA MAJI JIMBO LA HAI
Serikali imefanikisha upatikanaji wa kiasi cha Sh Bil 4.6 kwa ajili ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi katika jimbo la Hai kwa kuboreshaji mradi wa maji wa Hai mjini ,Upanuzi wa mradi wa maji NIre- Masanma na Kaseki -Kyeri .
Mbali na miradi hiyo pia imo miradi ya umaliziaji wa ujenzi wa mradi wa maji Rundugai ,Upanuzi wa mradi wa maji Lyamungo -Umbwe , Ujenzi wa tanki lita 100,000,upanuzi wa maji machame kisereni – Urara na Ujenzi wa mradi wa maji Rundugai Kawaya .
Hayo yamo katika taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Hai ,taarifa iliyowasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo Saashisha Mafuwe wakati wa mkutano mkuu maalumu wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Dream Park nje kidogo yam ji wa Bomang’ombe