Bilioni 44.8 kujenga chuo cha kimataifa cha reli mkoani Tabora

Bilioni 44.8 kujenga chuo cha kimataifa cha reli mkoani Tabora

Serikali ya Tanzania imesema imetenga Shilingi Bilion 44.8, kwa ajili ya kuanza Ujenzi Chuo kikubwa cha Reli mkoani Tabora chenye kiwango cha Kimataifa kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Kupitia kipande cha Tabora-Isaka.

Taarifa hiyo imetolewa mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli (TRC), Bi, Amina Lumuli ambapo ameeleza chuo hicgo kinatarajia kujengwa katika eneo la Malabi lenye ukubwa wa ekari 183.1. Kata ya Cheyo Manispaa ya Tabora.
Chuo cha Reli?
Kinafundisha nini?
Kinatoa kozi gani?
Degree, Diploma au Certificate?
 
What a waste!
Hizo pesa ni bora zingetumika kuimarisha chuo cha reli Morogoro.

Na pale morogoro chuo kipo ila huwezi kujua kama kuna chuo!!! Na wana eneo zuri sana lakuweka chuo ila wanalima mahindi tu pale[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Chuo cha reli Moro kina 'shared facilities' na chuo cha ualimu Kigurunyembe kama vile viwanja vya michezo. Pia kuna karakana kubwa ya reli ambapo wanafunzi wangeweza kupata mafunzo kwa vitendo.
Siungi mkono hoja ya kujenga chuo kipya Tabora.

Hawa watu mkataba wa kwanza walishakosea, wale wajenzi wakutoka dar to moro ndo walitakiwa kujenga chuo matokeo yake wakazidiwa akili ivyo habari ya chuo ikawa haipo..... sasa hawa wa sasa ndo wamestukia ndo wakaona chuo kiwe huko tabora lakini ni ujuha wa hali ya juu
 
Ndio. Its now or never! Either chuo kijengwe Morogoro au kisijengwe kabisa ...

Pale moro walitakiwa waboreshe nakuonyesha kuna chuo, ila huwezi kujua kama kuna chuo cha reli morogoro...... hata ukifika karakana ni ngumu kujua kama kuna chuo pale!!!! Atlist basi wangejenga chuo kidogo pale moro
 
Ujenzi Chuo kikubwa cha Reli mkoani Tabora chenye kiwango cha Kimataifa kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Kupitia kipande cha Tabora-Isaka
Hapa umenivuruga sijaelewa nimetoka kapa yaan umemaanisha nini
 
Morogoro kile ni tawi tu kwa ajili ya ufundishaji wa mafundi wa vichwa vya treni na madereva.

Main campus ipo Tabora ndipo wanapo fundwa Station masters, Train guards, Carriage and wagons examiners, permanent way inspectors.

Hivyo hata mimi naamini vingeboreshwa zaidi.

Sasa moro chuo cha reli kipo wapi mkuu?
 
Waeleze waelewe hao pingapinga!
 
Unaenda kutumia hela nyingi kujenga chuo cha mambo ya RELI hiv tumerogwa? Au mie sijaelewa.?

Natoka napo toka naenda kusoma maswwla ya reli? Nielewesheni.

Mbili.. Mie nashauri kama kuna chuo kipo wakifanyie rehabilitation kiwe chuo chenye hadhi zaidi.
 
Sasa moro chuo cha reli kipo wapi mkuu?
Kimsingi tangu awali kipindi chuo kinajengwa kulikuwa ni Tabora bila shaka 1947.

Baadae kulianzwa kufundishwa kozi mbalimbali baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya afrika mashariki.

Sasa kutokana na kwamba karakana kuu ya vichwa vya treni (Diesel locomotives workshop complex) ilikuwa morogoro ilionekana fani za ufundi wa vichwa vya treni (Locomotive Engineering in Diesel Mechanical & Electrical) pia udereva (locomotives driving technology) zipelekwe kule ili wanafunzi kuwa deep zaidi katika practical ndiyo ikawa ni tawi la chuo cha reli.

Hivyo Main campus ni TABORA....
 
Ni ya kizamani. Huwezi ilinganisha na ya Moro...
Siyo ya kizamani ya Morogoro ni kubwa Afrika mashariki yote pia ndiyo karakana ambayo mambo yote hufanyika mule Corrective maintenances zote hadi Locomotives overhaul
 
Chuo cha Reli?
Kinafundisha nini?
Kinatoa kozi gani?
Degree, Diploma au Certificate?
Kuna kozi ni Diploma
1. Ordinary Diploma in Rail Transportation (Tabora)
2. Ordinary Diploma in Locomotive Engineering in Diesel electrical(Morogoro)

Certificate
1. Basic Technician certificate in Rail Transportation(Tabora)
2. Basic Technician certificate in Track technology(Tabora)
3. Basic Technician certificate in carriage and wagon technology(Tabora)
 
Ujinga

Kama kilimo wamekosa kuajiriwa hawa je?
Acha kudis mkuu fuatilia tangu 2020 ajira ngapi utumishi wanatangaza za TRC ijumaa tarehe 17/03/2023 wametangaza ajira. Treni ni muunganiko wa kichwa na mabehewa unajua kwa utaratibu wa kitaalamu treni inayovuta Tani 1200 ni mafundi wangapi walifanya inspection ya mabehewa tuchukulie 20 na mfundi wangapi walifanya inspection ya locomotive hizo fani ni maalumu kaka.

The same DMI wana taaluma zao popote huzikuti. Au watu wa Aviation.
 
Chuo cha reli Moro kina 'shared facilities' na chuo cha ualimu Kigurunyembe kama vile viwanja vya michezo. Pia kuna karakana kubwa ya reli ambapo wanafunzi wangeweza kupata mafunzo kwa vitendo.
Siungi mkono hoja ya kujenga chuo kipya Tabora.

Chuo cha Tabora unakijua ? Kwa taarifa yako cha moro ni campus tu ya Tabora mzee
 
Hapa ndipo akili zetu sisi waafrika tunapoamua kuziweka mahala.

Chuo kipo Morogoro kwanini kisiboreshwe na kupanuliwa ili kiwe cha kimataifa?

Moro ni campus tu acheni ujuaji chuo kipo Tabora
 
Morogoro ni mkoa wa vyuo. Vyuo vyote vipya na vya zamani vinatakiwa kujengwa Morogoro; The rest, I can not accept...

Icho kilichopo morogoro unajua kinatoa kozi ngapi ama unajishaua tu moro na Tabora Unajua wapi ni sehem ya kimkakati zaidi wa ki reli acha kuongea tu bila utafit Tabora ni sehem ya kimkakati ya kireli kuna njia nne pale...

Tabora-kigoma

Tabora- mwanza

Tabora-mpanda

Tabora-dom/dar

Nachuo cha kozi zote kipo Tabora na Tabora ni mazingira mazur sanaa ya mambo ya kireli mzee
 
Kimsingi tangu awali kipindi chuo kinajengwa kulikuwa ni Tabora bila shaka 1947.

Baadae kulianzwa kufundishwa kozi mbalimbali baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya afrika mashariki.

Sasa kutokana na kwamba karakana kuu ya vichwa vya treni (Diesel locomotives workshop complex) ilikuwa morogoro ilionekana fani za ufundi wa vichwa vya treni (Locomotive Engineering in Diesel Mechanical & Electrical) pia udereva (locomotives driving technology) zipelekwe kule ili wanafunzi kuwa deep zaidi katika practical ndiyo ikawa ni tawi la chuo cha reli.

Hivyo Main campus ni TABORA....

Ni sawa lakini sasa hawaoni umuhimu wakuweka chuo pale?
 
Back
Top Bottom