KERO Bima ya Afya ya Jeshi(JWTZ) haitusaidii Wanajeshi na Familia zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nyie wenzetu ni wanajeshi wa wapi wenye mishahara mbaka inakatwa huko kwenye bima tunaomba tuwafatilie tujue
 
Aliyekuwa Chief of Staff wenu Meja Jen.Marco Gaguti aliwaambia muachane na mitandao kumbe hamkuelewa.😀

Watu walikuwa wanapigania hadi hayo maslahi yenu nyie mnapelekewa school buses makambini kwenda kujaza mikutano ya kampeni za uchaguzi.

Kulia kupokezana,na mkistaafu njoeni uraiani muone mziki wa spika za JBL.😁
 
Hii si kweli, nina ushuhuda, kuna hosp kibao tena RRH zinapokea na wateja wanahudumiwa na madaktari bingwa na bi gwa bobezi....hilo eneo ulilopo hama...au mna misinformation
Nikiwa kama Mtumishi wa Afya na hata leo nimepokea wazee wawili hapa Kituoni wanahizi Form kwa uzoefu wangu mdogo wa miaka mi3 sasa kazini nikiri hii Bima wengi wanailalamikia sana

Nakupa hii scenario kwanza mkababa walioingia nao JwTZ ukiachana na vituo vyao vituo vilivyobaki vingi ni kuanzia RRH wengi hawana accsess ya kuona baadhi ya hospitali has zile za Private inampa usumbufu usio na sababu mgonjwa kuna mzee waliwahi toka Shelui akaja hadi kwa mshauri wa Mgambo Singida akapewa kibali afu akaenda Makiungu kufika huko akaambiwa hawapokei hiyo Bima mind you katoka shelui na kaambiwa Makiungu kuna huduma bora au kuna huduma yeye alitaka apate huko ikabidi arudi tena Singida Mjini akatibiwe Hospitali ya Mkoa ambako wanapokea
 
Hoja hii naomba isikilizwe, JWTZ wanapata shida sana hasa wazazi wao walioko mbali hakuna hospitali za jeshi.

Wanajeshi wasingekatwa pesa ya matibabu kwa sababu hawana mshahara. Nasikitika sana kwa nini wanawakata pesa ya bima ya afya nasikitika.
Ukaamua uje public
 
Changamoto yangu inahusu huduma za Bima ya Afya ya Jeshi (MHIF), ambayo imekuwa kero kwa wanachama na wategemezi wao.

Kwa mujibu wa malalamiko haya, mwanajeshi mwanachama hukatwa takribani Shilingi 51,000 kila mwezi kwa ajili ya bima hiyo. Hata hivyo, matumizi ya bima hiyo yamekuwa na changamoto, kwani hospitali zinazotambuliwa ni chache, hasa zile za Serikali.

Mara nyingi, ili mwanachama kupata huduma katika hospitali nyingine, anatakiwa kuanza katika kituo cha afya cha Jeshi na kupata barua ya rufaa (referral). Hata hivyo, kuna nyakati ambapo daktari huamua kutompatia rufaa mara moja na kumtaka mgonjwa kusubiri au kuendelea na matibabu katika kituo hicho.

Hali hii inazua maswali kadhaa: Kwa nini bima ya afya ya wanajeshi imetengwa na mfumo wa bima unaotumiwa na watumishi wengine wa Serikali? Kwa nini mwanachama analazimika kupewa hospitali maalumu za kwenda badala ya kuwa na uhuru wa kupata huduma katika hospitali zilizo ndani ya mtandao wa bima? Kwa nini hata wategemezi nao wanapaswa kufuata utaratibu huo wa kupata rufaa?

Aidha, changamoto nyingine ni upatikanaji mdogo wa madaktari bingwa katika baadhi ya hospitali za Jeshi, hali inayoweza kuwaathiri wanachama wanaohitaji huduma za kibingwa.

Tunaomba mamlaka husika zifanyie kazi changamoto hizi na kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa MHIF, ikiwemo sababu za kuwepo kwa taratibu hizi na hatua zinazochukuliwa kuboresha huduma kwa wanachama na wategemezi wao.

Wanajeshi na familia zao wanastahili kupata huduma bora za afya kwa wakati, bila kukumbana na urasimu usio wa lazima katika kupata matibabu.
 
Mkubali mkatae achananeni na hiyo BIMA tumieni NHIF hiyi itaendelea kuwacost sana
 
Ulipaswa ukalalamike kwenye mamlaka zenu huko sasa ukilalamika humu sisi wananchi hatuwezi kuwasaidia sie wenyewe yametushinda tunasubil kudra tu.
 
Iyo bima kuna upigwaji mwingi sana una bima ya jwtz ila bado una lazimik kuwakatia familia yako bima ya NHIF buree kabsa iyo bima
 
JWTZ ni Wapumbavu ndiyomaana kila mtu anawadharau.
 
Ni vzr kukumbushana kuwa JWTZ ndio moyo wa nchi. Hakuna sovereignty bila jeshi. Kwa vyovyote vile, taarifa za Jeshi ndizo number one top secret za nchi.

Hii ndio sababu ya askari kutokutumia bima za kiraia. Hoja kubwa ilikuwa ni shirika litakalopewa kazi ya kutoa huduma za bima kwa askari lingekuwa na taarifa ya nchi ina askari wangapi kila wakati, na rekodi ya matibabu ya familia zao. Kiusalama hili halikubaliki kabisa.

Kwahiyo ni vyema mkazoea kukubaliana na hali halisi. Hata kama kunachangamoto maboresho myafanye kupitia mifumo ya ndani, siyo hii yetu ya kiraia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…