Bimmer na Landcruiser V8

Ile sio Supra Ni BMW z4 iliyochangamka(iliyofunikwa) tu.Ni ujinga tu.
 
Waulize hizo LC 200 wamezipandia wapi?sanasana anaeiponda LC 200ukimuuliza anaishia kukwambia anamiliki harrier old model na magari ya dizaini hio.Nilishangaa mbuzi mmoja humu anaiponda Nissan Y62 huku akiulizia kama anaweza akapata gx110 kwa mil 4.

Lkn ukikuta wanaongelea ma Porsche,G-Wagon, Ferrari,GT-Continental,Roll Royce,Maserati, McLaren Kama vile walishawahi kuzipanda kumbe Ni mwendo wa kucheki reviews tu Kule YouTube.
 
Yes.. Unaweza kutoka Dar mpaka Mwanza na kesho ukageuza kwa spidi yako mwenyewe.. Ila njia nzima ufukuzane na 1vd-ftv wakati wewe una 100hp.. inline 4.. 1.6lt.. Kesho gari hata kuwaka haiwaki..
Kwani unadhani hawajui Hilo mkuu?Ni vile wameamua tu kubisha.Jiandae kwa Ligi hapo.
 
Wana wanajifariji sana wengi wamiliki wa gari chakavu za mjepenga
 
Wanatapatapa sana hao. Ndiyo maana nasema kuna watu huwa wanasifia au wananunua vitu kwa mihemko na mikumbo tu ili nao waonekane wanajua kumbe wanaigiza.
 
Thank you. Kuna comment niliwaambia hata hizo Y62 V8 ziko vizuri kuliko baadhi ya BMW sema tu kuna watu wanazisujudia sana Bimmer kama kitu gani sijui.

Kuna picha zilitumwa kwenye uzi fulani zinalinganishwa interior designs za latest BMW na Mercedes Benz ikaonekana ya Merceds Benz ndiyo iko bomba kuliko ya BMW.

Kuna watu wakawa wanasema aahh Bimmer zake mbio bana urembo tuwaachie hao wengine. Leo hii tena wanasema hakuna anayemfikia BMW hata kwenye interior designs teh.
 
Umemaliza na huu ndio ukweli, haitokaa Toyoda akaipiku BMW . Sema wapambe wa toyota wanakuwa wanalingamisha gari zisizo lingana mtu anakuja linganisha 3 Series na V8 Badala ya kulinganisha na BMW X5 M competition na hiyo V8 zao
Hata hiyo x5 huwezi kulinganisha na LC VX in terms of reliability. Kwenye mbio Beemer anaweza kumsumbua kidogo ila kwa safari ndefu kwa hizi barabara zetu za kuunga hapa na pale bado LC 200 aka Kilimo kwanza Hana mpinzani
 
Ukiendesha gari kwa fujo kwenye hizi barabara zetu kama vile upo autobahn lazima ukirudi upite pale jerry spare part kuuguza majeraha🤣🤣. Ila LC V8 ama hizi 100 series hazijali we piga shimo unavyoweza ni mwendo mdundo tu.
 
Ukiendesha gari kwa fujo kwenye hizi barabara zetu kama vile upo autobahn lazima ukirudi upite pale jerry spare part kuuguza majeraha🤣🤣. Ila LC V8 ama hizi 100 series hazijali we piga shimo unavyoweza ni mwendo mdundo tu.
Hahahahahah unaenda pale kinyonge kuchapiwa mkeka wa bush zako ulizochakaza kwenye rasta😅😅😅 usiombe ukakuta na shockup za Nissan mbovu pia utajuta😅
 
Hata hiyo x5 huwezi kulinganisha na LC VX in terms of reliability. Kwenye mbio Beemer anaweza kumsumbua kidogo ila kwa safari ndefu kwa hizi barabara zetu za kuunga hapa na pale bado LC 200 aka Kilimo kwanza Hana mpinzani
Aisee X5 haina tatizo kukeep up na Landcruiser.. Gari engine kubwa.. Na imetengenezwa kuwa segment moja na Landcruiser.. Toleo la kwanza E53 engine ndogo ina 3lts inline six na kuna options ya 4lts V8.. Kwahiyo ipo vizuri stamina.. Ukisema tutoke wote Dar Mwanza na Landcruiser haina shida kabisa ipo njema..!

Ishu yangu ni kusema 3 series itamkalisha Landcruiser.. Hapo ndio nakataa.. Zipo 3 series powerful na zipo 3 series weak.. E36 316i nayo ni 3 series.. Hii haiwezi mwendo wa Landcruiser kwa muda mrefu.. Toa facts za matuta.. Weka mkeka wa lami njia nzima..!

Na hii kitu imeshaongelewa.. Gari ndogo ya Toyota Passo dashboard inasoma 180..Gari kubwa ya Toyota 70 dashboard inasoma 180..wakienda umbali mrefu Passo hawezi kukeep up na 70 hata kama wote wana dashboard sawa..

Hapa naona watu wanatetea sababu logo imebadilika kutoka Toyota kwa BMW..!
Kupambana na Landcruiser unahitaji Engine kubwa sio logo ya BMW..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…