Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Mkuu haya maswall unayojiulza bila kuw na majb,
Kwangu mm ni kama Leo umekuja kwenye fikla zang inawezekn vp yaan !? Ni vyema tupate haya majb kw wajuv wa haya mambo!

Mkuu hakuna kitu kina exist from nowhere. Kila kitu kina mwanzo. Ukiitazama hii hoja ukiwa na mawenge ya imani za kuja huwezi kuwa huru kufikiri zaidi.

Kwa kutumia nadharia yangu ya kutazama, utagundua kuwa nadharia zote za uumbaji, misingi yake imejikita kwenye kudhani au assumption.

Nataka nitumie mfano mwepesi kuonyesha ni jinsi gani kiumbe choche hakiwezi kujua chanzo chake;

Mosi, kwa kanuni ya uumbaji taarifa ya jinsi kilivyo chanzo cha kiumbe chochote sio muhimu kwa kiumbe husika.

Pili, Kwa kanuni ya uumbaji/uundaji taarifa ya jinsi kiumbe hicho kilivyotokea ni siri kubwa kwa chanzo cha kiumbe hicho!

Kwa mfano sisi wanadamu kwa level ya teknolojia tuliopo fikia sasa tumetengeneza vitu mbali mbali vinavyo tumia teknolojia ya hali ya juu sana kiasi kwamba akifufuka mtu aliyefariki miaka 1700 atafikiri tupo sayari mpya ama hii ni sayari tofauti na iliyokuwepo kabla ya kufariki kwake!

Tuchukulie vyombo vyote vya moto iwe vinatumika majini, ardhini au angani ni sawa na viumbe hai. Kwa mfano gari ni chombo cha moto ambacho kina tumika ardhini na kinashahibiana sana na jinsi mwanadamu alivyo na jinsi anavyofanya kazi.

Mkuu unavyo litazama gari, utaelewa kuwa gari ni muunganiko wa vumbuzi mbali mbali muhimu zilizowekwa pamoja ili kutimiza lengo la kusafirisha watu au mizigo.

Kwa hapa duniani magari huundwa au hutengenezwa na kampuni mbali mbali. Kampuni ni ushirika wa watu wenye adhma, dhamira, mawazo, ujuzi au uweledi mbali mbali kwa ajili ya kutimiza lengo lao.

Kwa hiyo kampuni ya kutengeneza magari ndio chanzo (Mungu) cha gari lolote. Je, unaweza kuliuliza gari kuhusu chanzo chake likakueleza? Ukweli ni kwamba haliwezi, kwa sababu zifuatazo:

1. Hakuna umuhimu huo kwa sababu katika utumikaji wake halihitaji chanzo chake kuwepo.

2. Taarifa ya namna ya kulitumia au kulirekebisha ili liendelea kufanya kazi vizuri ipo kwenye kitabu cha maelezo.

3. taarifa ya jinsi lilivyotokea (footprint/masterplan) hiyo ni siri ya chanzo/kampuni dhidi ya vyanzo/makampuni shindani.

Mkuu vivyo hivyo ni ngumu kujua chanzo cha kiumbe hai chochote ama kupata footprint ya kiumbe hai kwenye kiumbe hicho! Ni siri kubwa mno ya chanzo husika!

Na ndio maana hatukutani na Mungu mtaani wala huyo Mungu kutusikiliza mubashara kutatua changamoto zetu, au kutuondolea vikwazo mara moja tuombapo.

Narudia tena malighafi na Teknolojia iliyotumika kuumba viumbe hai ili kutimiza lengo la mtandao wa mawasiliano kati ya dunia yetu hii na sayari yenye makazi ya vyanzo vyetu/Miungu yetu sio ya dunia hapa.

Mkuu usikose kuuliza kama hujaelewa. Nawasilisha.
 
Mkuu hakuna kitu kina exist from nowhere. Kila kitu kina mwanzo. Ukiitazama hii hoja ukiwa na mawenge ya imani za kuja huwezi kuwa huru kufikiri zaidi..
“Kila kitu kina chanzo” Kanuni hii inatengezea INFINITY
Kwamba aliye muumba binadamu na yeye kaumbwa nk nk

Lakini pia kulinganisha kiumbe hai chenye utashi kamili kama binadamu na gari au meli nadhani sio sahihi..... ni mfano mfu
Hakuna namna gari au bunduki zinaweza kujiuliza zimetoka wapi?
Binadamu anaunda gari kwa kutumia vitu ambavyo vimeumbwa tayari, haviundi from nowhere kama ambavyo tunajiuliza aliyeumba vitu vyote duniani ni nani nani alifanyaje?

Lakini pia gari au ndege inamuhitaji binadamu kwa asilimia 100 kufanya kila kitu ili litumike, yaani kaliunda ili alitumie kurahisisha shughuli zake...... binadamu anajitegemea mwenyewe

Ukweli ni kwamba HATUJUI na tunatafuta majibu mepesi kwa kumuumba Mungu na nadharia za kisayansi
 
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.

Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.

Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.

Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?

Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?

Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?

Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??

Mkuu mwanadamu ana mwanzo na mwisho ila tu hajui chanzo chake. Kwa namna ulivyo aanza kutoa maelezo yako ya awali ni dhahiri kuwa mifumo hiyo na namna inavyofanya kazi haiku tokea tu from nowhere. Ilitengenezwa kwa maarifa na teknolojia ya hali ya juu ili kwa ushirikiano iunde chombo kikamilifu kinacho jitegemea kutimiza kusudi maalum duniani.

Teknolojia iliyotumika kuumba viumbe hai ni ya kujizalisha au kujitengeneza ili kupunguza gharama ya uzalishaji na usafirishaji kuja hapa dunia, unaweza usinielewe hapo.

Kuhusu uwezo wa mwanadamu kuwa mkubwa kuliko viumbe wengine ni la makusudi kabisa ili kutimiza malengo maalum duniani.

Chukulia kwa mfano vyombo vya moto na mitambo alivyotengeneza na mwanadamu, kila kimoja kinatofautiana na kingine kimuundo, matumizi na program ya uendeshaji. Ndivyo utofauti ulivyo kwenye viumbe hai.

Kukufafanulia zaidi chombo cha kwenda kutafiti anga za juu kina program yenye muunganiko wa maarifa na teknolojia ya hali ya juu kuliko vyombo vya moto vilivyopo duniani. Hivyo ndio mfano wa mwanadamu alivyoumbwa kwa teknolojia ya hali ya juu tofauti na viumbe wengine.

Fikiria gharama inayotumika kutengeneza vyombo vya moto ikiwemo na vyombo vya kwenda kutafiti anga za juu, ukijumlisha gharama za usafirishaji, gharama kukiwezesha kukaa huko a gani na kadhalika ni kubwa mno.

Ndio maana watengenezaji/waumbaji wakaja na teknolojia ya kujizalisha na kujikuza kwa viumbe hai mahali vilipo. Hii inampunguzia muumbaji gharama na muda wa kutengeneza kitu hicho hicho na kukisafarisha kwenda kinapohitajika.
 
Kwani ni lazima kila kitu kilichopo kiwe kimetengenezwa?

Huu ulazima umeutoa wapi?

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mtengenezaji wake, Mungu ametengenezwa na nani?

Na mtengenezaji wa Mungu ametengenezwa na nani?

Na mtengenezaji wa "mtengenezaji wa Mungu" ametengenezwa na nani?

Mkuu kama sisi binadamu tunaweza kutengeneza kitu kikafanya kazi na hicho kitu tulicho kitengeneza kikatengeza kitu kingine kipya basi vivyo hivyo na binadamu alitengenezwa na kiumbe mwenye maarifa na teknolojia ya juu zaidi ya mwanadamu. Vivyo hivyo kuweka mnyororro wa uumbaji/uundaji kuelekea nyuma ya uumbaji!
 
Swali la kizushi

Hivi utofauti wa Lugha za binadamu upo tu hauna chanzo chake?

Nguvu aliyonayo binadamu dhidi ya viumbe vingine na mazingira ya ulimwengu hakuna chanzo chake?

Binadamu hana kusudi la kuwepo kwake duniani?

Kwa nini binadamu huzaliwa wakati Iko siku atakufa. Huu mchakato wa kuzaliwa mpaka kufa hauna maana yoyote ile?

Mkuu nitajitahidi kukujibu kama ifuatavyo:

1. Lugha ni mfumo wa mawasiliano, uliowekwa ndani ya mwanadamu na mtengezaji/muumbaji wake. Chanzo cha lugha ni chanzo cha mwanadamu.

Mkuu ukifuatilia utagundua kuwa lugha huzaliwa, hubadilika na pia hufa. Lugha hubadilika kutokana na mazingira, mazoea, utamaduni, mila, desturi, siasa, imani, muingiliano wa jamii, sayansi na teknolojia.

2. Binadamu ameumbwa kwa upekee na upendeleo maalum ndio maana na chimbuko la nguvu yake.

Binadamu ana chanzo chake ambacho ni kiumbe/chanzo (sio lazima kinafanana na alivyo binadamu) chenye maarifa na teknolojia ya hali ya juu na kinaishi kwenye sayari ya nyota nyingine kwenye anga letu (our universe ) au anga lingine tofauti na la kwetu.

3. Mkuu kusudi kubwa la binadamu na viumbe wengine duniani ni kuwezesha mawasiliano yakinifu kwenda kwa chanzo/muumba wake bila yeye kujijua. Binadamu tunatumika kama satellite au vyombo vya anga za mbali zinavyotumika kuwezesha mawasiliano hapa duniani.

4. Kwanza, binadamu ameumbwa na mfumo wa kujizalisha, kujikuza na hatimaye kufa. Hii ni kupunguza gharama ya uzalishaji kwa muumbaji wake.

Pili, binadamu ameumbwa kutokana na malighafi ambayo haipo hapa dunia. (sio udongo) Malighafi hiyo ina tabia ya kuharibika/kupoteza nguvu/kuchakaa/kuzeeka/kufa kadri muda unavyoenda.

Tatu, kwa kuwa kuna mfumo wa kujizalisha ndio maana watoto wanazaliwa kabla ya mtu kufa ili kuendeleza mfumo wa mawasiliano kwenda kwa muumbaji.
 
Mkuu nitajitahidi kukujibu kama ifuatavyo:

1. Lugha ni mfumo wa mawasiliano, uliowekwa ndani ya mwanadamu na mtengezaji/muumbaji wake. Chanzo cha lugha chanzo cha mwanadamu.

Mkuu ukifuatilia utagundua kuwa lugha huzaliwa, hubadilika na pia hufa. Lugha hubadilika kutokana na mazingira, mazoea, utamaduni, siasa, imani, muingiliano wa jamii, sayansi na teknolojia.

2. Binadamu ameumbwa kwa pekee na upendeleo ndio maana ya nguvu yake.

Binadamu ana chanzo chake ambacho ni kiumbe/chanzo (sio lazima kinafanana na alivyo binadamu) chenye maarifa na teknolojia ya hali ya juu na kinaishi kwenye sayari ya nyota kwenye anga letu (our universe ) au anga lingine tofauti na la kwetu.

3. Mkuu kusudi kubwa la binadamu na viumbe wengine duniani ni kuwezesha mawasiliano yakinifu kwenda kwa chanzo/muumba wake bila yeye kujijua. Binadamu tunatumika kama satellite au vyombo vya anga za mbali zinavyotumika kuwezesha mawasiliano hapa duniani.

4. Kwanza, binadamu ameumbwa na mfumo wa kujizalisha, kujikuza na hatimaye kufa. Hii ni kupunguza gharama ya uzalishaji kwa muumbaji wake.

Pili, binadamu ameumbwa kutokana na malighafi ambayo haipo hapa dunia. Malighafi hiyo ina tabia ya kuharibika/kupoteza kunguvu/kuchakaa/kuzeeka/kufa kadri muda unavyoenda.

Tatu, kwa kuwa kuna mfumo wa kujizalisha ndio maana watoto wanazaliwa kabla ya mtu kufa ili kuendeleza mfumo wa mawasiliano kwenda kwa muumbaji.

Mkuu wewe umejuaje kama binadamu kaumbwa kwa mpangilio ulio ueleza hapa?

Huyo muumbaji kaacha wapi haya maelezo yako?
 
Mbunifu huyo alitokea wapi?

Kabla ya kubuni hivi vitu, Huko aliko kuwa huyu "mbunifu" kulitoka wapi?

Hiyo sehemu aliyo kuwepo huyu mbunifu kabla haja anza ubunifu wake iliumbwa na nani?

Mbunifu huyu aliwezaje kutokea tu Vuuuuuuuuuuh!😄 From Nothing aka anza ubunifu?

Kwamba hakuwa sehemu yeyote ile?

Mkuu jibu unaweza kulipata kwa kutazama matokeo ya ubinifu wa binadamu mwenyewe na makusudi yake hapa duniani. Kwa mfano tazama miundo mbinu aliyoibuni, mifumo, mtambo, majengo, vyombo vya moto, vitu mbali na kadhalika.

Baada ya kuvitazama, sasa jiulize hivyo vitu ukiviuliza vinaweza kukueleza kinagaubaga kuhusu sura, maumbile, ubunifu, maarifa, ujuzi, teknolojia, uwezo au uwepo wa binadamu.

Jibu ni hapana, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwetu binadamu. Sisi ni vyombo/viumbe kutoka kwa muundaji/muumbaji/chanzo chetu.
 
Mkuu wewe umejuaje kama binadamu kaumbwa kwa mpangilio ulio ueleza hapa?

Huyo muumbaji kaacha wapi haya maelezo yako?

Mkuu kaa chini tafakuri kwa kina kwa kutazama viumbe hai, mazingira na fanya tafiti kuhusu anga letu utanipata vizuri.

Tahadhari: Usifanye hayo ukiwa na mawazo au hisia imani yoyote. Fanya huo utafiti ukiwa huru.
 
Mkuu jibu unaweza kulipata kwa kutazama matokeo ya ubinifu wa binadamu mwenyewe na makusudi yake hapa duniani. Kwa mfano tazama miundo mbinu aliyoibuni, mifumo, mtambo, majengo, vyombo vya moto, vitu mbali na kadhalika.

Baada ya kuvitazama, sasa jiulize hivyo vitu ukiviuliza vinaweza kukueleza kinagaubaga kuhusu sura, maumbile, ubunifu, maarifa, ujuzi, teknolojia, uwezo au uwepo wa binadamu.
Vitu hivyo havina ufahamu, utambuzi wala Akili ya kuhoji au kufikiri.

Binadamu tuna Akili, ufahamu na utambuzi wa kuhoji kitu chochote kile.

Chukulia mfano Robots,
Maroboti tumeyaunda wenyewe binadamu lakini hayawezi kufanya kazi bila idhini, ruhusa, command, amri na maagizo yetu sisi binadamu.

Lakini binadamu tunaweza kufanya kitu chochote kile kulingana na maamuzi yetu binafsi. Hata jambo baya binadamu anaweza fanya kwa kuamua tu.

Kiasi kwamba hata huyo muumbaji wetu binadamu unaye dai yupo, Hawezi kudhibiti au kuzuia maamuzi yetu binadamu.

Binadamu aki amua, kaamua kumbadilisha ni mpaka yeye mwenyewe aamue kubadili maamuzi yake, Lakini muumbaji huyo hawezi kumbadilisha binadamu huyu maamuzi automatically.

Lakini binadamu tuna uwezo wa ku control mashine na mifumo yote tuna i control kwa amri zetu.
Jibu ni hapana, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwetu binadamu. Sisi ni vyombo/viumbe kutoka kwa muundaji/muumbaji/chanzo chetu.
 
Mkuu kama sisi binadamu tunaweza kutengeneza kitu kikafanya kazi na hicho kitu tulicho kitengeneza kikatengeza kitu kingine kipya basi vivyo hivyo na binadamu alitengenezwa na kiumbe mwenye maarifa na teknolojia ya juu zaidi ya mwanadamu. Vivyo hivyo kuweka mnyororro wa uumbaji/uundaji kuelekea nyuma ya uumbaji!
Na huyo kiumbe mwenye maarifa na teknolojia ya juu zaidi ya mwanadamu, Alitengenezwa na nani?
 
Mkuu kaa chini tafakuri kwa kina kwa kutazama viumbe hai, mazingira na fanya tafiti kuhusu anga letu utanipata vizuri.

Tahadhari: Usifanye hayo ukiwa na mawazo au hisia imani yoyote. Fanya huo utafiti ukiwa huru.

Mkuu ukiisha kukaa ukatafakari ukapata jibu yupo aliyeumba utakwenda mbele zaidi.... na huyu mjuzi wa yote haya nani kamuumba?

Hayo yote ni mawazo yako tu ila ukweli ni kwamba HATUJUI

NO BODY KNOWS
 
Vitu hivyo havina ufahamu, utambuzi wala Akili ya kuhoji au kufikiri.

Binadamu tuna Akili, ufahamu na utambuzi wa kuhoji kitu chochote kile.

Chukulia mfano Robots,
Maroboti tumeyaunda wenyewe binadamu lakini hayawezi kufanya kazi bila idhini, ruhusa, command, amri na maagizo yetu sisi binadamu.

Lakini binadamu tunaweza kufanya kitu chochote kile kulingana na maamuzi yetu binafsi. Hata jambo baya binadamu anaweza fanya kwa kuamua tu.

Kiasi kwamba hata huyo muumbaji wetu binadamu unaye dai yupo, Hawezi kudhibiti au kuzuia maamuzi yetu binadamu.

Binadamu aki amua, kaamua kumbadilisha ni mpaka yeye mwenyewe aamue kubadili maamuzi yake, Lakini muumbaji huyo hawezi kumbadilisha binadamu huyu maamuzi automatically.

Lakini binadamu tuna uwezo wa ku control mashine na mifumo yote tuna i control kwa amri zetu.

Mkuu usemayo ni kweli, ila unasahau kuwa unaviona hivyo vitu kutokuwa na uhai kwa sababu unavitazama from the point of view of being their creator/maker/source/manufacturer.

Hebu fikiria aliyetutengeneza,/tuumba anatuonaje assuming kuwa kuwa sisi ni vyombo/viumbe vyake! Binadamu anafanya kazi kwa kufuata program maalum ya uendeshaji (Operating system) aliyowekewa na muundaji!/chanzo/muumbaji. Na hiyo program (Os) ni standard kwa kila binadamu.

Kila kiumbe hai kina programu yake maalum na ni standard kwa kila kiumbe cha aina hiyo.
 
Mkuu ukiisha kukaa ukatafakari ukapata jibu yupo aliyeumba utakwenda mbele zaidi.... na huyu mjuzi wa yote haya nani kamuumba?

Hayo yote ni mawazo yako tu ila ukweli ni kwamba HATUJUI

NO BODY KNOWS

Mkuu, kama umefuatilia maelezo yangu nimeeleza mara nyingi kuwa sisi binadamu hatuwezi kujua hilo. Ila haimishi kuwa hakuna chanzo chetu!
 
Hiyo sayansi si inatumia uwezo wa binadamu kwenye kutengeneza (formulate) nadharia mbalimbali?

Mpaka sasa sayansi miaka Kwa miaka imethibitishwa kuwa nadharia zake kadhaa wa kadhaa hazikuwa sahihi.

Kabla ya kutengeneza hizo nadharia zake ambazo si sahihi kwa 100%, mwanasayansi hana uwezo wa kujijua yeye asili na chanzo chake kwa kuwa yeye si chanzo cha kuwa kwake.

Kwa ivo kuna kutafsiri mazingira na kuna kujua chanzo cha mazingira husika.

Kwanza Ili upate jibu la swali ni lazima ukubali kanuni ya ukokotozi wa swali husika.

Kujua chanzo na asili ya binadamu ni Lazima kuwe nje ya zile njia kuu (sita?) Za fahamu.

Ni lazima ujiweke kwenye Hali ya kuamini kuwa kwa sayansi haiwezekani kujua chanzo na asili ya binadamu.

Baada ya hapo tafuta maarifa toka ndani mwako (inner self) kujua wewe umekuwaje binadamu.

Mkuu, you almost got there!
 
Back
Top Bottom