ZionGate
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 6,362
- 2,991
Nasubiria jibu konk hapaKuamua huu ni ukweli ama uongo kwenye hoja hii nani anaamua!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nasubiria jibu konk hapaKuamua huu ni ukweli ama uongo kwenye hoja hii nani anaamua!!
Nasubiria jibu konk hapa
Huyo bwana wako aliyesema kaumba vitu Kwa siku 6 alafu siku ya 7 akapumzika ."Mimi ni alpha na omega, mwanzo na mwisho" asema Bwana.
Alikua anafirahia uumbaji wakeHuyo bwana wako aliyesema kaumba vitu Kwa siku 6 alafu siku ya 7 akapumzika .
Hiyo siku aliyepumzika alikuwa anafanya nn
Ana chekeleaAlikua anafirahia uumbaji wake
Kama ni hivyo basi 1 Day naye atakufa ,coz ni Omega"Mimi ni alpha na omega, mwanzo na mwisho" asema Bwana.
Mkuu haya maswall unayojiulza bila kuw na majb,
Kwangu mm ni kama Leo umekuja kwenye fikla zang inawezekn vp yaan !? Ni vyema tupate haya majb kw wajuv wa haya mambo!
“Kila kitu kina chanzo” Kanuni hii inatengezea INFINITYMkuu hakuna kitu kina exist from nowhere. Kila kitu kina mwanzo. Ukiitazama hii hoja ukiwa na mawenge ya imani za kuja huwezi kuwa huru kufikiri zaidi..
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.
Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.
Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.
Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?
Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?
Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?
Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??
Kwani ni lazima kila kitu kilichopo kiwe kimetengenezwa?
Huu ulazima umeutoa wapi?
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mtengenezaji wake, Mungu ametengenezwa na nani?
Na mtengenezaji wa Mungu ametengenezwa na nani?
Na mtengenezaji wa "mtengenezaji wa Mungu" ametengenezwa na nani?
Swali la kizushi
Hivi utofauti wa Lugha za binadamu upo tu hauna chanzo chake?
Nguvu aliyonayo binadamu dhidi ya viumbe vingine na mazingira ya ulimwengu hakuna chanzo chake?
Binadamu hana kusudi la kuwepo kwake duniani?
Kwa nini binadamu huzaliwa wakati Iko siku atakufa. Huu mchakato wa kuzaliwa mpaka kufa hauna maana yoyote ile?
Mkuu nitajitahidi kukujibu kama ifuatavyo:
1. Lugha ni mfumo wa mawasiliano, uliowekwa ndani ya mwanadamu na mtengezaji/muumbaji wake. Chanzo cha lugha chanzo cha mwanadamu.
Mkuu ukifuatilia utagundua kuwa lugha huzaliwa, hubadilika na pia hufa. Lugha hubadilika kutokana na mazingira, mazoea, utamaduni, siasa, imani, muingiliano wa jamii, sayansi na teknolojia.
2. Binadamu ameumbwa kwa pekee na upendeleo ndio maana ya nguvu yake.
Binadamu ana chanzo chake ambacho ni kiumbe/chanzo (sio lazima kinafanana na alivyo binadamu) chenye maarifa na teknolojia ya hali ya juu na kinaishi kwenye sayari ya nyota kwenye anga letu (our universe ) au anga lingine tofauti na la kwetu.
3. Mkuu kusudi kubwa la binadamu na viumbe wengine duniani ni kuwezesha mawasiliano yakinifu kwenda kwa chanzo/muumba wake bila yeye kujijua. Binadamu tunatumika kama satellite au vyombo vya anga za mbali zinavyotumika kuwezesha mawasiliano hapa duniani.
4. Kwanza, binadamu ameumbwa na mfumo wa kujizalisha, kujikuza na hatimaye kufa. Hii ni kupunguza gharama ya uzalishaji kwa muumbaji wake.
Pili, binadamu ameumbwa kutokana na malighafi ambayo haipo hapa dunia. Malighafi hiyo ina tabia ya kuharibika/kupoteza kunguvu/kuchakaa/kuzeeka/kufa kadri muda unavyoenda.
Tatu, kwa kuwa kuna mfumo wa kujizalisha ndio maana watoto wanazaliwa kabla ya mtu kufa ili kuendeleza mfumo wa mawasiliano kwenda kwa muumbaji.
Mbunifu huyo alitokea wapi?
Kabla ya kubuni hivi vitu, Huko aliko kuwa huyu "mbunifu" kulitoka wapi?
Hiyo sehemu aliyo kuwepo huyu mbunifu kabla haja anza ubunifu wake iliumbwa na nani?
Mbunifu huyu aliwezaje kutokea tu Vuuuuuuuuuuh!😄 From Nothing aka anza ubunifu?
Kwamba hakuwa sehemu yeyote ile?
Mkuu wewe umejuaje kama binadamu kaumbwa kwa mpangilio ulio ueleza hapa?
Huyo muumbaji kaacha wapi haya maelezo yako?
Mkuu jibu unaweza kulipata kwa kutazama matokeo ya ubinifu wa binadamu mwenyewe na makusudi yake hapa duniani. Kwa mfano tazama miundo mbinu aliyoibuni, mifumo, mtambo, majengo, vyombo vya moto, vitu mbali na kadhalika.
Vitu hivyo havina ufahamu, utambuzi wala Akili ya kuhoji au kufikiri.Baada ya kuvitazama, sasa jiulize hivyo vitu ukiviuliza vinaweza kukueleza kinagaubaga kuhusu sura, maumbile, ubunifu, maarifa, ujuzi, teknolojia, uwezo au uwepo wa binadamu.
Jibu ni hapana, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwetu binadamu. Sisi ni vyombo/viumbe kutoka kwa muundaji/muumbaji/chanzo chetu.
Na huyo kiumbe mwenye maarifa na teknolojia ya juu zaidi ya mwanadamu, Alitengenezwa na nani?Mkuu kama sisi binadamu tunaweza kutengeneza kitu kikafanya kazi na hicho kitu tulicho kitengeneza kikatengeza kitu kingine kipya basi vivyo hivyo na binadamu alitengenezwa na kiumbe mwenye maarifa na teknolojia ya juu zaidi ya mwanadamu. Vivyo hivyo kuweka mnyororro wa uumbaji/uundaji kuelekea nyuma ya uumbaji!
Mkuu kaa chini tafakuri kwa kina kwa kutazama viumbe hai, mazingira na fanya tafiti kuhusu anga letu utanipata vizuri.
Tahadhari: Usifanye hayo ukiwa na mawazo au hisia imani yoyote. Fanya huo utafiti ukiwa huru.
Vitu hivyo havina ufahamu, utambuzi wala Akili ya kuhoji au kufikiri.
Binadamu tuna Akili, ufahamu na utambuzi wa kuhoji kitu chochote kile.
Chukulia mfano Robots,
Maroboti tumeyaunda wenyewe binadamu lakini hayawezi kufanya kazi bila idhini, ruhusa, command, amri na maagizo yetu sisi binadamu.
Lakini binadamu tunaweza kufanya kitu chochote kile kulingana na maamuzi yetu binafsi. Hata jambo baya binadamu anaweza fanya kwa kuamua tu.
Kiasi kwamba hata huyo muumbaji wetu binadamu unaye dai yupo, Hawezi kudhibiti au kuzuia maamuzi yetu binadamu.
Binadamu aki amua, kaamua kumbadilisha ni mpaka yeye mwenyewe aamue kubadili maamuzi yake, Lakini muumbaji huyo hawezi kumbadilisha binadamu huyu maamuzi automatically.
Lakini binadamu tuna uwezo wa ku control mashine na mifumo yote tuna i control kwa amri zetu.
Mkuu ukiisha kukaa ukatafakari ukapata jibu yupo aliyeumba utakwenda mbele zaidi.... na huyu mjuzi wa yote haya nani kamuumba?
Hayo yote ni mawazo yako tu ila ukweli ni kwamba HATUJUI
NO BODY KNOWS
Hiyo sayansi si inatumia uwezo wa binadamu kwenye kutengeneza (formulate) nadharia mbalimbali?
Mpaka sasa sayansi miaka Kwa miaka imethibitishwa kuwa nadharia zake kadhaa wa kadhaa hazikuwa sahihi.
Kabla ya kutengeneza hizo nadharia zake ambazo si sahihi kwa 100%, mwanasayansi hana uwezo wa kujijua yeye asili na chanzo chake kwa kuwa yeye si chanzo cha kuwa kwake.
Kwa ivo kuna kutafsiri mazingira na kuna kujua chanzo cha mazingira husika.
Kwanza Ili upate jibu la swali ni lazima ukubali kanuni ya ukokotozi wa swali husika.
Kujua chanzo na asili ya binadamu ni Lazima kuwe nje ya zile njia kuu (sita?) Za fahamu.
Ni lazima ujiweke kwenye Hali ya kuamini kuwa kwa sayansi haiwezekani kujua chanzo na asili ya binadamu.
Baada ya hapo tafuta maarifa toka ndani mwako (inner self) kujua wewe umekuwaje binadamu.