Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho


Watu tunataka kumjua huyo muumbaji na umemjua vipi?
Wewe upo busy kueleza jinsi muumba alivyo tuumba kwa kufananisha na tulivyo viunda........ totally two different things

Kunatofauti kati ya kuumba na kuunda
Kuumba ni kutengeneza kitu from nothing
Kuunda ni kuchukua vitu vilivyopo na kuviunga kupata kitu

Unaulizwa umejuaje unaanza Hadithi za fikiria nanikaumba huu mpangilio?

Kuna dhana zaidi ya milioni za nani kaumba ulimwengu na vyote
Wengine Mungu kwasababu vitabu vimeandika, wengine wanadai wameongea na mungu, wengine wameota maono nk nk

Wewe umejuaje Muumba yupo na ametuumba akatuwekea (operating system) kama pc?
 

Mkuu tafakari juu ya hoja yangu kama unaona haina mantiki unaacha nayo. Hayo ni mawazo yangu, sio lazima ukubaliane nayo.
 
Wanashangaza sana Hawa Atheists!

Wao wanaamini Kuunda ila hawaamini Kuumba [emoji38].

We are the Image of God

Mungu anaumba

Wanaadamu tuna Unda.

You can't Ignore God the Almighty!

Ni ufinyu wa Kufikiri
Yeye Mungu aliumbwa na nani? Huyo alimuumba
Na yeye aliumbwa na nani, na huyu aliewaamba hawa aliumbwa na nani? Sisi ni image ya mungu kivipi eleza hili? Kwa undani pia watu tuelewe , mnatuacha gizani mnoo
 
Umekosa mifano hadi ufananishe binadamu na vyombo ambavyo katengeneza binadamu kweli ? Ungeangalia basi hata sifa ya kila kimoja, ( Binadamu na hilo gari ) Mfano wako hauna maana
 
Umekosa mifano hadi ufananishe binadamu na vyombo ambavyo katengeneza binadamu kweli ? Ungeangalia basi hata sifa ya kila kimoja, ( Binadamu na hilo gari ) Mfano wako hauna maana

Mkuu mimi nimetoa mfano huo ili kurahisisha majibu ya swali liloulizwa. Naona umehamaki kabla ya kutafakari.

Wote tunajaribu kutafuta majawabu, tunategemea kama hukubaliani na mtazamo wangu uweke wa kwako ili tujifunze kwa pamoja.

Kumalizia, sisi ni vyombo tu mbele ya chanzo chetu kama hayo magari yalivyo vyombo mbele yetu mkuu wangu!
 
Umekosa mifano hadi ufananishe binadamu na vyombo ambavyo katengeneza binadamu kweli ? Ungeangalia basi hata sifa ya kila kimoja, ( Binadamu na hilo gari ) Mfano wako hauna maana

Tatizo la huyu muungwana ni kwamba anashindwa kutofautisha kati ya KUUMBA na KUUNDA

Lakini pia anashindwa kutofautisha kati ya Living things na None living things

Kumfananisha kiumbe hai kama binadamu mwenye utashi na kifaa kama gari au jembe ni kukosa MANTIKI kabisa
 
Nimejifunza sana, hii mada na maoni ya watu wengi, ni kitu ambacho kimesisimua sana, kimehojiwa, kudadisiwa na watu makini sana humu, kuhusu uwepo wa mungu, mimi natharia yangu ilikua mungu ni siri kubwa sana, binadamu hajuwi hata ile moja kuhusu, uumbaji na vilivyoko. Mfano mdogo tu chawa wanavyotokea mazingira ya uchafu ndani ya nguo ya binadamu, na wanakua na uhai??
 
Utashi Wa binadamu unatokana na nini??
 
Umezungumza jambo muhimu Sana.
Mfano Tu Mende anavyotokea kwenye uchafu wa chakula,chooni kwenye giza.

Kama mungu katuumba yeye Kwanini afanye Siri , sisi waja wake tumjue?

Je kuna watu wanaficha tusimjue mungu,
Je kuwepo Kwa mungu si kunatakiwa kubainika Kwa kila mwanadamu
 
Kwani kumjua Mungu kwako wewe kukoje??
 
Mimi naona jambo, la kuumbwa na nani binadamu? wapo viumbe wanaotuzidi mbali walitumia madini ghali sana kutuumba ili tuwe tunajidhalisha kuepusha ghalama, kwa madini haya , kama sisi binadamu tunavyofanya kwenye sayansi na teknolojia za leo, pima tu binadamu wa zamani, waliokufa bila uwepo wa magari, ndege, na n.k. Endapo watafufuka leo watajiuliza nani kaumba haya magari watajifkiria wao mungu, hata pia zile nyota za angani, wataalamu wapo sisi ambayo hatujuwi tutajiuliza maswali bila majibu ila ukweli wapo. MUNGU NI KITU KUZIDI UWEZO KWA VITU VINGINE.
 
Mkuu nakupa maua yako, angalau umenielewa nadharia yangu, pokea maua haya: 💐
 
Uumbaji wa binadamu siyo suala tata Bali hugeuzwa tata na wasioamini uumbaji.
 
Watu tuna tabia ya kusema....."Kichwa changu,.Moyo wangu,...Mguu wangu,..Akili yangu, figo yangu na kadhalika......Swali la Kujiuliza Je,Mtu hasa ni Nani,? Mtu ambae hapo anaongea kuonyesha kwamba yeye anamiliki hivyo viungo vilivyopo kwenye mwili wake.

Sijui naeleweka,? Fikiria mtu akitumia kauli hii ➡️ "Mwili wangu unauma" .....Hapa ndiyo swali langu linapoibuka kwamba je Mtu ni nini? Mpaka ajione kama yeye na mwili wake ni two separate entities.?


Naamini still nipo ndani ya mada husika Kwasababu mada inamuhusu kiumbe Mtu,..wajuzi tujaribu kujadiliana juu ya hili maana binafsi limenifikirisha na huenda majibu yake ni mepesi sana.

Ahsanteni.
 
Sidhani kama mwanadamu anakusudi la specific la kuwepo duniani. Kila nachokifanya ni kwa ajiri ya uhai wake yeye mwenyewe. Binadamu huchakugua kitu gani afanye,nanna gani awe,hivyo hutengeneza kusudi lake yeye mwenyewe.
"existence precedes essence" means that a personality is not built from a previously designed model or for a precise purpose, because it is the human being who chooses to engage in such enterprise..

Tofauti na vitu vingine vingi kama gari, limetengenezwa kwa kusudi maalum,hivyo "Essence precedes existence"

Lakini binadamu kuexist kwanza then hufanya makusudi yake mwenyewe..
 
Since mwanadamu kuexist kwanza then kufanya maamuzi na makusudi yake mwenyewe,na ameubwa kwa mfano wa Mungu. SO tunaweza sema kila mtu anaUMungu ndani yake ,mawazo hutoka ndani ya mtu na yeye huchagua kitu gani afanye au asifanye kutokana na experience na mazingira.

Since we got free will,means we are our own God.
Mtu huzalwa mwisho kufa,na wengine kuzaliwa,,dunia haina mwisho mtu akifa amekufa hakuna maisha mengine kama tunavyohubiriwa,.

Ulimwengu upo na utaendelea kuwepo milele..If otherwise kuna muumbaji ambae haingilii kabisa maisha ya mwanadamu,kwa sababu kama anaingilia then wanadamu hatuna free will of choice.
Na kama dunia ina mwisho na hukumu,basi mzani pekee utakua wa Mema na mabaya.Coz hatuitaji dini au mtu yeyote kutambua jambo jema au baya nafsi huuzunika na kufurai.
 
Ndg Alien, ili upate kujua na kufahamu binadamu ametoka wapi na kusudio la uwepo wake, hauna budi kupitia maandiko mbali mbali. Maandiko haya yatahusisha vyanzo vyote vya imani zetu za dini mbali mbali ikiwepo na tafiti za kisayansi, za awali na za wakati huu.
Kwa upande wa dini zetu zote, chimbuko la imani hizi ni toka enzi za tawala za Wa - Sumerian. Hawa walitawala zama zile, waliandika maandiko mengi ambayo sasa ndiyo msingi wa imani za dini zote duniani na pia chanzo cha technologies zote tunazozitumia leo hii, na bado tuu mwanzo tu mwa maarifa ( technologies) waliokuwa nazo. Haya yote yaliachwa ktk maandiko ya vibao (tablets) nyingi, tangu za chanzo cha binadamu, utawala, dini, sciences, na maarifa mengi mengi sana! Ndiyo maana, hawa wenzetu Wazungu waling'ang'ania kufanya utafiti wa kuchimbua sehemu mbali mbali za kale kwa gharama kubwa sana! Hivi kweli huwa hamjiulizi tu, kwa nini hawa jamaa wali - hung'ang'ana sana katika tafiti kale?
Haya, kwa ufupi sana,
Chanzo cha binadamu ni matokea ya cloning toka kwa viumbe wa sayari ingine walipofika katika sayari ya "Dunia" wakiwa katika harati zao za kutafuta kitu cha kuponya anga la sayari yao isidhurike na mionzi ovu. Ndipo wakagundua kuwa sayari yetu, yaani DUNIA inayo hayo madini mengi sana.
Walitua na kuanza uchimbaji wa hayo madini kwa zana zao bora sana, huku wakitumia nguvu kazi toka miongoni mwa viumbe wenzao. Waliendekea hivyo hadi viumbe wenzao wakachoshwa na kazi hizo nzito za uchimbaji madini, ndipo wakubwa wao walipokaa (wakiwa ktk sayari hii hii ya dunia) na kuona kuwa kuna wanyama/hayawani, kwa mbali, wanao ufanano na wao. Ndipo walipoanza ulinganisho wa DNA zao na za hao. Walifanya majaribio hayo ya kimaabara mara nyingi tu, ndipo walipofikia uamuzi wa DNA manipulation, kuchanganya zao na za hao wanyama/ hayawani.
Matokeo yake ni kupata mbadala wa wafanyakazi waliotokana na zao la kia maabara. Lengo likiwa ni kuwapunguzia uzito wa kazi viumbe wenzao
Kumbe basi, utakuwa umepata chanzo halisi cha binadamu na lengo/ kusudio lake la uwepo wake hapa duniani.
NB: Kwa MTANZANIA ukitaka umnyime kitu, basi mwambie asome, hapo umempoteza kabisa, kwani ni mvivu mno wa kusoma! Mwisho, imeandikwa, "" Mshike sana ELIMU kwani....,.......... !
Mengi sana utayapata toka hizo tablets za Wa -Sumerians, hasa ukitembelea maktaba za mambo kale pale Uingereza (London) na zile za Ujerumani, omba uzisome, nyingi zipo coded na ktk lugha kale, hivyo unahitaji utalaam wa aina yake ili uyaelewe. Hapa MTANZANIA tumepigwa na kitu kizito sana kichwani na ktk paji la uso!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…