Ndg Alien, ili upate kujua na kufahamu binadamu ametoka wapi na kusudio la uwepo wake, hauna budi kupitia maandiko mbali mbali. Maandiko haya yatahusisha vyanzo vyote vya imani zetu za dini mbali mbali ikiwepo na tafiti za kisayansi, za awali na za wakati huu.
Kwa upande wa dini zetu zote, chimbuko la imani hizi ni toka enzi za tawala za Wa - Sumerian. Hawa walitawala zama zile, waliandika maandiko mengi ambayo sasa ndiyo msingi wa imani za dini zote duniani na pia chanzo cha technologies zote tunazozitumia leo hii, na bado tuu mwanzo tu mwa maarifa ( technologies) waliokuwa nazo. Haya yote yaliachwa ktk maandiko ya vibao (tablets) nyingi, tangu za chanzo cha binadamu, utawala, dini, sciences, na maarifa mengi mengi sana! Ndiyo maana, hawa wenzetu Wazungu waling'ang'ania kufanya utafiti wa kuchimbua sehemu mbali mbali za kale kwa gharama kubwa sana! Hivi kweli huwa hamjiulizi tu, kwa nini hawa jamaa wali - hung'ang'ana sana katika tafiti kale?
Haya, kwa ufupi sana,
Chanzo cha binadamu ni matokea ya cloning toka kwa viumbe wa sayari ingine walipofika katika sayari ya "Dunia" wakiwa katika harati zao za kutafuta kitu cha kuponya anga la sayari yao isidhurike na mionzi ovu. Ndipo wakagundua kuwa sayari yetu, yaani DUNIA inayo hayo madini mengi sana.
Walitua na kuanza uchimbaji wa hayo madini kwa zana zao bora sana, huku wakitumia nguvu kazi toka miongoni mwa viumbe wenzao. Waliendekea hivyo hadi viumbe wenzao wakachoshwa na kazi hizo nzito za uchimbaji madini, ndipo wakubwa wao walipokaa (wakiwa ktk sayari hii hii ya dunia) na kuona kuwa kuna wanyama/hayawani, kwa mbali, wanao ufanano na wao. Ndipo walipoanza ulinganisho wa DNA zao na za hao. Walifanya majaribio hayo ya kimaabara mara nyingi tu, ndipo walipofikia uamuzi wa DNA manipulation, kuchanganya zao na za hao wanyama/ hayawani.
Matokeo yake ni kupata mbadala wa wafanyakazi waliotokana na zao la kia maabara. Lengo likiwa ni kuwapunguzia uzito wa kazi viumbe wenzao
Kumbe basi, utakuwa umepata chanzo halisi cha binadamu na lengo/ kusudio lake la uwepo wake hapa duniani.
NB: Kwa MTANZANIA ukitaka umnyime kitu, basi mwambie asome, hapo umempoteza kabisa, kwani ni mvivu mno wa kusoma! Mwisho, imeandikwa, "" Mshike sana ELIMU kwani....,.......... !
Mengi sana utayapata toka hizo tablets za Wa -Sumerians, hasa ukitembelea maktaba za mambo kale pale Uingereza (London) na zile za Ujerumani, omba uzisome, nyingi zipo coded na ktk lugha kale, hivyo unahitaji utalaam wa aina yake ili uyaelewe. Hapa MTANZANIA tumepigwa na kitu kizito sana kichwani na ktk paji la uso!