Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Mimi point yangu ni kwamba, Dunia na Binadamu havina mwanzo wowote ule.

Binadamu wapo tu hawana mwanzo wala mwisho.

Na ulimwengu hivyo hivyo.

Hakuna chanzo chochote kile cha kidini au kisayansi kilicho umba ulimwengu na Binadamu.

Ulimwengu na Binadamu vipo tu havina mwanzo wala mwisho.
🤔
 
Mkuu mimi sijui chanzo cha dunia

Scriptures za kidini zimejaa hekaya tupu na zinapingana kwasababu zimeandikwa na watu tu kama wewe

Sayansi haijui, ilichofanya ni kutengeneza THEORIES tu

Scriptures na sayansi wanatofautiana sana

Mimi ni muumini mzuri wa sayansi lakini Napata tabu sana kuanza kutumia theory za kisayansi na imani za vitabu kujua ulimwengu umefanyikaje
Absolutely Time, absolutely Space,
Ila Mimi naona Time doesn't exist
 
Hana mwanzo hana mwisho siamini, mwanzo wangu ni wazazi, nao wazazi wana mwanzo, ukienda kwa mfumo huo utakuta kuna mwanzo ambao hauna mwanazo, ulioanzisha binadamu na ni Muumba.
 
Uuambaji uliofanikishwa na Supreme power umebase katika imani, utaelewa vizuri ukisoma mwenyewe kupitia vitabu vya dini. Umeenda mbali na kuelezea hata chanzo cha mtu, kwani alitokana na Supreme energy, hivyo huyo mtu akabeba sifa za kuishi nje ya muda(umilele), kwani hiyo Supreme power ilikuwepo hata kabla ya muda na itaendelea kuwepo hata baada ya muda. Hii ni kwa mujibu wa theory za dini.

Uumbaji uliobase kwa theory za Big bang umebase zaidi kwa logic ambapo unaonesha muunganiko wa tiny particals(atoms) kutengeneza object, na kwasababu particles zina masses hivyo zinakuwa affected by gravity, mwisho wake inatokea object kama stars, human being and so on. Lakini pia bado kuna dark matter nyingi tu still ni fumbo kwa science.

Sasa kwa theory zote za science na dini ukiziangalia kwa makini zinashabiiana na pia zinatofautiana. Mimi ukiweza ku verify kuwa kuna object inayoweza kuishi nje ya muda( umilele) nitakubaliana na wewe kuwa ulimwengu hauna chanzo.
Absolutely Time, absolutely Space,
Ila Mimi naona Time doesn't exist
 
Una hoja mkuu ebu itetee.
Time ya kwenye mwezini ni tofauti na Mars, earth, Jupiter.
Hapa duniani tumejiwejea Muda, Muda wa kufirika Tu, Ndio maana DK, Saa,siku mwezi,mwaka vinajurudia Tu Yani ni hakuna mwisho. Yani Muda unaanza alafu unaishia palepale ulipoanzaia.

Mwaka huu NASA wameanzisha calendar ya kwenye mwezini, Kwa Hiyo vizazi vinavyokuja watakuta mwezini kuna calendar tayar, kumbe calendar haikuwepo on the first place.

China, Ethiopian, Jewish, Christians,butha, Islam butha Wana calendars zao na mambo Yana kwenda Tu 😂 kama hakuna calendars kabisa .

Actually badala ya kusema Time Mimi naona tusema circle AU mzunguko, coz Muda AU Time ni ule ule haubadiliki
 
Hii ndiyo nadharia inayosemwa inatakiwa kukubaliwa na kila binadamu na ndiyo nadharia inayoitwa na baadhi ya watu kuwa ni kamilifu na timilifu.

Kuwa hakuna ajue wewe binadamu umetokea wapi na kwa nini upo ivo ulivo. Kuwa Binadamu hana kusudio lolote lile la kuwepo kwake duniani.

Na haileweki imekuwaje binadamu kuna mambo anayoyaita mema na mengine anayaita mabaya.

Hitimisho ni kuwa binadamu ni kiumbe kisichoelezeka.
hakuna hasara kubwa duniani, kama hutokuwa na majibu ya maswali yafustayo:
1. wewe ni nani.
2. ni kwanini uko duniani.
3. Ni nini kitafuata baada ya maisha haya.

MWAMINI YESU UPOKEE WOKOVU
 
Time ya kwenye mwezini ni tofauti na Mars, earth, Jupiter.
Hapa duniani tumejiwejea Muda, Muda wa kufirika Tu, Ndio maana DK, Saa,siku mwezi,mwaka vinajurudia Tu Yani ni hakuna mwisho. Yani Muda unaanza alafu unaishia palepale ulipoanzaia.

Mwaka huu NASA wameanzisha calendar ya kwenye mwezini, Kwa Hiyo vizazi vinavyokuja watakuta mwezini kuna calendar tayar, kumbe calendar haikuwepo on the first place.

China, Ethiopian, Jewish, Christians,butha, Islam butha Wana calendars zao na mambo Yana kwenda Tu 😂 kama hakuna calendars kabisa .

Actually badala ya kusema Time Mimi naona tusema circle AU mzunguko, coz Muda AU Time ni ule ule haubadiliki
Nakubaliana na wewe time is relative and not absolutely ndo maana time ya moon au planet nyingine ni tofauti na earth due to utofauti wa speed and gravity.
 
Kila kitu lazima kiwe na chanzo na mwisho wake.Haiwezekani binadamu iwe alitokea tu vuuuu.yawezekana Hadi Sasa tukawa hatujajua tu kuwa chanzo chetu ni nini lakini lazima tuwe na chanzo.
 
hakuna hasara kubwa duniani, kama hutokuwa na majibu ya maswali yafustayo:
1. wewe ni nani.
2. ni kwanini uko duniani.
3. Ni nini kitafuata baada ya maisha haya.

MWAMINI YESU UPOKEE WOKOVU
Soma bandiko lote ndiyo utaelewa...
 
Time ya kwenye mwezini ni tofauti na Mars, earth, Jupiter.
Hapa duniani tumejiwejea Muda, Muda wa kufirika Tu, Ndio maana DK, Saa,siku mwezi,mwaka vinajurudia Tu Yani ni hakuna mwisho. Yani Muda unaanza alafu unaishia palepale ulipoanzaia.

Mwaka huu NASA wameanzisha calendar ya kwenye mwezini, Kwa Hiyo vizazi vinavyokuja watakuta mwezini kuna calendar tayar, kumbe calendar haikuwepo on the first place.

China, Ethiopian, Jewish, Christians,butha, Islam butha Wana calendars zao na mambo Yana kwenda Tu 😂 kama hakuna calendars kabisa .

Actually badala ya kusema Time Mimi naona tusema circle AU mzunguko, coz Muda AU Time ni ule ule haubadiliki
Mkuu najaribu kukuelewa lakini natofautiana na mtazamo wako

Hiyo NADHARIA yako inaweza kufanya vitu vingi sana VISIWEPO

Binadamu ni kiumbe mdadisi na mjuzi sana, na ili UDADISI ufanye kazi hapa katikati ni lazima vitu vipewe maana na majina ili viweze kutumika katika UJUZI

MUDA ni matokeo ya udadisi wa ukomo wa jambo fulani kutukia.
Mfano wakati zama za kale kabisa kabla ya masaa wala kalenda hizijabuniwa
Utaitaje pale wanaume wanapokwenda kuwinda kutafuta chakula hadi watakapo rudi? Kwa walikua wanajua inabidi watafute HARAKA chakula na kurudi nyumbani ili watu wapate chakula wasife kwa njaa
Na kwamba ikiwa watatatafuta bila kupata ndani ya wakati muafaka watakuta wamekufa kwanjaa

Kwamba ukizama majini kuvua pweza utaiteje ule muda umetumia bila kuvuta hewa kabla hujarudi juu?
Kwamba usiporudi ndani ya huo muda wanajua lazima kunashida imekupata huko chini kwasababu ume pita ule “muda” ambao mtu anaweza kukaa bila kuvuta hewa

Mifano hii inaonyesha kwamba tunaishi against kitu fulani ambacho tunakimbizana nacho wakati wote....... ndio kikapewa jina kikaitwa MUDA

Muda ukazidi kugawanywa kulingana na ujuzi ulivyokua unakua, baada ya kugundua majira na mzunguko wa dunia ndio tukapata muda tunaotumia sasa

Muda wa mwezini na duniani ni sawa tu kinachotofautiana ni namna unavyogawa kulingana na mzunguko wake tu
Muda upo pale pale ni swala la kuamua tu kwamba kwenye mwezi mzunguko wake kamili ni dakika 90 lakini sisi tutaita ni siku moja

Kwahiyo Muda upo
 
Mayu umeongea jambo moja kubwa Sana... Ulimwengu upo tu, na sisi binadamu tunachofanya ni kuutafsiri na kuweka kanuni zinazotuwezesha kufaidi uwepo wa ulimwengu Kwa wakati husika.
 
Kwa Imani ya kidini
Binadamu aliumbwa na Mungu ndio mwanzo wake huo.
Kwa wenye Imani hii.
 
hakuna hasara kubwa duniani, kama hutokuwa na majibu ya maswali yafustayo:
1. wewe ni nani.
2. ni kwanini uko duniani.
3. Ni nini kitafuata baada ya maisha haya.

MWAMINI YESU UPOKEE WOKOVU
Mkuu tafadhali dadafua majibu ya maswali haya
 
Mkuu tafadhali dadafua majibu ya maswali haya
mkuu hili ni somo pana sana. ni la kiroho kwa sababu mtu ni roho. Hivyo cha msingi ni kuanza kujiuliza kwa moyo wa dhati, kisha Roho wa Mungu atakufunulia. majibu yake hayako kwa namna ya akili.

JESUS is Lord&Savior
 
Mambo ya kiroho watu wanataka yajibiwe kiakili.
 
Back
Top Bottom