Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Baridi ipo ila haionekani!

Upepo upo ila hauoneoani!

Inasemwa; fulani ana akili! Lakini haionekani!

Upendo (love) upo lakini hauonekani!

Athari/matokeo ya hivyo ndivyo vinavyothibitisha uwepo wa hivyo!
 
Ndoto ni imaginations, Hazipo kwenye uhalisia.

Ndoto zipo kwenye mawazo ya kufikirika, Sio kwenye uhalisia.
Mkuu. Utakuwa sawa iwapo consciousness inatokana na brain 100% na hakuna kingine out there zaidi ya ubongo.

Kinyume na hapo hakuna limitation na lolote linawezekana na tafsiri ya uhalisia haitafungwa na mwili na nyama ili uwe uhalisia.

Kwani, unapokuwa ndotoni, ukaota unakimbizwa na ngiri, wakati ule unapoteseka na hiyo ndoto unakuwa haupo katika uhalisia kwasababu mwili wako upo kitandani?

Usipoamka ukafa ukazikwa tunathibitisha vipi kuwa huo ulimwengu uliokuwa unakimbizwa na ngiri nao unapotea sababu mwili wako umekufa?

Tunathibitisha vipi kuwa uhalisia wa kifo si ndoto isiyokwisha ili tujiaminishe kuwa baada ya huu uhalisia wa mwili na nyama hakuna kingine.
 
Baridi ipo ila haionekani!

Upepo upo ila hauoneoani!

Inasemwa; fulani ana akili! Lakini haionekani!

Upendo (love) upo lakini hauonekani!

Athari/matokeo ya hivyo ndivyo vinavyothibitisha uwepo wa hivyo!
Kitu kinaweza kuwepo angalau kwa namna zifuatazo:
Kuonekana, Kushikika, Kusikika na kuhisika.

Upepo upo kwa "kusikika" unapo vuma na kutambuliwa upo.

Baridi na joto vipo kwa "kuhisika" na hapa vinatambuliwa vipo.

Akili Haipo kwenye uhalisia. Akili ni neno la kufikirika tu kuonyesha hali fulani ya uwezo wa fikra za mwanadamu.

Sasa, Mungu hayupo kwa namna yoyote ile Haonekani, Hashikiki, Hasikiki na wala Haisiki.

Mungu huyo ni mawazo ya kufikirika tu Imagination just an illusion.
 
Acha story za kufikirika.
 
Yaani nimesoma bandiko lako nachoweza kusema ni kwamba wewe ni Walking Dead.. unasubiri kuzikwa tu.
 
Kumbuka hapa ubongo bado, unafanya kazi.

Na ubongo hufanya kazi wakati wote.
Usipoamka ukafa ukazikwa tunathibitisha vipi kuwa huo ulimwengu uliokuwa unakimbizwa na ngiri nao unapotea sababu mwili wako umekufa?
Ukifa, Ubongo una acha kufanya kazi completely. Fikra zote zina stop, Kiasi kwamba hata huo ulimwengu unapotea.
Tunathibitisha vipi kuwa uhalisia wa kifo si ndoto isiyokwisha ili tujiaminishe kuwa baada ya huu uhalisia wa mwili na ny.
Ili ndoto, iwe na muendelezo lazima Ubongo ufanye kazi. kifo kinafanya ubongo uache kufanya kazi kabisa.

Hata ndoto hizo Haziwezekani..
 
Imethibitishwa kisayansi kuwa consciousness inakufa baada ya mwili kufa?
 
Imethibitishwa kisayansi kuwa consciousness inakufa baada ya mwili kufa?
Sasa kama "conscious" Haifi, Binadamu si angeweza kufahamu kinachoendelea?

Ubongo ukisha Stop, kila kitu kina Stop.
 
Jiwe kuchora A itaonekana kawaida ila jiwe kuandika Allen killewela hapa lazima ujue Kuna Intelligentsia imehusika nyuma yake.

Kuhusu kuwa tupo tupo it means hatuna Mana yoyote Wala value hata uelekeo.
Unepewa thaman kulingana na chanzo chako na thaman yk ipo ndani yako itajulikana utakapoiweka nje.

"You can't go any direction coz our life has final cause and meaning " Euthyphro Plato works Collection.
 
Sasa kama "conscious" Haifi, Binadamu si angeweza kufahamu kinachoendelea?
Hakuna riport ya kisayansi inayothibitisha ukomo wa consciousness iwapo itahamishwa kwenye mwili usiokufa na Kama iwapo mwisho wa mwili huu ndio mwisho wake, kama unayo iweke hapa.
Ubongo ukisha Stop, kila kitu kina Stop.
Boss, Unahitimisha kwa takwimu zipi za kisayansi? Kama ni hisia zako unatumia huna tofauti na tunaosema Kuna MUNGU.
 
Mtoa mada amesema binadamu ni kiumbe kisichoelezeka Yani akijulikani Chanzo chake Wala mwisho wake

Nikajua labda viumbe vingine anaweza kuvielezea Chanzo chake na mwisho wake ndio maana nikataka anielezee Chanzo na mwisho wa kuku

Kumbe pia hata Chanzo na mwisho wa kuku hajui Sasa si angesema tu viumbe vyote havielezeki Chanzo chake Wala mwisho wake Kwa Nini ataje binadamu peke yake
 
Unaota upo ulaya unakula samaki wakati ujawahi kwenda Wala kuimage hivyo
 
Unaota upo ulaya unakula samaki wakati ujawahi kwenda Wala kuimage hivyo
Kwani haujawahi kusikika lolote kuhusu ulaya?

Mpaka ubongo umeweza kuota upo ulaya hapo ni tayari kwamba taarifa za ulaya ushawahi kuzisoma au kusikika mahali.
 
Sio kila kitu lazima kiwe na chanzo cha makusudi. Vitu vingine ni coincidence and being at the right time at the right place. Wewe jiulize kwanini sayari zipo 8 lakini ni moja tu ndiyo inasupport maisha. Siamini nilichoandika lakini ukitumia logic, critical thinking na facts hio ndio conclusion.

Coincidence.
 
Umewahi ota ndoto,ni jinsi gani unaweza thibitisha ndoto zipo.
Kwa mfano wa ndoto, mimi huwa siwaelewi wanaosemaga wanaota ndoto gani sijui! Sijawai ota chochote najuaga labda ni mitume tu ndo walikuwa wanaota ndoto!
 
Kwamba ni lazima kuota kwa vile tu kuna taarifa flan ndani ya ubongo!?

Na usipoota ndoto yeyote kwa muda wa maisha yako, (kama mimi) ina maana hakuna taarifa yeyote kwenye ubongo!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…