Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Mkuu hii sio binadamu tu, kila kitu chenye asili ya hii dunia haikielezeki na akiwezi kufahamka kwa ukamilifu wake, ndio mana wametengeneza taasisi kama science na kuanzisha dini ili kuleta majibu ya kutunga na tusiwe na shauku ya kutaka kujua ukweli halisi
Historia ya Adam na eve/hawa sio kweli, na ufahamu wote wa dunia na outta space na galaxies sio kweli. Ulimwengu mzima ni hii dunia tu hakuna nje ya dunia nakila kitu kimo ndani ya ulimwengu huu,yaani nyota mwezi,jua sayari kila kitu kimo ndani ya hii dunia,

Hayo maigizo ya outer space sayari zenye udongo na mwezi wa kwenda mtu akatua na jua Iloilo umbali wa 53 mil miles ni uzushi mtupu
Ni phenomenal kubwa sana sisi binadamu tulio hai Tupo hapa saivi na tunaishi wengi wemepita kwa malaki ya miaka nyuma na wengi watakuja baada yetu kwa malaki ya miaka, hii dunia haina mwisho wa ukubwa na haina mwisho wa maisha
Waliokuja mwanzo na kuweza ku-collect info muhimu wametuzidi akili wanatudangabya tu, kuleta dini na science ili kutupumbaza watu wote dunia nzima.
Umewaza kitoto sasa,ulimwngu mzima ni dunia tu?? Wakati kuna matilioni ya sayari,nyota zote zipo kwnye dunia? Wakati kuna manyota makubwa mara mabilioni ya dunia .fanya tafiti kabla hujaandika ujinga
 
Infropreneur Bado hujajibu hoja yangu ya msingi kuhusu Hiyo nadharia yako kwamba kila kitu chenye chanzo ni Lazima chanzo hicho kiwe na chanzo kingine na Kwa maana nyingine hali hiyo huendelea bila kikomo!!

Yaani chanzo kimoja huanzisha mzunguko wa vyanzo usio na mwisho.
 
Kwamba ni lazima kuota kwa vile tu kuna taarifa flan ndani ya ubongo!?

Na usipoota ndoto yeyote kwa muda wa maisha yako, (kama mimi) ina maana hakuna taarifa yeyote kwenye ubongo!?
Kwani nimeweka ulazima wa kwamba kila mtu huota ndoto?

Nimesema hivi, matukio ya ndotoni ubongo wako una taarifa nayo either ushawahi kuyaona, kuyasoma, kusimuliwa, kuyashuhudia, kuya angalia, kuyafanya au kuya sikiliza.
 
Umewaza kitoto sasa,ulimwngu mzima ni dunia tu?? Wakati kuna matilioni ya sayari,nyota zote zipo kwnye dunia? Wakati kuna manyota makubwa mara mabilioni ya dunia .fanya tafiti kabla hujaandika ujinga
Nadhani ni watu wachache hufahamu kuwa Kuna tofauti kati ya dunia (world) na ulimwengu (universe).

Hakuna haja ya kutumia lugha Kali na ngumu badala yake tuelimishane.
 
Infropreneur Bado hujajibu hoja yangu ya msingi kuhusu Hiyo nadharia yako kwamba kila kitu chenye chanzo ni Lazima chanzo hicho kiwe na chanzo kingine na Kwa maana nyingine hali hiyo huendelea bila kikomo!!

Yaani chanzo kimoja huanzisha mzunguko wa vyanzo usio na mwisho.
Ukisema kitu fulani ni chanzo.

Kwanza lazima uthibitishe kweli ni chanzo.

Pili ueleze na uthibitishe chanzo hicho, Hakina chanzo kingine chochote kile.

Pia ueleze chanzo hicho kimewezaje kutokea tu from Nothing, Bila chanzo kingine chochote kile.
 
Sasa hapo ndipo Ninashidana na hii nadharia ambayo inashadadiwa sana na wapinga uwepo wa Mungu.

Jee Mungu ni nani au ni nini? Jee unaweza kuelezea kuwa Ili Mungu awe Mungu anatakiwa/inatakiwa awe na sifa zipi??
 
Mungu ni dhana ya kufikirika isiyo kuwepo inayo dhaniwa kwamba eti ndicho chanzo cha Dunia na kila kitu.

Waamini Mungu wanasema Mungu ni muweza wa yote, Ila kashindwa kudhibiti uovu na mabaya.

Waamini Mungu wanasema Mungu ni mwenye kujua yote, ila kashindwa na alishindwa kumdhibiti huyo shetani mapema.

Waamini Mungu wanasema Mungu ni mwenye Upendo, huruma na mwema sana. Ila kwa ukatili,uovu, mabaya, mateso, magonjwa, majanga ya asili yaliyopo Duniani yana dhihirisha na kuthibitisha Mungu huyo hayupo.

Mungu huyo mwenye Sifa tajwa hapo juu kwa mujibu wa waamini Mungu, Angekuwepo...

Unge kuwa hata huhitaji kumuomba kitu, Maana yeye Mungu mjuzi wa vyote angelitambua mahitaji yako kabla hata hujamuomba.

Hivyo Mungu huyo hayupo.
 
Hii ndiyo nadharia inayosemwa inatakiwa kukubaliwa na kila binadamu na ndiyo nadharia inayoitwa na baadhi ya watu kuwa ni kamilifu na timilifu.

Kuwa hakuna ajue wewe binadamu umetokea wapi na kwa nini upo ivo ulivo. Kuwa Binadamu hana kusudio lolote lile la kuwepo kwake duniani.

Na haileweki imekuwaje binadamu kuna mambo anayoyaita mema na mengine anayaita mabaya.

Hitimisho ni kuwa binadamu ni kiumbe kisichoelezeka.

Sio binadamu tu mkuu

Kwanza unatakiwa kujua kwamba binadamu HAJUI KILA KITU kuhusu huu ULIMWENGU na vyote vilivyopo

Shida inaanza pale anapo “umbwa” ambaye atakua anajua kila kitu ili kujipa majibu ya mambo tusiojua na kujifariji ujinga kuwa yeye ndio ameumba kila kitu na tusivyojua

Kama unasumbuka sana haiwezekani binadamu na ulimwengu kutokea tu basi hutaishia hapo, ukimjua aliyeumba utataka kumjua na yeye kaumbwa na nani?

Ukweli ni kwamba hakuna anayejua
Lakini pia hayupo huyo aliyeumbwa na binadamu (Mungu) ili yapatikane majibu ya mambo tusio yajua kuwa yeye anayajua
 
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.

Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.

Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.

Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?

Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?

Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?

Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??
Uke unabuniwaje mzee?

Ushawishi kufikiria zile hadithi za dini kuwa binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu?

Hujawahi jiuliza kama binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu huo mfano umeangazia kwenye kitu gani?

Kwasababu binadamu tuna matako, so could we think the same way to God?

What if God has got some ass too?
 
Waamini Mungu wanasema Mungu ni mwenye Upendo, huruma na mwema sana. Ila kwa ukatili,uovu, mabaya, mateso, magonjwa, majanga ya asili yaliyopo Duniani yana dhihirisha na kuthibitisha Mungu huyo hayupo.
Hapa Nina swali ambalo sijibiwi ingawa naona kama ni swali rahisi.

Ili useme hili jambo ni baya ama jema unatumia kigezo gani na kinatokana na msingi upi??

Hayo uliyoyaorodhesha hapo Yana shida gani?

1. Ukatili unaujuaje na kwa vipi uwe ni kitu kibaya?

2. Uovu unapimwaje?

3. Kwani majanga ya dunia chanzo chake ni Nini?
 
Uke unabuniwaje mzee?

Ushawishi kufikiria zile hadithi za dini kuwa binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu?

Hujawahi jiuliza kama binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu huo mfano umeangazia kwenye kitu gani?

Kwasababu binadamu tuna matako, so could we think the same way to God?

What if God has got some ass too?
Tatizo linaanzia hapo.

Jee mfanano na Mungu ni wa kimaumbile tu ya kimwili? Au ni mfanano wa mambo ya kiroho ambayo huamini kuwa yapo??
 
Tatizo linaanzia hapo.

Jee mfano Wa Mungu maumbile tu ya kimwili? Au ni mambo ya kiroho ambayo huamini kuwa yapo??
Mungu ni roho

Roho haionekani

Mungu kamuumba mtu kwa mfano wake.

Mungu huyo asiyeonekana alifinyanga udongo unaoonekana kutengeneza mtu

Mungu huyo huyo ambaye ni roho na asiyeonekana alipulizia puani pumzi kwenye huo udongo, huo udongo ukawa mtu.

Huyo mtu akaitwa adamu.

Adamu alikuwa ameumbwa akiwa amekamiliika viungo vyote.

Ila swali la kujiuliza alikuwa na sehemu za siri kwa ajili ya kazi gani?

Sehemu za siri zinakazi mbili, kutoa taka na kutumika kwenye tendo la ngono.

Sasa sex haikuwa kwenye malengo kwasababu hakuwepo mwanamke na wala haikuwa idea ya Mungu kumuumba mwanamke. Mpaka pale Adam alipoanza kulalamika kuhusu upweke

Sasa fikiria nyakati ambazo Adam yupo solo

Maana yake sehemu za siri zilikuwa zinakazi ya kutoa uchafu maana yake ni matokeo ya mtu kula msosi kisha ukafanyika mmeng'enyo ndio zile taka zitolewe kwa njia hiyo.

Na wakati huo huo ukumbuke hakuna maelezo kuwa Adam alikuwa ana nyumba yenye choo.

Bali hadithi zinasema alikuwa anashinda misituni tu na wanyama ina maana kama ni haja basi alikuwa anaimalizia huko huko (environment pollution)
 
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.

Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.

Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.

Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?

Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?

Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?

Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??
Najutia Kwa nini sikukueleza kuwa Kwa bahati mbaya kile kitabu cha falsafa kilitumbukia Kwa bahati mbaya kwenye sufuria la supu , hivyo basi sikuwa na budi kukiacha humo humo vikachemka pamoja na Ile nyama ambayo supu yake ndo umeinywa ..

You are to philosophical bro. Najiuliza maswali mengi pia ambayo sipati majibu yake
 
Ndugu zangu binadamu ana usiri mkubwa sana ndani yake, ni kiumbe wa pekee sana ambaye amepewa akili, utashi na uwezo kama wako wa kumjenga au kumptosha binadamu mwenzake. Kwa waliopitia mengi mazito huwezi kumpuuza Mungu hata kidogo, ni kufuru na hatia kubwa.
Pekee nilishapita kipindi cha kufikiria mada za kuona hakuna Mungu na reasons za kibinadamu zenye nguvu zaidi ya hiyo yako, niliingia mitandaoni kutafuta vitabu vya ajabu sana ili mradi nijiridhishe na hayo mawazo yangu mwishowe Niliamini hakuna MUNGU kweli. Lakini Mungu hutuacha tupitie nyakati kama hizo ili atuoneshe uwezo wake, na kwa upande wako haitachukua muda utanielewa ninachomaanisha.

Binadamu ni roho tu huu mwili ni box. Unapokuwa na roho hai huwezi kumkufuru Mungu. Ntakuja nielezee visa vilivyonifanya nijue Mungu yupo na sisi ni roho
 
Hapa Nina swali ambalo sijibiwi ingawa naona kama ni swali rahisi.

Ili useme hili jambo ni baya ama jema unatumia kigezo gani na kinatokana na msingi upi??

Hayo uliyoyaorodhesha hapo Yana shida gani?

1. Ukatili unaujuaje na kwa vipi uwe ni kitu kibaya?

2. Uovu unapimwaje?

3. Kwani majanga ya dunia chanzo chake ni Nini?
Ngoja nijibu swali lako.

Unatumia kigezo gani kujua hili baya na hili zuri

Kuna kitu kinaitwa "empathy"

Empathy ni kitendo cha kushea feelings za mtu mwingine (compassion) na kuanza kuzi feel kwa kujiweka wewe katika ile nafasi.

Yani unamuondoa yeye kwenye hiyo nafasi halafu unajiweka wewe.

Hiyo itakupa uwezo wa wewe kutambua kihisia ni kivipi mtu mwingine anavyojiskia pindi hicho kitendo kikifanyika.

Mfano mimi nimekuona mahala ukipokea peaa, nikapanga mpango wa kukuibia pesa zako.

Lakini kabla ya kuja kutekeleza kitendo cha wizi nitaanza kufikiria "vipi kama ndio mimi ningekuwa na hizo hela halafu mtu akaja kuniibia nitajiskiaje?"

"Je mimi napenda kuibiwa?"

"Vipi kama hizo hela za jamaa ni hela alizokopa kwa ajili ya matibabu ya ndugu yake mpendwa?"

"Vipi kama ingekuwa ndio mimi ndugu yangu namuona anafariki kwa kukosa huduma za matibabu kwasababu hela iliyopaswa kutumika kama malipo imeibiwa?"

"Au labda ilikuwa ni hela ya mkopo nimechukua kwa ajili ya kufungua biashara halafu imeibiwa na benki imekuja kuuza mali zangu, ningejiskiaje?"
 
Back
Top Bottom