Hii hoja yako huoni kama ni dhaifu. Maana kuzaliwa ndani ya dunia haimaanishi kwamba dunia ipo ipo milele yote.
Kwani kuna wakati dunia haikuwepo kisha ikawepo?
Unachotakiwa kuonesha ni kwa nini dunia ipo tu haina mwanzo na huo mwanzo wake ni kwa nini usiwe na chanzo.
Hakuna ulazima wa dunia iwe na mwanzo.
Kama ulazima huo upo, Hata huo mwanzo wa dunia lazima uwe na mwanzo wake.
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mwanzo, Hata mwanzo wa mwanzo lazima uwe na mwanzo.
Hivyo basi Dunia ni mwanzo usio na mwanzo mwingine.
Na dunia ipo inaonekana, Na hakuna uthibitisho wowote ule unao onyesha kwamba dunia haikuwepo.
Dunia ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.
Nimetumia mantiki yako kukujibu.
Kama miaka 300 iliyopita hukuwepo na wanasayansi wanasema kuwa dunia ina mamilioni ya miaka,
Dunia ina mamilioni ya miaka kwa vile wanasayansi hawana majibu sahihi ya wakati gani dunia ilianza.
Ni makisio yao tu (predictions) kusema kwamba dunia ina mamilioni ya miaka, Wanasayansi hao hawana uthibitisho wowote ule.
Ushahidi na uthibitisho wa kwamba Dunia iliumbwa mamilioni na mabilioni ya miaka huko nyuma Haupo.
Hivyo hata kusema kwamba Dunia ina mabilioni ya miaka ni makisio tu.
Ukweli ni kwamba Dunia haina mwanzo, wala mwisho.
Dunia ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo milele.
unabishaje kwamba kabla ya wewe kuna watu walikuwepo na kushuhudia viashiria vya kuumbwa kwa dunia??
Watu hao walio shuhudia viashiria vya kuumbwa Dunia walikuwa wanaishi kwenye nini?
Watu hao walio shuhudia kuumbwa Dunia walikuwa wakiishi sehemu gani tofauti na duniani?
Hiyo sehemu walioishi watu hao ni ipi?
Na sehemu hiyo ilitoka wapi?
Unaposema "unaamini" hapo unaleta mambo ya imani. Kwa nini unataka Imani yako kwamba kulikuwa na watu wengine miaka 300 iliyopita ikubalike
Kwani miaka 300 iliyopita kulikuwa hakuna watu?
Watu walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo.
Hakuna wakati ambao Binadamu hakuwepo halafu ghafla akawepo.
Binadamu (watu) walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo milele.
na "imani" ya wengine kwamba Dunia iliumbwa isikubalike??
Dunia hiyo iliumbwa kutoka wapi?
Na huko ilikokuwa kuliumbwa na nani?
Yani sehemu iliyotumika kuumba dunia iliumbwa na nani?
kwa nini unaamini kwamba dunia hawezi kuwepo bila ya binadamu kuwemo ndani mwake!?
Dunia inaweza kuwepo bila ya binadamu.
Lakini hakuna wakati wowote ule ambapo Dunia ilikuwepo bila binadamu.
Mfano mabomu ya nyuklia yakalipuliwa dunia nzima binadamu tutatoweka wote na dunia itabaki.
Hivyo dunia inaweza kuwepo bila ya binadamu, Lakini binadamu hawezi kuwepo bila ya dunia.
Kwa mujibu wa imani za wengine, ni kwamba Dunia iliumbwa kwanza kisha ndipo binadamu akaumbwa. Hii inaleta mantiki sana.
Dunia hiyo iliumbwa kutoka wapi?
Huyo aliye umba dunia aliumbwa na nani?
Kabla ya kuumba Dunia, Sehemu aliyokuwepo huyo muumbaji ili umbwa na nani?
Binadamu alitokana na nini?
Binadamu alitokana na binadamu ndio uthibitisho uliopo mpaka sasa.
Kwamba binadamu mwanaume na mwanamke wanazaa binadamu mwingine kwa mbegu zao.
Hakuna uthibitisho mwingine wa kuthibitisha kwamba binadamu alitokana na kiumbe kingine au namna nyingine.
Nadharia zote za kisayansi, kihistoria na kidini hazina uthibitisho wa uhakika mpaka sasa zaidi ya makisio tu.
Jinsi maumbile ya binadamu yalilvyo na mpangilio maalum unadhani alitokana na nini. Hakuna mbunifu wake??
Mpaka sasa hakuna majibu sahihi yenye uthibitisho wa uhakika kwamba mpangilio huu ulitokana na nini.
Mbunifu wake hayupo mpaka sasa na hathibitishiki yupo zaidi ya mawazo ya kufikirika tu kwamba mbunifu huyo yupo.