Binadamu Kumlaumu Mungu kwa Makosa Yake Mwenyewe.

Binadamu Kumlaumu Mungu kwa Makosa Yake Mwenyewe.

Mimi sikupewa fursa ya kuchagua mema na mabaya, sikuwepo bustani ya Eden. Watoto wote wakiwemo albino wanaokufa kwa kansa, vita, njaa na mauaji ya kila aina pamoja na wanaobakwa hawakupewa fursa ya kuchagua mema na mabaya huko kwenye story yenu ya Eden.

Mtoto wa mwaka 1995 au 1980 unataka apewe Fursa ipi iliyotokea wakati Dunia inaumbwa na Wazazi wa kwanza wanaumbwa?

Na Je! Mungu aliposema UTAKUFA HAKIKA. Ulidhani Kufa kwa Njaa siyo KIFO? , Kufa kwa Kukatwa mapanga Njiani ukitokea kwenu siyo KIFO.

JE! hujawahi kusikia Neno LAANA, laana anaweza Kufanya Babu Yako jambo lisimpate Yeye ila Likawapata Wajukuu zake hiyo Ndio maana Ya Laana hata Kama HUKUWEPO
 
Ukipita Mitandaoni utakuta Kwamba Kuna Mijadala Mingi inayohusu Mungu kwamba kama Anatupenda Kwanini Tunateseka ,, oooh kwanini Kuna Mafuriko...oooh kwanini Watoto wanakufa na Njaa.. Oooh kwanini Vita Haviishi.. Haya Yote Hayana Tofauti na Kumlaumu Mungu kwa Makosa Yetu Wenyewe

Mwanzo 2:16-17
“Mwenyezi-Mungu alimwamuru huyo mwanamume, “Waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani; lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.””

Neno HAKIKA UTAKUFA limebeba Maana Kubwa sana. Kumbuka Hakukuambia utakufa Ukiwa umelala Kitandani. UTAKUFA vifo vya AINA yote (VITA, NJAA, MAGONJWA, KUJIUA , MAFURIKO n.k) Hivyo Vyote ni Vifo

Sasa Unamshangaa Mtu anasema Kama Mungu anatupenda sana Kwanini Tunapatwa na Magonjwa, Vita , Njaa inaua watoto n.k. Kwani wakati anakuambia Wewe Usile maana Yake Alikupa Uwezo wa Kuchagua MEMA na MABAYA na uliishi Katika Kutokuwa na Magonjwa wala Vifo bustanini Mwake toka Mwanzo ila Kwa Vile ulichagua MABAYA usimlaumu Yeye tena.

Wasioamini Wengi wanasema, wanaoamini wanasema Mungu ni UPENDO ..je! Upendo huo ni upi mbona Tunaangaika Duniani. MNaanhaika Ndio maana Hukufuata Ulichoambiwa na Baba yako kabla, kwa Wenye Watoto wadogo tunajua unaweza Mkataza kitu maana Unajua Madhara yake baadae. Je! Akipatwa na Madhara hayo uliyomkataza Ina maanisha Wewe MZAZI huna UPENDO na Mtoto huyo? Jibu ni Hapana Utampenda Daima hata kama amekosea na Ulimuonya, hivyo Hivyo Kwa Mungu Wetu anatupenda Daima na Ametuonya Sana Ila Sisi Tunamlaumu kila Mara

Sasa Neema Imekuja Kwetu Tena Na Neema Hiyo ni Hii YESU alipokuja Ametupa Nafasi Ya Kurudi tena Katika Neema Ile Ile ya Bustani ya EDENI.Tuliyokuwa nayo Mwanzoni. Tulifanya KOSA la Kula Tunda Lile na Laana Hiyo Imekuja Kwetu alipokufa Msalabani Alichukua Dhambi Yetu hii na Kuifia Msalabani

Ndio maana Katika Mahubiri yake Alikiwa anasisitiza UZIMA WA MILELE , UZIMA WA MILELE maana Tulipoteza uzima Huo Mwanzoni

Mungu angetuacha Tufe tu maana Hana Cha Kupoteza ila Imeandikwa KWA MAANA MUNGU Aliupenda Ulimwengu Mpaka akamtoa Mwanae wa Pekee ili.Kila Amwaminie ASIPOTEE basi AWE NA UZIMA WA MILELE
Mwenyezi Mungu alimuumba mtu ili awe khalifa duniani,

Adam anasema: yeye kula tunda halikuwa kosa linaloweza kukwepeka,na ilikuwa njia ya wao kuletwa duniani.

Ukishajua kusudi la mtu kuumbwa, huwez kulaumu kwanini alikula tunda.
========================

Pili
Mwenyezi Mungu anasema:
Habadilishi yaliyomo kwenye nafsi ya mtu hadi ubadilike wewe mwenyew.
Kwa mfano;
Unafanya surgery kubadilisha maumbile yako,
 
Kwani Ni nani aliyekuambia Kwamba Ukitenda Dhambi kama Nyoka(shetani) basi Mungu anakuzuia Kutembea uende Popote utakapo?
Kwa hiyo huyo Mungu aliruhusu shetani aendelee kuwepo bustanini baada ya kumuasi ili aje kuwadanganya kina Eva?

Kwa nini Mungu hakumfukuza Shetani bustanini mara moja! mara tu alipoona ameasi?

Kwa nini Mungu aliruhusu Shetani aendelee kuwepo bustanini baada ya kuasi na akasubiri aje kuwadanganya kina Eva?

Na mbona kina Adam na Eva, walifukuzwa bustanini mara moja, baada tu ya kula tunda?

Kwa nini kina Adam na Eva hawakuachwa kuendelea kuwepo bustanini kama vile Shetani alivyoachwa kuwepo bustanini baada ya kuasi?

Au huyo Mungu na Shetani ni maswahiba walioshibana wanaopanga namna ya kumtesa binadamu?

Ukisema Mungu alimwacha Shetani aingie Bustanini. Je kosa la Mungu ni Lipi kama TAYARI alishamuumba ADAM na EVA aliowapa Uhuru wa Kuchagua KUTOKULA LILE TUNDA. Je! Ulitaka Mungu awaambie Shetani anakuja kuwadanganya? Wakati keshawapa AKILI na ONYO?
Kwa nini Shetani aruhusiwe kuwepo bustanini baada ya kuasi?

Kwa nini Shetani hakufukuzwa bustanini mara moja baada ya kuasi kwake?

Mbona kina Adam walifukuzwa bustanini mara moja baada ya kuasi.

Kwa nini Shetani aliachwa?
NA kama Unasema Aliruhusu Binadamu aangamie Je! Kwanini Wewe upo MPAKA leo!? Kwanini Hujaangamia. JE UMESAHAU kwamba Kwa Vile alikupenda Sana Alimwacha NUHU na Watoto wake kwenye SAFINA. kwanini hakuwaangamiza WOTE wafe ili AANZE UPYA.
Kwanza mimi siamini habari za huyo Mungu.

Huyo Mungu hayupo.

Habari za Biblia ni hekaya kama zilivyo hekaya za Abunuwasi.

Hazina mantiki.
MUNGU Anakupenda na Alikuumba Ka UPENDO mkubwa Kuliko hata malaika upendo wake hatuwezi kuupima hata Tukiongea muda mrefu ni UPENDO wa Agape usio kuwa na Kipimo
Mungu angekuwa anatupenda, asingeruhusu Dunia yenye mateso kiasi hiki kwa binadamu.

Mungu huyo angekuwa anatupenda, angeumba dunia isiyo na mabaya.

Na angeumba binadamu wema tu, watakao tenda mema siku zote na wakati wote.
 
Halafu kwanza wakati Adam na Eva wanakula tunda sisi hatukuwepo.

Hatupaswi kupewa adhabu kwa kosa ambalo halituhusu na kwanza hatukuwepo.

Huyo Mungu atatoaje adhabu kwa watu wote kwa kutumia kosa la watu wawili?

Kwani sisi ndio tulikula hilo tunda?

Huyo Mungu asitupakazie makosa ya watu wengine!

A deal na haohao kina Adam na Eva wake. Maana wao ndio walikuwa huko bustanini.

Sisi wengine asituhusishe kwenye adhabu zao.

1. Kwani Ulitaka Uwepo kwa Namna Gani Infropreneur? Ulitaka uwepo Bila Kuzaliwa maana Wote tunakuja Duniani kwa Njia Hiyo. Wewe ulitaka Uwepo kwa Njia Ipi?. Maana Mtu aliyezaliwa 1980,1990,1890 anatakaje Kuwepo Mwaka 1700, au 1300 ? Au basi Mwanzo kabisa wa Ulimwengu anawezaje Mtu huyo kuwepo bila Vizazi kupita kwanza vilivyomtangulia! Hiyo ni LAANA waliyoifanya Wazazi wetu hatuna cha Kuwalaamu kwa Kudanganywa maana hata ww ushawahi kudanganywa na ukafanya UOVU, kwao waliteleza na Hekima kubwa ni KUWASAMEHE wazazi wako maana Hawakujua kwamba Ww utateseka Hivi. Ila NEEMA hiyo ya Ww kusema Hukuwepo YESU alishasema Mwenyewe amekufa Msalabani kwa DHAMBI zetu na Ndio maana Alijiita Mwana Wa ADAM na Dhambi Kuu iliyoingia Dunia ni Hiyo ya Kula Tunda Tulilokatazwa.

2. Umesema Mungu asikuweke kwenye Adhabu isiyo ya Kwako. Je Unadhani ungekujaje Duniani Bila Wao. Maana Waliambiwa Kwamba Kama Wakila Tunda Watakufa HAKIKA. Na si kwamba Mungu hakuwapa Adhabu aliwapa Adhabu aliwafukuza Bustanini na Mule Bustanini kulikuwa na Mti wa Uzima wa Milele pia. Ambapo Kama Wangeendelda Kukaa Mule Basi huyo huyo Shetani ambaye Mungu alimuumba Angewashawishi wale Ili waishi milele na Shetani huyo angejitwalia Jeshi kubwa la Binadamu litakalopingana na Mungu. Kwahiyo ndio maana akawatoa Bustanini
 
Huyo Mungu angeweza kufanya laana hiyo iishie kwa haohao Adamu na Eva.

Sio kusambaza laana hiyo kwa vizazi vyote ambavyo havihusiki na hao kina Adam.

Huu ni uonevu na ujinga!
 
Kwa nini huyo Mungu hakumdhibiti nyoka asiharibu uumbaji wake?

Kwa nini huyo Mungu hakumdhibiti nyoka asiwepo bustanini kumdanganya Eva?

Kama Eva alikuwa na haki ya kukubali, kwa nini apewe adhabu?

Kwa nini Mungu aweke haki na uhuru wa kukubali halafu baadae aje kukuadhibu?

Hii ni haki au mtego?

Kwa nini Mungu aliumba wanadamu wenye uwezo wa kudanganywa na nyoka?

Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu ambao hawadanganywi?

Mungu mnayedai kwamba ni mjuzi wa vyote, Je hakujua kwamba nyoka atakuja kudanganya binadamu amdhibiti na kumzuia mapema?

Huo uhuru wa binadamu kuamua jambo baya limtokee, uliwekwa na nani?

Mungu muweza wa vyote, aliumbaje binadamu wanaoweza kutenda mabaya?

Mungu muweza wa vyote, alishindwaje kuumba binadamu wema tu, watakao mtii na kutenda mema siku zote na wakati wote?
1. Usitumie neno KWAHIYO MUNGU ALIRUHUSU. Unakuwa unakosea Maana Hata Wewe nikikuambia twende Tukaibe Benki Utakuja BILA kufikiria chochote kile utaenda nami Kufanya Uharibifu. MUNGU haruhusu ila Ni Willing yako mwenyewe. Shetani Hakuruhusiwa kufanya Hivyo bali alienda kwa Tamaa zake mwenyewe Ili apate Watu wengi na ROHO nyingi ili aanzishe Jeshi Lake la UOVU

2. Umeuliza pia kwanini hakumdhibiti Nyoka 🐍, hakumdhibiti maana aliumba Kiumbe ambacho alikipa Uhuru wa KUKATAA kinaposhawishiwa. Je ! Hujawahi kuona Watu wanaowadhibiti mabinti (geti kali) bila Kuwapa ruhusa yeyote ile vitu gani baadae wanafanya. Je Unataka Mungu akufanyie Hivyo Akufunge Mnyororo wakati Huo huo amekupa Akili ya Kukataa vishawishi si UTAKUJA kumlaumu pia Kwamba Hakukuweka huru na Wakati amekuumba Kiumbe Huru

3. Umeuliza pia kwanini akupe uhuru wa kuchagua halafu akuadhibu. MUNGU Hana Nia Ya Kukuadhibu Adhabu ALIMPA SHETANI Peke yake ya Kuzimu na Ataaribu ROHO yake au Kuiangamiza ROHO yake na Malaika zake MILELE muda utakapofika. Ila WEWE amekupa Muda wa Kumrudia na Umepata Neema hiyo ili Awavute Wengi wasiangamie. Utaadhibiwa pale tu utakapokuwa mkaidi kutotubu dhambi zako na Kuendelea Kufuata Udanganyifu wa Shetani hapo Ndipo amekuambia TUBUNI DHAMBI ZENU NA MUAMINI YESU KRISTO KWAMBA ALIWALIPIA ILE DHAMBI YENU NANYI MTARITHI UZIMA WA MILELE. Sasa hapa Umepewa muda wa Kumrudia yeye ili Shetani asiende na Wanadamu kwenye Hukumu yake basi Aende na Malaika zake waovu tu wewe upate uzima wa Milele

4. Umeuliza pia ALISHINDWAJE KUUMBA BINADAMU WASIODANGANYIKA! Siyo Binadamu tu hata Malaika wake amewaumba Wanadanganyika ndio Maana Ya Neno FREE WILL. Kumbuka Ameumba Ng'ombe , Kuku , Bata ambao hawana Fres Will Je Ulitaka AKUUMBE hivyo? uwe kama Ng'ombe au SAMAKI AU simba porini anayewaza Chakula Tu hajali ameua Mtoto wake au amemuua swala bila Kuwaza Mara mbili mbili. Viumbe kama Wewe au Malaika ni VIUMBE pekee ambavyo amevipa Free Will

5. Umeuliza pia MUNGU mwenye Uwezo wote ameumbaje Binadamu anayeweza Kutenda Maovu.. JE! HUJUI KWAMBA KUNA BINADAMU AMBAO HAWATENDI MABAYA NA WAPO DUNIANI? Toka azaliwe ameishi kwa kumtumikia Mungu bila kutenda uovu JE hao unawazungumziaje?

Mfano Mzuri ni AYUBU Ambaye hakumtendea Mungu ubaya wala UOVU wowote ule. Lakini SHETANI alimvamia na kumtia magonjwa ila AYUBU hakukubali kutenda UOVU na MUNGU ALIMLIPA MARA MBILI Akamzawadiwa Mara mbili ya Utajiri wake aliokuwa nao

6. Umeuliza Pia Mungu ameshindwaje Kuumba Binadamu wema tu. Je nikuulizd Wewe je UNASHINDWA KUWA MWEMA MAISHA YAKO YOTE ? Unaweza si ndio ila UTACHAGUA MWENYEWE kuua, kuiba, kusema Uongo na kutamani Vitu Viovu. Ila UNAWEZA KUWA MWEMA BILA SHURUTI
Sasa Kwanini Kama Wewe unaweza Kuamua Hata KESHO kutokusema UONGO siku nzima uanze Kumlaumu Mungu. Hujui AMESHAKUUMBA wewe mwema toka Tumboni mwa Mama Yako
 
Huyo Mungu angeweza kufanya laana hiyo iishie kwa haohao Adamu na Eva.

Sio kusambaza laana hiyo kwa vizazi vyote ambavyo havihusiki na hao kina Adam.

Huu ni uonevu na ujinga!
Siyo UONEVU maana ALISHATAMKA kwamba Kama Wakila Tunda Hilo WATAKUFA HAKIKA. Kwahiyo Walitakiwa KUFA ili MUNGU asionekane Muongo maana SHETANI ALISEMA HIVI

Mwanzo 3:4-5
“Nyoka akamwambia mwanamke, “Hamtakufa! Mungu alisema hivyo kwa sababu anajua kwamba mkila matunda ya mti huo mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

Kwahiyo KAMA WASINGEPATWA NA KIFO Mungu angeonekana MUONGO na Shetani ni mkweli. Na wewe 🫵 ungekuja kusema Humu pia kwamba Mbona Hawakufa Kwahiyo Mungu alisema Uongo. 👿 angebeba Kombe kwa Ushindi. Kwahiyo Maneno ya Mungu Ni UKWELI daima na SHETANI ni baba wa UONGO ndio maana Anawaaminisha hata Nyie kwamba Mungu hawapendi ndio maana Mnateseka kama Angekuwa anawapenda Msingeteseka hapa Duniani

Anawaambia Hivyo Ili Muamini Mungu hana Upendo na Nyie na Mumulaumu maisha Yenu yote ndio kazi ya Shetani ilivyo
 
1. Usitumie neno KWAHIYO MUNGU ALIRUHUSU. Unakuwa unakosea Maana Hata Wewe nikikuambia twende Tukaibe Benki Utakuja BILA kufikiria chochote kile utaenda nami Kufanya Uharibifu. MUNGU haruhusu ila Ni Willing yako mwenyewe. Shetani Hakuruhusiwa kufanya Hivyo bali alienda kwa Tamaa zake mwenyewe Ili apate Watu wengi na ROHO nyingi ili aanzishe Jeshi Lake la UOVU

2. Umeuliza pia kwanini hakumdhibiti Nyoka 🐍, hakumdhibiti maana aliumba Kiumbe ambacho alikipa Uhuru wa KUKATAA kinaposhawishiwa. Je ! Hujawahi kuona Watu wanaowadhibiti mabinti (geti kali) bila Kuwapa ruhusa yeyote ile vitu gani baadae wanafanya. Je Unataka Mungu akufanyie Hivyo Akufunge Mnyororo wakati Huo huo amekupa Akili ya Kukataa vishawishi si UTAKUJA kumlaumu pia Kwamba Hakukuweka huru na Wakati amekuumba Kiumbe Huru

3. Umeuliza pia kwanini akupe uhuru wa kuchagua halafu akuadhibu. MUNGU Hana Nia Ya Kukuadhibu Adhabu ALIMPA SHETANI Peke yake ya Kuzimu na Ataaribu ROHO yake au Kuiangamiza ROHO yake na Malaika zake MILELE muda utakapofika. Ila WEWE amekupa Muda wa Kumrudia na Umepata Neema hiyo ili Awavute Wengi wasiangamie. Utaadhibiwa pale tu utakapokuwa mkaidi kutotubu dhambi zako na Kuendelea Kufuata Udanganyifu wa Shetani hapo Ndipo amekuambia TUBUNI DHAMBI ZENU NA MUAMINI YESU KRISTO KWAMBA ALIWALIPIA ILE DHAMBI YENU NANYI MTARITHI UZIMA WA MILELE. Sasa hapa Umepewa muda wa Kumrudia yeye ili Shetani asiende na Wanadamu kwenye Hukumu yake basi Aende na Malaika zake waovu tu wewe upate uzima wa Milele

4. Umeuliza pia ALISHINDWAJE KUUMBA BINADAMU WASIODANGANYIKA! Siyo Binadamu tu hata Malaika wake amewaumba Wanadanganyika ndio Maana Ya Neno FREE WILL. Kumbuka Ameumba Ng'ombe , Kuku , Bata ambao hawana Fres Will Je Ulitaka AKUUMBE hivyo? uwe kama Ng'ombe au SAMAKI AU simba porini anayewaza Chakula Tu hajali ameua Mtoto wake au amemuua swala bila Kuwaza Mara mbili mbili. Viumbe kama Wewe au Malaika ni VIUMBE pekee ambavyo amevipa Free Will

5. Umeuliza pia MUNGU mwenye Uwezo wote ameumbaje Binadamu anayeweza Kutenda Maovu.. JE! HUJUI KWAMBA KUNA BINADAMU AMBAO HAWATENDI MABAYA NA WAPO DUNIANI? Toka azaliwe ameishi kwa kumtumikia Mungu bila kutenda uovu JE hao unawazungumziaje?

Mfano Mzuri ni AYUBU Ambaye hakumtendea Mungu ubaya wala UOVU wowote ule. Lakini SHETANI alimvamia na kumtia magonjwa ila AYUBU hakukubali kutenda UOVU na MUNGU ALIMLIPA MARA MBILI Akamzawadiwa Mara mbili ya Utajiri wake aliokuwa nao

6. Umeuliza Pia Mungu ameshindwaje Kuumba Binadamu wema tu. Je nikuulizd Wewe je UNASHINDWA KUWA MWEMA MAISHA YAKO YOTE ? Unaweza si ndio ila UTACHAGUA MWENYEWE kuua, kuiba, kusema Uongo na kutamani Vitu Viovu. Ila UNAWEZA KUWA MWEMA BILA SHURUTI
Sasa Kwanini Kama Wewe unaweza Kuamua Hata KESHO kutokusema UONGO siku nzima uanze Kumlaumu Mungu. Hujui AMESHAKUUMBA wewe mwema toka Tumboni mwa Mama Yako
Kula chuma hicho
Isaya 45:7
"Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote"
 
Kula chuma hicho
Isaya 45:7
"Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote"
Mstari Huo Umetoka Isaya 45:7 ndio.. Mungu alikuwa anamwambia Mfalme Koreshi kwamba Atawaangamiza wafalme Wengine na Atawaletea Mabalaa wafalme hao watakaopigana na Mfalme Koreshina Ndio maana Akatamka maneno hayo Kwamba Yeye ni Mungu wa Mwanga na Giza na Anasababisha Pia Ubaya kwa Wafalme wengine wasiomwamnin yeye maana Yeye ni Mungu Mmoja na Hakuna Mwingine zaidi yake. Soma Isaya 45:5 utaelewa lengo la Matamko hayo

Ndio maana ya Mstari Huo Kwamba Atawaletea Mabalaa na Kuvunja Vunja Milango yao ya Shaba na Alimwambia Mfalme Koreshi kwamba Atamtangulia Na Kuisawazisha Milima ili ajue kwamba Yeye ni Mungu wa Israeli na Pia anaweza Kuleta Mabalaa kwa Wafalme wengine si Mungu wa Ubaya kama.Ww unavyotaka Kuiweka
 
Nope,
Warumi 9: 17-18
Yeye ndiye aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu kwa makusudi na malengo yake, Farao alikuwa akikamilisha tu drama yake yake kama mojawapo ya character 😁
 
Nope,
Warumi 9: 17-18
Yeye ndiye aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu kwa makusudi na malengo yake, Farao alikuwa akikamilisha tu drama yake yake kama mojawapo ya character 😁
Ndio ili Ajue Nguvu yake Ipoje Kushinda Nguvu za Miungu wa Misri maana Pharao alikuwa anaitegemea Miungu yake Imsaidie kukabiliana na Nguvu za Mungu.

Kama Mungu asingeufanya Moyo wa Pharao kuwa mgumu(kukataa kuwaruhsu wana wa Israel kuondoka) unadhani Angejuaje Kwamba Mungu ana Nguvu kuliko Miungu yake ya Kuchonga?

Kila Jambo analolifanya Ni kwa UTUKUFU wake hata YUDA aliyemsalifi Yesu alikuwa kwenye Mpango wake mwenyewe wa Ukombozi. Je kama Yuda asingepewa Moyo Mgumu wa Kumsaliti Yesu unadhani Ukombozi ungekuwepo.

Ni kama Wewe Hivyohivyo Unavyoona Kama Hakuna Mungu, Mungu anatutesa tu,Hatupendi(Moyo mgumu) ila Baadae unaweza Ukapatwa na Jambo Ukasema Kweli Mungu Yupo
 
Kama Mungu alijua hapendi mabaya yafanyike, kwa nini aliruhusu mabaya yawepo?

Kama huyo Mungu hakupenda na hapendi binadamu afanye mabaya, kwa nini aliweka uwezo wa binadamu kuchagua kutenda mabaya?

Kama huyo Mungu hapendi mabaya yafanyike, kwa nini hakuyazuia yasiwepo kabisa duniani?

Kwa nini uhuru wa binadamu utegemee uwepo wa mabaya?

Kwani binadamu hawezi kuwa mwenye uhuru pasipo mabaya kuwepo?
Kuna mwingine yupo Lodge Sasa hivi baada ya round 2 na Sasa ni Mapumziko, anazini na Mke wa jirani yake....!
Kwenye Mapumziko kidogo ili aje atafute Goli la 3, kampigia simu jamaa yake sana, na wanabishana kuhusu Mungu, huyu Mzinzi ambaye yupo Lodge saa hii na Mke wa jirani yake, anamuuliza Maswali sawa na haya ulouliza hapa, Yani vile vile...!

Sasa mm najiuliza, huyu jamaa hata Condom hatuamini, akija kuambukizwa ukimwi hapa, Kuna siku ataanza kusema Kwa Nini Mungu hakuondoa Ukimwi...!?

Mkuu sio wewe, nazungumzia yule Mzinzi ambaye yupo Lodge muda huu na Mke wa jirani yake.
 
Mtoto wa mwaka 1995 au 1980 unataka apewe Fursa ipi iliyotokea wakati Dunia inaumbwa na Wazazi wa kwanza wanaumbwa?

Na Je! Mungu aliposema UTAKUFA HAKIKA. Ulidhani Kufa kwa Njaa siyo KIFO? , Kufa kwa Kukatwa mapanga Njiani ukitokea kwenu siyo KIFO.

JE! hujawahi kusikia Neno LAANA, laana anaweza Kufanya Babu Yako jambo lisimpate Yeye ila Likawapata Wajukuu zake hiyo Ndio maana Ya Laana hata Kama HUKUWEPO
Sasa katika mahakama za Dunia tu hata zilizo duni kama za Tanzania huwezi kumuhukumu mtu kwa makosa ya mtu kwa makosa hata ya baba na mama yake waliomzaa, sasa huyo mungu wenu yeye anahukumuje watu kwa mababu walioishi miaka elfu sita iliyopita??
 
Kumbe huyo Mungu aliumba viumbe wenye uwezo wa kutomtumikia halafu hapohapo anataka kutumikiwa.

Huyo Mungu wenu ana ugua ukichaa.

Yani anataka kutumikiwa, lakini anaumba viumbe wenye uwezo wa kutomtumikia.

Halafu asipotumikiwa anatoa adhabu, wakati ni yeye mwenyewe, aliumba viumbe wenye uwezo wa kutomtumikia.

Huyo Mungu wenu, pamoja na nyie waamini wake, hamjielewi kabisa!
1. Aliumba Viumbe wengi na Mojawapo ni Wewe aliyekupa FREE WILL wengine wapo ambao hawajapewa Uwezo huo. Je Hao Unawasemeaje!?. Mfano Kuku , Samaki , Ng'ombe n.k
Kwahiyo Ni Maamuzi yako mwenyewe KUTOMTUMIKIA AU KUMTUMIKIA hakulazimishi ila Amekupa Tahadhari kama Alivyokupa Tahadhari Kwenye BUSTANI YA EDENI kwamba Alikuumba ili Umtumikie Yeye peke yake na Ndio lengo lake uone UTUKUFU wake kwamba Ni Mwema. Ila Ukichagua KUTOMTII MUUMBA WAKO kuna Adhabu kwa Ww kutomtii MUUMBA WAKO Kwahiyo hata Muda Huu unaotumia JF amekupatia ili Siku Moj Ubadilike utubu dhambi zako na Uweze Kumrithi ufalme wake hapo Mwisho utakapofika

2. Unaposema Wasiomtii anawapa ADHABU mbona Usemi Kuna Ambao WAMEMTII hawatapewa ADHABU. Je hao waliomtii Wamewezaje kumtii na WEWE ukashindwa.? Huoni kwamba UMECHAGUA mwenyewe Kutomtumikia YEYE. yaani Mdogo wako au Baba yako , au mama yako wamemtumikia na Ukawakuta Mbinguni wewe Ulishindwaje ukatupwa MOTONI ? Maana yake Ulikuwa na Uwezo wa KUMTUMIKIA NA kuacha DHAMBI ila Ulichagua Upande Wa UOVU mwenyewe
 
Sasa katika mahakama za Dunia tu hata zilizo duni kama za Tanzania huwezi kumuhukumu mtu kwa makosa ya mtu kwa makosa hata ya baba na mama yake waliomzaa, sasa huyo mungu wenu yeye anahukumuje watu kwa mababu walioishi miaka elfu sita iliyopita??
Nenda KOREA KASKAZINI. Baba yako akikosea hata wewe utahukumiwa kwa Makosa ya Baba yako na kizazi chako pia au Korea Kaskazini haipo Duniani!?

MUNGU Alimuonya ADAM mapema kabisa(kama Wewe mama yako alipokuwa anakuambia OTO OTO OTO ila ukawa mkaidi ukashika moto jikoni ukaungua ). Hivyo hivyo Mungu alipomuumba Adam na EVA aliwapa ONYO , hakuwaumba Kama ROBOTI aliwaumba Viumbe Wenye Uelewa wa kukataa na KUKUBALI jambo. Kwahiyo USIMLAUMU Mungu kwa Makosa Yako mwenyewe maana Alikukataza.

SHETANI alipokuja EVA NA ADAM walijua kabisa kwamba Tunda Hili TULIKATAZWA KULILA ila Shetani ametuambia Tutakuwa kama Mungu halafu Hatutakufa kama MUNGU alivyosema kwa maneno ya Uongo ya Shetani (wakawaka Tamaa kwamba Watakuwa na Nguvu kama Mungu na Hawatakufa) sasa kwann tusile Uwenda MUNGU anatuonea Wivu tutafanana na Yeye basi Tule ili Tuwe sawa na YEYE. Sasa unamlaumuje Mungu kwa Kosa lako na Tamaa zako mwenyewe maana Akili yako ilitaka kuwa kama Yeye

HATA Wewe ushatamani Kuwa kama BOSS wako , Binadamu wengi hujawa na Tamaa ya Kutaka kuwa kama Boss wake Kazini na Humfanyia Fitina na Chuki na Kumchongea ili Akae kwenye Kiti chake hii ndio LAANA tuliyoipokea Toka MWANZO KWAHIYO usilaumu. OMBA REHEMA NA MSAMAHA kwamba ULIKOSEA
 
North Korea ni shithole, hauwezi kuwa mfano mzuri kwa mungu wako, anaweza kufanya vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom