Binadamu Kumlaumu Mungu kwa Makosa Yake Mwenyewe.

Unapokuwa huwezi Kufahamu jambo unawezaje Kuuliza Wengine Jambo ambalo ww unasema Ni Ngumu Kufahamu?

Kama Wengine wanakuambia Chanzo ni Mungu ila Wewe unakataa ila Ukiulizwa wewe unasema ni Ngumu Kufahamu ina Maana Huna Ukweli Mwingine unaoweza Kupita Ukweli Tulionao Sisi ..ndio maana Unashindwa kufahamu

Kama Una Ukweli Kuzidi Huu ndio Uanze Kubisha...
Unathibitishaje chanzo ni Mungu?

Kwa sababu kwanza, hujathibitisha Mungu yupo.

Unafosi tu, Mungu ni chanzo. Wakati bado umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.
 
1. Farao wa Misri alijua Yupo kwa kupigwa mapigo
2. Mfalme Wa Babylon alidhibitisha Yupo kwa Daniel Kushindwa Kuliwa na Simba Wenye Njaa
3. Eliya aliomba Mungu Moto ukashuka mbele ya Watu wasioamini

YOTE KWA YOTE. YESU ALIKUJA NA KUFANYA MIUJIZA MBELE YA WASIOAMINI NA WAKAAMINI KWAMBA MUNGU YUPO.

Huwezi muona kwa Macho maana Siyo kuku, bata , au samaki mwenye Mwili Yeye ni ROHO
Hayo yote hujathibitisha yametokea. Huyo Daniel hata hujathibitisha alikuwapo kweli.
 
Ningekuwa na uwezo wa kuumba mtoto ambaye hawezi kunitukana ningefanya hivyo.

Lakini sina uwezo huo, kwa sababu siwezi mambo yote.

Sasa Mungu ambaye mnadai anaweza yote, Alishindwaje kuumba binadamu ambao hawataweza kumkana, kumuasi na kutenda mabaya?

Ningekuwa na uwezo wa kuzaa watoto ambao hawanikosei, ningefanya hivyo.

Lakini siwezi kufanya hivyo, kwa sababu sina uwezo huo na siwezi mambo yote.

Sasa huyo Mungu wenu mnayedai anaweza yote, Kama hapendi binadamu wamkosee, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kumkosea?
Nami Nimeshakuambia Huko Nyuma na Nakuambia Tena. Ni nani aliyekuambia Binadamu wote wanatenda Mabaya? Binadamu wote wana-asi.

Hujui kuna Binadamu ambaye hajawahi kutenda Mabaya maisha Yake yote na Hajawahi kumu-asi Mungu ?

Na Nilikupa Mfano. AYUBU hakuwahi Kutenda Dhambi na Kumuasi Mungu. Unaposema Mungu ameumba Binadamu anayeweza Kumuasi Unazungumziaje Ambao hawajawahi Kuasi

Unawazungumziaje Binadamu hao ??
 
mbona wewe unakataa pia madai ya jamaa kwamba "hakuna chanzo" ? sababu unazotumia wewe kukataa na yeye anatumia kukataa madai yako - mjadala sio rahisi namna hiyo mkuu
Ukikataa Jambo Basi Uwe na Uthibitisho wowote wa Kukataa. Maana Mimi Nimetoa Mifano ya Uwepo wa Mungu. Nikasema Alikuwepo Mussa aliyedhibitisha Mungu Yupo, Alikuwepo Eliya , Alikuwepo Pia YESU KRISTO na alitenda Miujiza Mingi akafanya Kudhibitisha Kuwa Mungu Yupo kupitia Miujiza hiyo aliomba Kwa Jina Lake MUNGU naye MUNGU akamjibu kama Asingekuwepo basi Miujiza Hiyo Isingekuwepo na Isingetokea, manaa Yake MUNGU alimsikiliza

Basi WEWE una Ukweli Gani Tofauti na Wangu tuusikilize
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hayo yote hujathibitisha yametokea. Huyo Daniel hata hujathibitisha alikuwapo kweli.
Kivipi ? Maana Imeandikwa Walikuwepo na Walitenda Miujiza Kwa Kumuomba MUNGU NAYE akawajibu..

Maana Ukisema Tu kwamba Haijadhibitishwa hata Mtu aliyezaliwa 2010 anaweza Kukuambia NYERERE hakuwepo. Ili umdhibitishie lazima Umpe Maandishi asome Historia yake.
 
Unathibitishaje chanzo ni Mungu?

Kwa sababu kwanza, hujathibitisha Mungu yupo.

Unafosi tu, Mungu ni chanzo. Wakati bado umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.
Nimekuambia Kwamba Chanzo ni Yeye maana ninaamini katika Manabii aliowatuma na YESU KRISTO Mwenyewe

Hakuna Nabii aliyefanya JAMBO kwa Nia Yake Binafsi bali ALIMUOMBA MUNGU akajibu. Sasa Unataka Nidhibitishe Vipi zaidi ya Hapo.

1.YESU alimuomba MUNGU Amfufue Lazaro naye akafufuka

Unataka Nidhibitishe vipi Kwamba Mungu Yupo zaidi ya Haya niyasemayo..

WEWE NDIO UNATAKIWA KUNIJIBU KWAMBA hamna MUNGU maana Hao wote hawakujibiwa Walichoomba
 
Ukikataa Jambo Basi Uwe na Uthibitisho wowote wa Kukataa. Maana Mimi Nimetoa Mifano ya Uwepo wa Mungu. Nikasema Alikuwepo Mussa aliyedhibitisha Mungu Yupo, Alikuwepo Eliya , Alikuwepo Pia YESU KRISTO na alitenda Miujiza Mingi akafanya Kudhibitisha Kuwa Mungu Yupo kupitia Miujiza hiyo aliomba Kwa Jina Lake MUNGU naye MUNGU akamjibu kama Asingekuwepo basi Miujiza Hiyo Isingekuwepo na Isingetokea, manaa Yake MUNGU alimsikiliza

Basi WEWE una Ukweli Gani Tofauti na Wangu tuusikilize
uthibitisho ni kitu complex mkuu,
 
Kivipi ? Maana Imeandikwa Walikuwepo na Walitenda Miujiza Kwa Kumuomba MUNGU NAYE akawajibu..

Maana Ukisema Tu kwamba Haijadhibitishwa hata Mtu aliyezaliwa 2010 anaweza Kukuambia NYERERE hakuwepo. Ili umdhibitishie lazima Umpe Maandishi asome Historia yake.
Kuandikwa haithibitishi mtu alikuwapo.

Kuna somo linaitwa historicity, jinai ya kuthibitisha kama kilichoandikwa kilitokea kweli au ni hadithi za kuungaunga tu, inaonekana hulielewi.
 
1. Mungu hakumruhusu Nyoka Kuingia Bustanini. Nyoka Yule alikuwa tayari ameshamhasi Mungu , kwahiyo alikuwa anafanya Mambo Yake kuharibu Uuambaji wa Mungu, Na Pia Eva Alikuwa na Haki ya Kukataa au Kukubali Ila Kwa Vile Alidanganywa kama Mm na Wewe tunavyoweza Kudanganywa na Marafiki zetu tukaingia Matatizoni. Mfano Unaweza Pia Ww kudanganywa Kwamba Ukaibe benki pesa 💰 utajirike, ingawa ushaambiwa Kuiba Benki utafungwa jela Hakika ila Ukaenda ukaiba na Ukafungwa kweli. Je utamlaumu Mungu kwanini alimruhusu Rafiki yako Akudanganye

2. Mpango wa Mungu upo Pale pale Kwamba Uwe na Uzima wa Milele. Hajawahi kupanga Uangamie Hata Siku Moja. Ni WEWE mwenyewe Ulijiangmiza Ulipodanganywa na Nyoka. Usimlaumu Mungu. Maana Alikuambia HAKIKA UTAKUFA ila Wewe nyoka alipokuambia Kwamba Ukila Utakuwa kama Mungu ukijua Mema na Mabaya ukawaka Tamaa kwamba Utakuwa kama Mungu. Kwahiyo Mungu hajawahi Kuruhusu mambo mabaya Yakutokee ila Wewe mwenyewe una Uhuru Huo wa Jambo Baya Likutokee.

3. Mungu Hakuzembea Wala hakufungi Mnyororo wewe kwenda Popote utakapo hata shetani 👿alivyomhasi alimtupa Chini na Akamwambia atamhukumu siku yake ikifika. Wewe Ukitenda Dhambi anakupa Muda wa kujirekebisha na Kumrudia maana Ameshakupa Neema Ya Kukusamehe kupitia Yesu Kristo Mwenyewe kwamba kwa Vile Ulipoteza Neema Hiyo basi Anakurudishia Tena kwa Njia Ya Yesu Kristo Mwanae
Kitendo tu cha kumuumba shetani ni lawama tosha!
 
Nami Nimeshakuambia Huko Nyuma na Nakuambia Tena. Ni nani aliyekuambia Binadamu wote wanatenda Mabaya? Binadamu wote wana-asi.

Hujui kuna Binadamu ambaye hajawahi kutenda Mabaya maisha Yake yote na Hajawahi kumu-asi Mungu ?

Na Nilikupa Mfano. AYUBU hakuwahi Kutenda Dhambi na Kumuasi Mungu. Unaposema Mungu ameumba Binadamu anayeweza Kumuasi Unazungumziaje Ambao hawajawahi Kuasi

Unawazungumziaje Binadamu hao ??
Kwa hiyo Mungu aliumba baadhi ya binadamu wamuasi na baadhi wasi muasi?
 
Nimekuambia Kwamba Chanzo ni Yeye maana ninaamini katika Manabii aliowatuma na YESU KRISTO Mwenyewe

Hakuna Nabii aliyefanya JAMBO kwa Nia Yake Binafsi bali ALIMUOMBA MUNGU akajibu. Sasa Unataka Nidhibitishe Vipi zaidi ya Hapo.

1.YESU alimuomba MUNGU Amfufue Lazaro naye akafufuka

Unataka Nidhibitishe vipi Kwamba Mungu Yupo zaidi ya Haya niyasemayo..

WEWE NDIO UNATAKIWA KUNIJIBU KWAMBA hamna MUNGU maana Hao wote hawakujibiwa Walichoomba
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Unathibitishaje huyo Mungu unayedai kumwamini ni ukweli na si uongo?

Kwa sababu hata uongo unaweza kuaminiwa vilevile.
 
Kwa hiyo Mungu aliumba baadhi ya binadamu wamuasi na baadhi wasi muasi?
Hakuumba Wanadamu wanaotenda Mema na wanaotenda Mabaya KAMWE. Ila Aliumba Binadamu ambaye Atakuwa Huru katika Kuchagua Mambo Mema na Mabaya

Hata Wewe Unaweza Ukaamua mjikusanye Kundi la Vijana mkaibe Benki na Utajirike Uache Kufanya Mjadala na Mimi.. Ila Kwanini unashindwa? Manaa Ushaambiwa Ukifanya Hivyo UTAFUNGWA au UTAUAWA

Ndicho Mungu alichowaambia ADAM na EVA Mkila Tunda Hilo Hakika Mtakufa. Sasa Tuweke Mfano Hilo Tunda ni BENKI na ADAM na EVA wakadanganywa na SHETANI kwamba wakienda Kuiba Benki hawatafungwa wala Hawatauawa ila Watakuwa na Pesa nyingi kama Mungu, wakawaka Tamaa kwamba Watakuwa kama Mungu wakiamininShetani uenda akawa Sahihi..Na Walipojaribu Kwenda Kuiba BENKI wakamatwa Wakafungwa au Kuuawa... Wakajuta sana kwa Kitendo hicho baada ya Kufanya(Utenda Ovu lazima Ujute ila Ukitenda Jema Hujuti kamwe)

JE! Kosa La Mungu Hapo Ni Nini? Na utasema MUNGU aliumba Viumbe Vitakavyomuasi. ? Hujui HATA shetani alipewa UHURU huo na AKACHAGUA kuasi mwenyewe kwa ROHO yake Bila Kushurutishwa na Kiumbe Kingine na Akawadanganya Malaika wengine pia ila WALIKATAA KUMFUATA(Free will yao ilichagua hivyo) ila Wengine wakamfuata(free will yao ilichagua Kumfuata)..
 
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Unathibitishaje huyo Mungu unayedai kumwamini ni ukweli na si uongo?

Kwa sababu hata uongo unaweza kuaminiwa vilevile.
Sijaamini UONGO.

Kama Ningeamini UONGO ningekuwa na Hatia kwamba YESU alipomuomba Mungu ili Amfufue LAZARO , Mungu hakumjibu na Wala LAZARO hakukufufuka bali alibaki Kaburini tu...

Na Naweza Thibisha Kwamba Ni Mungu kweli na Sijaamini UONGO Maana YESU alimuomba Na akajibu hakuna Alichoomba Akanyimwa.
1. Alimuomba Mungu abariki Mikate mitano na Samaki Wawili ikabarikiwa Ikaongezeka Ikawa Mingi watu wakala zaidi ya 5000
2. Alimuomba Mungu Lazaro afufuke akafufuka Kweli na hata Wasioamini (waroma kipindi hicho) walishuhudia Muujiza Huu na Lazaro akawa anapita Mitaani na Mafarisayo walitaka kumuua Lazaro ili Kutomfanya Yesu Kuwa Maarufu kwa Muujiza Huu..
3. MUSSA Aliomba Mungu , Mungu akajibu Bahari ikapasuka Waisraeli wakapita.

Mifano Ni Mingi Ipo Ambayo Inathibitisha kwamba Niaminicho Ni Kweli na Si naamini UONGO
 
Hakuumba Wanadamu wanaotenda Mema na wanaotenda Mabaya KAMWE. Ila Aliumba Binadamu ambaye Atakuwa Huru katika Kuchagua Mambo Mema na Mabaya
Kwa nini Mungu atoe adhabu kwa watakao tenda mabaya, wakati anajua kabisa watu wako huru kutenda mabaya?

Kama kuna adhabu kwa mtu kuchagua kutenda mabaya, Sasa mtu atakuwaje huru kutenda mabaya?

Wakati anajua kuna adhabu ipo.

Huoni kwamba huo uhuru haupo?
Hata Wewe Unaweza Ukaamua mjikusanye Kundi la Vijana mkaibe Benki na Utajirike Uache Kufanya Mjadala na Mimi.. Ila Kwanini unashindwa? Manaa Ushaambiwa Ukifanya Hivyo UTAFUNGWA au UTAUAWA

Ndicho Mungu alichowaambia ADAM na EVA Mkila Tunda Hilo Hakika Mtakufa. Sasa Tuweke Mfano Hilo Tunda ni BENKI na ADAM na EVA wakadanganywa na SHETANI kwamba wakienda Kuiba Benki hawatafungwa wala Hawatauawa ila Watakuwa na Pesa nyingi kama Mungu, wakawaka Tamaa kwamba Watakuwa kama Mungu wakiamininShetani uenda akawa Sahihi..Na Walipojaribu Kwenda Kuiba BENKI wakamatwa Wakafungwa au Kuuawa... Wakajuta sana kwa Kitendo hicho baada ya Kufanya(Utenda Ovu lazima Ujute ila Ukitenda Jema Hujuti kamwe)

JE! Kosa La Mungu Hapo Ni Nini? Na utasema MUNGU aliumba Viumbe Vitakavyomuasi. ? Hujui HATA shetani alipewa UHURU huo na AKACHAGUA kuasi mwenyewe kwa ROHO yake Bila Kushurutishwa na Kiumbe Kingine na Akawadanganya Malaika wengine pia ila WALIKATAA KUMFUATA(Free will yao ilichagua hivyo) ila Wengine wakamfuata(free will yao ilichagua Kumfuata)..
Kwa nini Mungu aweke freewill ya binadamu kuweza kuchagua kutenda mabaya wakati anajua kabisa hapendi mabaya yafanyike?

Kwa nini freewill haiwezi kuwepo bila mabaya kutendeka?
 
Sijaamini UONGO.

Kama Ningeamini UONGO ningekuwa na Hatia kwamba YESU alipomuomba Mungu ili Amfufue LAZARO , Mungu hakumjibu na Wala LAZARO hakukufufuka bali alibaki Kaburini tu...

Na Naweza Thibisha Kwamba Ni Mungu kweli na Sijaamini UONGO Maana YESU alimuomba Na akajibu hakuna Alichoomba Akanyimwa.
1. Alimuomba Mungu abariki Mikate mitano na Samaki Wawili ikabarikiwa Ikaongezeka Ikawa Mingi watu wakala zaidi ya 5000
2. Alimuomba Mungu Lazaro afufuke akafufuka Kweli na hata Wasioamini (waroma kipindi hicho) walishuhudia Muujiza Huu na Lazaro akawa anapita Mitaani na Mafarisayo walitaka kumuua Lazaro ili Kutomfanya Yesu Kuwa Maarufu kwa Muujiza Huu..
3. MUSSA Aliomba Mungu , Mungu akajibu Bahari ikapasuka Waisraeli wakapita.

Mifano Ni Mingi Ipo Ambayo Inathibitisha kwamba Niaminicho Ni Kweli na Si naamini UONGO
Sasa unaleta hadithi za Biblia unasema sio uongo?

Unathibitishaje huyo Yesu alilisha watu 5000?

Ulikuwepo huyo Yesu akilisha watu?

Unathibitishaje Lazaro alifufuliwa?

Ulikuwepo Lazaro akifufuliwa?

Au unaleta hadithi za kutungwa za hekaya za Biblia?
 
Kwa nini Mungu atoe adhabu kwa watakao tenda mabaya, wakati anajua kabisa watu wako huru kutenda mabaya?

Kama kuna adhabu kwa mtu kuchagua kutenda mabaya, Sasa mtu atakuwaje huru kutenda mabaya?

Wakati anajua kuna adhabu ipo.

Huoni kwamba huo uhuru haupo?

Kwa nini Mungu aweke freewill ya binadamu kuweza kuchagua kutenda mabaya wakati anajua kabisa hapendi mabaya yafanyike?

Kwa nini freewill haiwezi kuwepo bila mabaya kutendeka?
1. Umeuliza Kwanini Mungu atoe Adhabu kwa Watendao mabaya...
unauliza Hilo Mbona Uulizi pia Kwanini MAHAKAMA inakupa Adhabu ya Kifo, Wewe Mwenyewe Ukiua ? Kwanini Isikuache Tu uendelee na Maisha Yako.. Kama BINADAMU Mnajiadhibu Wenyewe Mkitenda MABAYA unaulizaje hilo Swala Kwa MUNGU kwanini Akuadhibu..

2. Umeuliza kama Kuna Uhuru(free will ) ya Kutenda mabaya kwanini watu wasiachwe kutenda mabaya. Basi tuwape Uhuru huo Halafu watu waje KUUA familia Yako Wwe na Watoto wako , au Wazazi wako .. Halafu Hutakiwi Kulia Wala Kuumia UWAACHE maana Wametenda mabaya Maana Kwako Mabaya Hayana Madhara na Unayapenda sana Kuliko MEMA. Wakikuua hata Ww au Mkeo unatakiwa Kucheka Tu Usilie wala Kwenda Kushtaki Popote

3. Umeuliza Pia Kwanini MUNGU aweke freewill. Mungu aliweka Free will ili UWeze Kutambua Kwamba Swala Hili(kuua, uwongo,uasheratu) ni BAYA na Swala Hili Ni ZURI. hakuweka Ili Uwe Huru Kuchagua Mabaya na Kuacha Mema.. Hata BINADAMU SISI hata Wasiomjua Mungu Wamejiwekea Sheria UKITENDA MABAYA utaadhibiwa na UKITENDA mema Utaishi kwa UHURU.
Nilikuuliza Huko Nyuma Mwanao Akikutukana utamuacha Tu kwa Sababu Ana Uhuru wa Kukutukana ?

4. Pia umeuliza je Freewill haiwezi kuwepo bila Mabaya kutendeka..? Nadhani unauliza kile kile ambacho nishakujibu. Kwamba Kuna Binadamu hawatendi mabaya na Wamechagua Kufanya hivyo na Wanauwezo huo huo wa kutenda Mabaya ila Wamechagua Kuwa WEMA maisha Yao yote. Hata wewe unaweza
 
Sasa unaleta hadithi za Biblia unasema sio uongo?

Unathibitishaje huyo Yesu alilisha watu 5000?

Ulikuwepo huyo Yesu akilisha watu?

Unathibitishaje Lazaro alifufuliwa?

Ulikuwepo Lazaro akifufuliwa?

Au unaleta hadithi za kutungwa za hekaya za Biblia?
Unasema Biblia ni Hadithi za UONGO haya Basi na Nilitaka Uje Hapo hapo Useme kwamba Ni Hadithi.. Basi Soma Hapa

Uwepo wa Yesu wa Nazareti na matendo yake ya ajabu (miujiza) unathibitishwa na vyanzo vingi vya kihistoria nje ya Biblia, vikiwemo vya waandishi wa Kiyahudi, Warumi, na hata wakosoaji wa kale wa Kikristo. Wanahistoria wengi duniani wanakubali kuwa Yesu alikuwa mtu halisi wa kihistoria aliyewahi kuishi karne ya kwanza.
Hapa chini kuna vyanzo muhimu vya kihistoria visivyo vya kibiblia vinavyozungumzia uwepo wake na miujiza yake:

1. Flavius Josephus (Mwanahistoria Myahudi – Karne ya 1)

Flavius Josephus ndiye chanzo cha karibu zaidi kisicho cha kibiblia tulicho nacho. Katika kitabu chake maarufu cha Jewish Antiquities (mwaka 93-94 BK), anamrejelea Yesu mara mbili:
• Kuhusu Miujiza: Katika sehemu inayojulikana kama Testimonium Flavianum, Josephus anamuelezea Yesu kama "mtu mwenye hekima" aliyefanya "mambo ya ajabu/matendo ya kushangaza" (kwa Kigiriki: paradoxa), neno ambalo lilitumika kumaanisha miujiza au matendo yasiyo ya kawaida.
• Kuhusu Kifo na Uwepo: Anataja pia kuwa alisulubiwa chini ya Pontio Pilato na kwamba alikuwa na ndugu aliyeitwa Yakobo.

2. Cornelius Tacitus (Mwanahistoria wa Kirumi – Karne ya 2)
Tacitus anachukuliwa kuwa mmoja wa wanahistoria waaminifu na wakubwa wa Dola ya Kirumi. Katika maandiko yake ya Annals (mwaka 116 BK), alieleza jinsi Kaisari Nero alivyowashtaki Wakristo kwa moto wa Roma. Tacitus aliandika kwa uwazi kuwa jina lao lilitokana na "Kristo (Christus), aliyeuawa kwa adhabu kali wakati wa utawala wa Tiberio, chini ya procurator Pontio Pilato." Huu ni uthibitisho thabiti wa kisiasa kutoka kwa adui wa Ukristo kuhusu uwepo na kuuawa kwa Yesu. [1, 2, 3, 4]

3. Talmud ya Kiyahudi (Maandiko ya Kirabi – Karne za Mapema)
Talmud ya Babeli (Sanhedrin 43a) inatoa ushuhuda wa kipekee kwa sababu inatoka kwa maadui wa kidini wa Yesu. Maandiko haya hayakanushi kuwa Yesu alifanya mambo ya ajabu, badala yake yanataja kuwa: "Yesu aliuawa usiku wa kuamkia Pasaka kwa sababu alijihusisha na uchawi na kuwapotosha Waisraeli." Wanahistoria wanabainisha kuwa kuita miujiza yake "uchawi" ni uthibitisho wa maadui kwamba kweli alifanya matendo yasiyo ya kawaida ambayo hawakugundua chanzo chake. [1, 2, 3, 4]

4. Celsus (Mwanafalsafa wa Kigiriki na Mkosoaji wa Ukristo – Mwaka 175 BK)
Celsus alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa kwanza kuandika kitabu dhidi ya Ukristo. Katika maandiko yake yaliyohifadhiwa kupitia majibu ya mwanateolojia Origen, Celsus hakubisha kamwe ikiwa Yesu alikuwepo. Badala yake, alidai kuwa Yesu alikulia Misri ambako alijifunza nguvu za uchawi, na aliporudi Israeli alitumia nguvu hizo kujitangaza kuwa Yeye ni Mungu. Hili linathibitisha kuwa hata wakosoaji wa karne ya pili walikiri uwepo wa nguvu za miujiza za Yesu lakini wakatafuta vyanzo mbadala vya nguvu hizo. [1, 2, 3]

HAYA KAMA BIBLIA Unasema Ni HADITHI basi Nimekuwekea VYANZK nje na BIBLIA..

MAANA kuna Watu wanaweza Kusema Hajawahi Kuwepo Mtu aliyeitwa NYERERE nchini Tanzania kwa Sababubamezaliwa 2006 ukawapa Maandishi yako mwenyewe wakakataa unatakiwa Uwaaminishe nje ya Maandishi yako nami Nimefanya Hivyo hivyo
 
Vitabu vinavyo daiwa na kuaminiwa kwamba ni vya Mungu ni vingi sana.

Kuna hiyo Biblia yenu. Ninyi wakristo.

Kuna Quran ya waislamu.

Kuna Torah ya wayahudi.

Kuna Tripitaka ya wabudha.

Kuna The Vedas ya wahindu.

Kuna The Kojik ya washinto kule Japan.

Kuna The Guru Granth Sahib ya wasikhism.

Kuna Rastafar Bible ya Rastafarians.

Sasa wewe unathibitishaje kwamba Biblia yako tu ndilo neno la Mungu?

Wakati kuna maandiko mengi tu yanayo aminiwa kwamba ni ya Mungu.

Au unatetea Biblia tu, kwa vile ndivyo ulivyo kariri na kuaminishwa?
 
1. Umeuliza Kwanini Mungu atoe Adhabu kwa Watendao mabaya...
unauliza Hilo Mbona Uulizi pia Kwanini MAHAKAMA inakupa Adhabu ya Kifo, Wewe Mwenyewe Ukiua ? Kwanini Isikuache Tu uendelee na Maisha Yako.. Kama BINADAMU Mnajiadhibu Wenyewe Mkitenda MABAYA unaulizaje hilo Swala Kwa MUNGU kwanini Akuadhibu..

2. Umeuliza kama Kuna Uhuru(free will ) ya Kutenda mabaya kwanini watu wasiachwe kutenda mabaya. Basi tuwape Uhuru huo Halafu watu waje KUUA familia Yako Wwe na Watoto wako , au Wazazi wako .. Halafu Hutakiwi Kulia Wala Kuumia UWAACHE maana Wametenda mabaya Maana Kwako Mabaya Hayana Madhara na Unayapenda sana Kuliko MEMA. Wakikuua hata Ww au Mkeo unatakiwa Kucheka Tu Usilie wala Kwenda Kushtaki Popote

3. Umeuliza Pia Kwanini MUNGU aweke freewill. Mungu aliweka Free will ili UWeze Kutambua Kwamba Swala Hili(kuua, uwongo,uasheratu) ni BAYA na Swala Hili Ni ZURI. hakuweka Ili Uwe Huru Kuchagua Mabaya na Kuacha Mema.. Hata BINADAMU SISI hata Wasiomjua Mungu Wamejiwekea Sheria UKITENDA MABAYA utaadhibiwa na UKITENDA mema Utaishi kwa UHURU.
Nilikuuliza Huko Nyuma Mwanao Akikutukana utamuacha Tu kwa Sababu Ana Uhuru wa Kukutukana ?

4. Pia umeuliza je Freewill haiwezi kuwepo bila Mabaya kutendeka..? Nadhani unauliza kile kile ambacho nishakujibu. Kwamba Kuna Binadamu hawatendi mabaya na Wamechagua Kufanya hivyo na Wanauwezo huo huo wa kutenda Mabaya ila Wamechagua Kuwa WEMA maisha Yao yote. Hata wewe unaweza
Kwa nini binadamu akichagua kutenda mabaya aadhibiwe?

Wakati yuko huru kutumia freewill ileile iliyowekwa kufanya chochote apendacho.

Kama binadamu akitenda mabaya ata adhibiwa, huoni kwamba uhuru wa kutenda mabaya unakuwa haupo kwa sababu ya mtu kuhofia adhabu?

Ni sawa na wewe umwambie mwanao yuko huru kwenda shuleni kusoma au kubaki nyumbani kucheza, Lakini endapo atabaki nyumbani kucheza, utamchapa viboko.

Sasa hapa mtoto anakuwa hayupo huru, kwa sababu akibaki nyumbani kucheza utamchapa. Na hana budi kwenda shuleni ili akwepe viboko.

Vivyo hivyo, Kama kuna adhabu kwa kutenda mabaya, then freewill ya mtu kuchagua kutenda mabaya haipo. Kwa sababu kuna adhabu.

Na ili kukwepa adhabu, kila mtu atalazimika kutenda matendo mema.

Freewill ya kutenda mabaya inakuwa haipo. Kwa kuhofia adhabu.

Therefore, Freewill haipo na binadamu wote tunalazimika kutenda mema tu.
 
Back
Top Bottom