Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 14,578
- 31,662
Kama Mungu aliumba watu wamtumikie yeye peke yake, Kwa nini tena aweke freewill ya kutomtumikia?1. Aliumba Viumbe wengi na Mojawapo ni Wewe aliyekupa FREE WILL wengine wapo ambao hawajapewa Uwezo huo. Je Hao Unawasemeaje!?. Mfano Kuku , Samaki , Ng'ombe n.k
Kwahiyo Ni Maamuzi yako mwenyewe KUTOMTUMIKIA AU KUMTUMIKIA hakulazimishi ila Amekupa Tahadhari kama Alivyokupa Tahadhari Kwenye BUSTANI YA EDENI kwamba Alikuumba ili Umtumikie Yeye peke yake na Ndio lengo lake uone UTUKUFU wake kwamba Ni Mwema. Ila Ukichagua KUTOMTII MUUMBA WAKO kuna Adhabu kwa Ww kutomtii MUUMBA WAKO Kwahiyo hata Muda Huu unaotumia JF amekupatia ili Siku Moj Ubadilike utubu dhambi zako na Uweze Kumrithi ufalme wake hapo Mwisho utakapofika
Huu si ukichaa?
Yani anaweka freewill ya kutotumikiwa halafu asipotumikiwa anatoa adhabu!
Sasa kulikuwa na haja gani kuweka freewill ya kutotumikiwa?
Kwa nini Mungu aingilie freewill ya mtu, kuchagua kutomtumikia kwa kumpa adhabu?2. Unaposema Wasiomtii anawapa ADHABU mbona Usemi Kuna Ambao WAMEMTII hawatapewa ADHABU. Je hao waliomtii Wamewezaje kumtii na WEWE ukashindwa.? Huoni kwamba UMECHAGUA mwenyewe Kutomtumikia YEYE. yaani Mdogo wako au Baba yako , au mama yako wamemtumikia na Ukawakuta Mbinguni wewe Ulishindwaje ukatupwa MOTONI ? Maana yake Ulikuwa na Uwezo wa KUMTUMIKIA NA kuacha DHAMBI ila Ulichagua Upande Wa UOVU mwenyewe
Je huyo Mungu hajui kwamba watu wametumia freewill ileile kutomtumikia?
Kwa nini atoe adhabu, wakati freewill ya kutotumikiwa aliiweka yeye mwenyewe?
Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?