Binadamu Kumlaumu Mungu kwa Makosa Yake Mwenyewe.

Nimeamini sababu nimewakuta na kuwaona watoto zake na mke wake..!!

Vipi wewe umebahatika kumuona Yesu? Musa? Bikira Maria? Shetani?
 
Kama freewill ya kutenda mabaya imewekwa lakini hatupaswi kutenda mabaya hayo, Sasa kulikuwa na haja gani ya kuweka freewill ya kutenda mabaya?

Huyo Mungu aliweka freewill ya kutenda mabaya kama pambo tu?
SWALI Lako ni Zito sana ila Nitakujibu ili Uelewe kwanini aliweka Free will ya MEMA na MABAYA

1. Bila Uhuru wa Kuchagua Mabaya Wema Hauna Thamani,Kama Mungu angetuumba tukiwa na uwezo wa kufanya wema tu, tungekuwa kama "roboti" zilizowekwa programu (programmed robots).• Roboti ikikuletea glasi ya maji, huwezi kuishukuru kwa "wema" wake, kwa sababu haina uamuzi mwingine. Vivyo hivyo, ili utii na upendo wetu kwa Mungu na wanadamu wenzetu uwe na maana, lazima kuwe na uwezo wa kuchagua kutositii au kutopenda.

2. FREE WILL ya Ukweli lazima Iwe na UPANDE WA KUCHAGUA.
Uhuru wa kuchagua (Freewill) siyo kitu kinachoweza kugawanywa nusu. Huwezi kuwa na uhuru wa kuchagua kwenda "kulia" kama hakuna upande wa "kushoto".

3. Mungu alitaka kuumba viumbe vyenye hadhi na utu (dignity), viumbe vinavyoweza kufikiri, kupima mambo na kufanya maamuzi yao wenyewe.
Kuondoa uwezo wa kuchagua mabaya maana yake ni kuondoa uhuru wa mawazo, ubunifu, na utashi.

Kwa maana hiyo, freewill siyo pambo, bali ni msingi mkuu unaotofautisha wanadamu na viumbe visivyo na akili (kama mawe au miti).
 
Nimeamini sababu nimewakuta na kuwaona watoto zake na mke wake..!!

Vipi wewe umebahatika kumuona Yesu? Musa? Bikira Maria? Shetani?
1. Je unataka Kuniambia Mtoto atakayezaliwa 2098 atawaona Watoto wa Nyerere na Mke wake kama Wewe? Utamwaminishaje kwamba Alikuwepo Mtu aitwaye Nyerere na Si Mwingine aliyepigania Uhuru

2. Mimi sijawaona ila Ninaamini Kilichoandikwa kwamba Ni KWELI na sijapata Kuona Kweli Iliyozidi Ninayoiamini
 
Kwa nini thamani ya wema itegemee mabaya?

Kama huyo Mungu alijua hapendi mabaya yafanyike, kwa nini aliweka thamani ya wema itegemee mabaya, wakati anajua hapendi mabaya yafanyike?

Alishindwaje kuumba thamani nyingine ya wema pasipo mabaya kufanyika?
2. FREE WILL ya Ukweli lazima Iwe na UPANDE WA KUCHAGUA.
Uhuru wa kuchagua (Freewill) siyo kitu kinachoweza kugawanywa nusu. Huwezi kuwa na uhuru wa kuchagua kwenda "kulia" kama hakuna upande wa "kushoto".
Kama freewill ya ukweli lazima iwe na upande wa kuchagua, kwa nini mtu akichagua mabaya iwe si sawa?

Halafu akichagua mema iwe sawa.

Kama mtu akichagua kutenda mabaya si sawa, basi hata hiyo freewill ya kuchagua upande si sawa.

Kwa sababu ina pendelea upande mmoja tu wa kutenda mema, uonekane ndio sawa.
3. Mungu alitaka kuumba viumbe vyenye hadhi na utu (dignity), viumbe vinavyoweza kufikiri, kupima mambo na kufanya maamuzi yao wenyewe.
Kuondoa uwezo wa kuchagua mabaya maana yake ni kuondoa uhuru wa mawazo, ubunifu, na utashi.
Kwa hiyo viumbe vikiweza kutenda mabaya ndio vinakuwa vibunifu vyenye utashi?

Hii ni akili au matope?
Kwa maana hiyo, freewill siyo pambo, bali ni msingi mkuu unaotofautisha wanadamu na viumbe visivyo na akili (kama mawe au miti).
Nakwambia hivi, Huyo Mungu wako ana ugua ukichaa.
 
1. Nina maanisha Kulingana na Thread yangu TULICHAGUA MABAYA BADALA YA MEMA. halafu Tunamlaumu MUNGU kwa Uchaguzi wetu wenyewe

2. Umeuliza Kwamba Mungu kwanini Hakutuumba Bila Kasoro.. Binadamu Umekamilika huna Kasoro Yeyote ile, ungekuwa na Kasoro kama Angekuumba Bila Mikono, Huna Kichwa , Sikio Moja Lingine Halipo hapo Ungesema una Kasoro ila Binadamu umekamilika Huna Kasoro Hata Moja.

3. Unaposema Kwamba Biblia Imesema Anakujua Toka Tumboni mwa Mama Yako ni kweli anakujua na Anajua Hatma yako pia. Ndio maana nikamjibu member mmoja hapo Juu kwamba Uhuru wa kuchagua (Freewill) siyo kitu kinachoweza kugawanywa nusu. Huwezi kuwa na uhuru wa kuchagua kwenda "kulia" kama hakuna upande wa "kushoto".
• Uwezo wa kutenda mabaya ni matokeo ya uwepo wa uhuru wa kweli, na siyo kwamba Mungu alitengeneza mabaya kama bidhaa ya makusudi ili watu waijaribu,

Ni sawa na serikali inayompa raia uhuru wa kuendesha gari; uhuru huo unajumuisha uwezo wa kuendesha salama au kusababisha ajali. Serikali haitaki upate ajali, lakini haiwezi kukupa gari kisha ikufunge mikono.

4. Kuhusu SHETANI nitakujibu Hivi
Mungu hakumuumba "Shetani" akiwa mbaya; alimuumba kiumbe safi na cha kiwango cha juu (Malaika) ambacho pia kilikuwa na 'freewill' (uhuru wa kuchagua).•
Kwa nini asimuue mapema? kama Mungu angemwangamiza Shetani sekunde ile ile alipofanya uasi, maana yake kuanzia hapo viumbe vyote vingine (Malaika waliobaki na wanadamu) wangemtii Mungu kwa woga wa kifo na siyo kwa upendo wa dhati.

Na Kama Mungu angekuwa anafuta au kuua kila kiumbe kinachoanza tu kuwaza au kufanya vibaya, ulimwengu usingekuwa na uhuru tena. Ungekuwa ulimwengu wa vitisho, ambapo unalazimika kuwa mwema kwa sababu kuna "bunduki" imeelekezwa kichwani kwako.


5. Je! LAWAMA ni za Nani.

Ni kweli Shetani anashawishi na kupandikiza mawazo mabaya (kupitia mapepo au vishawishi), lakini siyo kulazimisha. Hakulazimshi uyatende mawazo mabaya Uliyonayo

• Shetani hana mamlaka ya kukushika mkono na kukufanyisha ubaya usiotaka. Yeye anatoa "ofa" au ushawishi tu, (kama Alivyomwambia YESU pale Alipokuwa a anamjaribu)lakini maamuzi ya mwisho yanabaki kwako.

• Ni sawa na muuzaji wa dawa za kulevya mtaani. Muuzaji ana makosa kwa kuleta dawa hizo, lakini kama wewe ukiamua kuzinunua na kuzitumia, huwezi kujiondoa kwenye lawama na kusema "Yeye ndiye aliyenishawishi." Lawama zinakuwa za pande zote mbili: Mshawishi ana makosa yake, na mtendaji ana makosa yake kwa kukubali ushawishi huo.
 
Kwanza hii AI unayotumia inakupa majibu yasiyo na mantiki.

Kazi yako ni kukopi na kupesti.

Kwa nini Mungu ampe Shetani uwezo wa kujaribu binadamu?

Ina maana huyo Mungu anapenda kuona binadamu wakijaribiwa?

Huyo Mungu kama anajua yote tangu mwanzo na hata milele, Sasa anatujaribu sisi binadamu ili agundue nini asichokijua?

Hivi huyo Mungu wenu anajielewa kweli?
 
Kwani Tulipokuwa tunasoma Shuleni Kinyume cha Ukweli ni nini , unaandika UONGO.. Ukiulizwa kinyume cha Cheupe ni nini Unajibu CHEUSI..

Sasa Kinyume cha WEMA NI NINI ? AU KINYUME CHA UBAYA NI NINI?
Labda Nikuulize Wewe uwenda Una Hekima Alitaka Aweke nini Ili kiwe mbadala wa MABAYA?

Kwa Sababu MABAYA yana Madhara na MEMA hayana MADHARA.. Usingechagua Kula Tunda Pale Bustani ya Edeni kama alivyofanya Adam na Eva. Leo hii USINGEKUWA UNALIA mtoto wako , mke, babu, bibi , mama au Baba Akifariki, Usingesema Maisha Magumu

Ila Kwa Vile Ulichagua MABAYA ndio maana Unateseka kwahiyo Upande Mmoja Ni Madhara na Upande Mwingine hauna Madhara
Kwa hiyo viumbe vikiweza kutenda mabaya ndio vinakuwa vibunifu vyenye utashi?

Hii ni akili au matope?
Kwanini umekaa upande Wa Mabaya Tu? Kwanini kwako matendo mabaya Ndio yametawala Kuliko Mema? Utashi hauwezi kukaa sehemu yenye Mabaya
Nakwambia hivi, Huyo Mungu wako ana ugua ukichaa.
Yeye si Binadamu hawezi Ugua wala Kuumwa .. Amekamilika Na Ni Mtakatifu.. Magonjwa au Ukichaa Huwapata viumbe
 
1. Mungu anajua kabisa kile kilicho moyoni mwa mwanadamu hata kabla hajazaliwa. Kwa hiyo, majaribu hayapo kwa ajili ya Mungu "kujifunza" kitu asichokijua.

2. Majaribu yanakuwepo ili wewe mwenyewe ujijue msimamo wako na ukomavu wako
Mungu hafurahii kuona binadamu wakiteseka au wakijaribiwa kwa maana ya ukatili, bali anaruhusu majaribu kama njia ya kuleta ukomavu wa kiadili na kiroho.

3.Mungu hafurahii kuona binadamu wakiteseka au wakijaribiwa kwa maana ya ukatili, bali anaruhusu majaribu kama njia ya kuleta ukomavu wa kiadili na kiroho.Dhahabu ili ing'ae na kuwa safi, lazima ipitishwe kwenye moto mkali ili kuondoa takataka zote. Bila moto, inabaki kuwa jiwe la kawaida tu

4.Kuna mkanganyiko kwamba kwa sababu Mungu anajua mwisho wetu, basi Yeye ndiye anayetulazimisha kufanya maamuzi tunayofanya. Hii siyo kweli.Ujuzi wa Mungu hauondoi uhuru wako: Mungu kujua kuwa kesho utachagua kufanya jambo baya, haimaanishi kwamba Yeye amekulazimisha kufanya ubaya huo. Yeye anasimama nje ya muda na anaona maamuzi yako yote ya hiari.
 
Huyo Mungu mnayedai kwamba anaweza yote, Angeweza kuumba Dunia ya binadamu wanaotambua wema tu. Pasipo kuyajua mabaya.

Huyo Mungu angeweza kuumba binadamu wenye ufahamu wa kutenda matendo mema tu, pasipo kuwa na ufahamu wa mabaya.

Na maisha yakawa safi tu!
Kwa Sababu MABAYA yana Madhara na MEMA hayana MADHARA.. Usingechagua Kula Tunda Pale Bustani ya Edeni kama alivyofanya Adam na Eva. Leo hii USINGEKUWA UNALIA mtoto wako , mke, babu, bibi , mama au Baba Akifariki, Usingesema Maisha Magumu
Kwani binadamu wote ndio tulichagua kula hilo tunda, Au ni huyo Adam na Eva tu?
Mungu gani mkamilifu anaumba Viumbe wenye uwezo wa kutenda mabaya?

Huo ni ukamilifu au ukichaa?
 
1. Mungu anajua kabisa kile kilicho moyoni mwa mwanadamu hata kabla hajazaliwa. Kwa hiyo, majaribu hayapo kwa ajili ya Mungu "kujifunza" kitu asichokijua.

2. Majaribu yanakuwepo ili wewe mwenyewe ujijue msimamo wako na ukomavu wako
Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu wanaojua misimamo yao na ukomavu wao bila majaribu?
Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu wenye ukomavu wa kimaadili na kiroho pasipo majaribu?

Au huyo Mungu anapenda kuwajaribu binadamu?

Na anafurahi kuona akitujaribu?
Jomba! Huyo Mungu wenu hajielewi kabisa.

Ana ukichaa na uwendawazimu.
 
Mbona Alifanya Hivyo Na Ulikuwa na Maisha Safi tu Bustani ya EDENI.. Nini kilikupata Mwanadamu ukaona maisha Haya Masafi huyataki TENA.. na Sasa Unamlaumu Yeye?

Kwani binadamu wote ndio tulichagua kula hilo tunda, Au ni huyo Adam na Eva tu?
Kwani Tanzania Ikikopa Pesa World Bank mbona Wajukuu zako wanalipa Deni hilo kwani Ni Wao waliokopa Au Wewe.. ?
Mungu gani mkamilifu anaumba Viumbe wenye uwezo wa kutenda mabaya?

Huo ni ukamilifu au ukichaa?
Hata Wewe ni Mkamilifu hakukuumba Kwamba Si Mkamilifu. Una Uwezo wa Kuchagua. Kila Saa nakuambia Jambo Hili..kuna Binadamu HAWATENDI mabaya Maisha Yao Yote. JE! HAO hawajaumbwa na MUNGU? Kuna Binadamu hajawahi Kutenda Uovu wowote ule maisha yake Yote na Nilikupa Hata Mifano.. Uwezo wanao ila Wamechagua Kutotenda UBAYA hata Ww unaweza na Hao Binadamu wengine pia Wanaweza Ila Wamechagua Kuwa WAOVU
 
Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu wanaojua misimamo yao na ukomavu wao bila majaribu?
Mbona Nishakujibu ila Moyo wako umekuwa Mgumu kuelewa
Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu wenye ukomavu wa kimaadili na kiroho pasipo majaribu?

Au huyo Mungu anapenda kuwajaribu binadamu?

Na anafurahi kuona akitujaribu?
Nimekuambia Wapo Binadamu hao na Hawatendi UOVU na ni wakomavu Pia na Nishakupa na Mfano mzuri kabisa AYUBU ni mmoja Wapo.. Au wewe unaona Dunia Nzima Ni Watu waovu?
Jomba! Huyo Mungu wenu hajielewi kabisa.
Wewe Mungu wako Ni YUPI! Tuone matendo Yake
 
Mbona Alifanya Hivyo Na Ulikuwa na Maisha Safi tu Bustani ya EDENI.. Nini kilikupata Mwanadamu ukaona maisha Haya Masafi huyataki TENA.. na Sasa Unamlaumu Yeye?
Nilikuwa ama walikuwa (wao) kina Adam na Eva?

Bustanini hakukuwa na watu wengine zaidi ya huyo Adamu na Eva.

Sasa iweje sisi tuhusishwe na makosa yao wakati hatukuwepo?

Sisi hatukuwepo na wala hatuhusiki na lolote.

Huyo Mungu asipakazie binadamu wote makosa ya watu wawili.

Anatakiwa ku-deal na huyo huyo Adamu sio kutupakazia makosa yao, yasio tuhusu!

Biashara za kupakazia Binadamu wote makosa ya watu wawili ni UPUMBAVU.

NA HUYO MUNGU NI MPUMBAVU!!!
Kwani Tanzania Ikikopa Pesa World Bank mbona Wajukuu zako wanalipa Deni hilo kwani Ni Wao waliokopa Au Wewe.. ?
Kama kila mtu huhukumiwa kutokana na matendo yake mwenyewe aliyoyatenda, iweje tupakaziwe makosa ambayo hatukutenda sisi?
Kwamba kuna Binadamu hajawahi kutukana, kuiba, kupigana, kusema uongo, kuzini, kutapeli?

Yote haya ni mabaya na kila mtu ashafanya, labda wale watoto wadogo wasio na ufahamu.

Halafu wewe hapa unasema kuna Binadamu hajawahi kutenda mabaya.

Acha kudanganya wewe!
 
Mbona Nishakujibu ila Moyo wako umekuwa Mgumu kuelewa

Nimekuambia Wapo Binadamu hao na Hawatendi UOVU na ni wakomavu Pia na Nishakupa na Mfano mzuri kabisa AYUBU ni mmoja Wapo.. Au wewe unaona Dunia Nzima Ni Watu waovu?
Huyo Mungu alishindwaje kufanya Binadamu wote wawe wakomavu kama huyo Ayubu?

Au alitaka Binadamu wengine wafanye mabaya?
Wewe Mungu wako Ni YUPI! Tuone matendo Yake
Hakuna Mungu.

Mungu hayupo.

Huyo Mungu mmejitungia tu wala hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mnaleta hekaya na hadithi za vitabuni tu.

Hamna tofauti na mtu anayeleta hadithi za Abunuwasi, Esopo na Kalume-Kenge.
 
Nilikuwa ama walikuwa (wao) kina Adam na Eva?

Bustanini hakukuwa na watu wengine zaidi ya huyo Adamu na Eva.

Sasa iweje sisi tuhusishwe na makosa yao wakati hatukuwepo?
Nimekupa Mfano wa Kibinadamu tu kwamba Ikiwa Tanzania inaweza kukopa Fedha World bank, ila wewe🫵 pamoja na Wajukuu zako ndio mtazilipa ,Je! Kwanini Unazilipa Kupitia kodi zako wakati waliokopa ni Kina Nyerere na Mkapa Huko zamani..
Adam na Eva ndio wazazi wa Kwanza walitenda Kosa Kila Binadamu analilipa Maana Kama Waliambiwa Watakufa Sidhani Wewe KUJITOA kwako kutakuepusha Na KUFA. Adhabu yao imekuwa yako Kwahiyo ipokee hata kama Unakana hukutenda Kosa hilo.. Unaposema HAUUHUSIKI NA LOLOTE.. JE! Hutakufa? Maana Moja Wapo ya Laana ilikuwa UTAKUFA , wewe hutakufa?

Kama kila mtu huhukumiwa kutokana na matendo yake mwenyewe aliyoyatenda, iweje tupakaziwe makosa ambayo hatukutenda sisi?
Kwani Hukumu ya Mwisho Unadhani utahukumiwa kwa Sababu adamu alikula Tunda!? Yeye aliambiwa atakufa Na Kama Asingezaa Watoto Na EVA wakasema tusizas basi Usingekuwepo..

Warumi 5:12,
"Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia duniani, na kwa dhambi hiyo kifo; na hivyo kifo kikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi."

Kifo na mateso vimetufikia wote si kwa sababu Adamu alikosea, bali kwa sababu sisi sote tuliozaliwa tumerithi ule udhaifu na "wote tumefanya dhambi" wenyewe. Adamu alikuwa kama chemchemi ya maji; alipoweka sumu kwenye chemchemi (kwa kufanya dhambi), maji yote yanayotoka pale (sisi wanadamu) yanatoka yakiwa na chembechembe za ile sumu.
 
Huyo Mungu alishindwaje kufanya Binadamu wote wawe wakomavu kama huyo Ayubu?

Au alitaka Binadamu wengine wafanye mabaya?
Kwani mbona Sasa Hivi Upo na Mimi hapa Tunajadiliana mambo haya. Je kwanini Hujaenda Kutenda UOVU wowote ule?! Ungekuwa labda unafanya mipango ya Wizi, Ulevi, Uzinzi na uasherati n.k

Ayubu ni kama Wewe na Mimi aliamua Kuwa Mkomavu .. Binadamu wote Tumeumbwa Kama AYUBU
Hakuna Mungu.

Mungu hayupo.

Huyo Mungu mmejitungia tu wala hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mnaleta hekaya na hadithi za vitabuni tu.

Hamna tofauti na mtu anayeleta hadithi za Abunuwasi, Esopo na Kalume-Kenge.
1. Basi Kama Mungu Hayupo Wewe unaamini UMETOKA WAPI au Milima, Maji, Damu inayotembea Mwilini mwako.. Hivyo Vyote Chanzo chake ni Nini?

2. Mimi ninaweza Thibitisha kulingana na Maandiko mengine hata hayatoki kwenye Biblia bali Vyanzo vingine nje ya Biblia na Matendo yake yameonekana hata kwa Watu wasio amini kama Wewe
 
Sijadanganya WAPO ndio.. Na Nishakupa Mifano kibao ya Kibiblia YESU ni Mmoja Wapo kama AYUBU humtaki.

Lakini Wewe Huwezi Kukubali Maana Neno MABAYA limekaa Sana Kichwani Kuliko WEMA. Wema Wapo na WANAISHI hapa Duniani na HAWATENdi Mabaya

Ila Kama 🫵 unatenda Mabaya YESU alisema Kwamba Njooni Kwangu Nyinyi nyote mnaoelemewa na Mizigo nami Nitawapumzisha. Akiwa na Maana Mizigo(dhambi) Tubu mkaribie Yeye nawe utakuwa Mwema na Utaoata Nafasi ya Kurithi Uzima wa Milele..
 
Sijatoka popote.

Nimezaliwa kutoka kwa wazazi wangu. Hapahapa ulimwenguni.

Milima, maji na vitu vyote except man-made things havijatoka mahali, havijaumbwa na havina chanzo. Vimekuwepo milele na wala havihitaji chanzo.

Kama vitu vinahitaji chanzo hata huyo Mungu anahitaji chanzo. Kama huyo Mungu haitaji chanzo, hata Ulimwengu hauhitaji chanzo.

Hakuna Mungu.

Mungu hayupo.
 
Mifano ya kibiblia ni ya imani yako tu. Hata waislamu wana mifano yao ya Quran. Hata wahindu wana mifano yao ya kitabu chao cha The Vedas, Hata wayahudi wana mifano yao ya kitabu chao cha Torah.

Kwa hiyo wewe usidhani kwamba mifano yako ya Biblia ya kina AYUBU ndio mifano bora ya kweli, Wakati ni mifano ya imani yako tu. Uliyoaminishwa tu. Hata mtu wa imani nyingine ana mifano ya kwenye kitabu chake.
 
Unatoa mifano ya Biblia kwa vile wewe ndio unaiamini na unamuamini huyo Yesu wa Biblia.

Hata muislamu anaweza kutoa mifano ya Quran, kusema Mungu wake Allah yupo.

Mifano ya Biblia ni kulingana na imani yako wala sio uthibitisho kwa watu wote. Kwa sababu sio watu wote wana amini hiyo Biblia.

Kama ambavyo wewe ukipewa mifano ya Quran utaikataa. kwa vile huamini Quran. Vivyo hivyo mifano ya Biblia ni BATILI kwa wasio amini Biblia.

Kwa hiyo huwezi kutumia Biblia yako kuhalalisha mawazo yako ya imani yako kwa sababu hata watu wengine pia wanaweza kutumia vitabu vyao vya kiiimani kama Qur'an, Torah na Tripitaka kuwahalalisha mawazo yao.

Na sisi hatutaki hadithi za vitabuni zinazo pingana maelezo ya kiimani. Tunataka ukweli wenye logical consistency.

Sasa wewe unaleta hadithi zako za Biblia kama mifano, kitu ambacho hata muislamu anaweza kuleta hadithi zake za Quran na kusema ndio mifano.

MIFANO YAKO YA BIBLIA NI KWAKO TU. NA SI KWAMBA NDIO MIFANO YA UKWELI KWA WATU WOTE.
 
Kusema kwamba Adamu na Eva ndio wazazi wa kwanza ni kufosi tu hadithi zako za Biblia ulizo aminishwa. Kulingana na imani yako tu!

Hata Wahindu wanaamini kwamba Svayambhuva Muna na  sharatupa ndio wazazi wa kwanza kulingana na imani yao.

Kwa hiyo imani yako ya kuamini Adamu na Eva ndio wazazi wa kwanza, ni imani yako tu. Uliyoaminishwa. Si kweli wala haikubaliki na kuaminiwa na watu wote.

Kwa sababu kila mtu ana imani yake anayoiamini.

Na imani yako sio bora sana yenye ukweli kuliko imani za wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…