Binadamu tunaishi ili iweje? Au tupo duniani kufanya nini? Why Do We Live?

Binadamu tunaishi ili iweje? Au tupo duniani kufanya nini? Why Do We Live?

2] Ivi Mkuu, kwanini lengo la kuishi liwe determined na mtu husika?

Kwa sababu mtu husika ana uwezo wake wa kuwaza, kufikiri na kuchambua mambo mwenyewe kutegemea (mis)information alizonazo na mazingira yaliyomzunguka.

Kumuachia jukumu hili mtu mwingine ina maana ame-outsource ubongo wake. Bodly, hana tofauti na robot.

Wewe unaona lengo la mtu kuishi liwe determined na nani? Na kwa nini?

Hivi kila mtu awe na lengo lake (la kuishi) na atekeleze lengo hilo, wewe unahisi nini kitatokea? Na jee matokeo yake ni nini?

Ni ngumu kujua nini kitatokea. A happy world? I don't know. Inategemea na malengo ya watu binafsi ambayo siyajui.

3] Do you believe on existance of God?

No, I don't.
 
Mkuu Nilisikia mahala kuwa waislamu wanaamini kila binadamu aliyekuja duniani aliomba kuja hapa duniani ni kweli?!

Hahahahahaaa!
Iyo hadithi ya aolela ulela hata mimi nilishaiskia! Tena walifika mbali na kusema mtu anaulizwa kabisa 'afeje' 'akifa aende peponi au motoni' nk nk!

Hakuna ukweli wowote hapo!
 
Allah(s.w) amesema katika Qur'an: walaktal'jinna walyinnsa ilal yaabuduuna, maana yake: sikuwaumba majini na wanadamu, ila waniabudu. Hilo ndiyo lengo kuu la kuumbwa kwa mwanaadamu.

Oh boy.. there we go!
 
is well and good ,the world will tell on its own way and time.you will never ever see and read the real semantic in my statements by been arrogant through predicting the unknown.Attacking a person individually by insults is lack of potential knowledge stability and outputting ignorant inborn character you where hiding.I thank my GOD that the rail is straight and the praise towards is infinity.keep dreaming

Kuandika kizungu sio proof ya kuwa unaakili nyingi! Sipati picha porojo unalitoa kubishana na watu hapa ungetolea ufafanuzi wa zile hoja zako!
Shame on you! Hah!
 
Kuandika kizungu sio proof ya kuwa unaakili nyingi! Sipati picha porojo unalitoa kubishana na watu hapa ungetolea ufafanuzi wa zile hoja zako!
Shame on you! Hah!

i stand to defend my being
 
Toa hayo maandiko kwa kuandika hizo aya zake hapa si wote wanajua kusoma au wana quran. Andika hizo aya hapa jf kila mtu azione mjadala uendelee.

Nimeshamuekea tafsiri zake ni yeye tu wakuproof huo mkanganyiko, check post #97 !
 
Kwa sababu mtu husika ana uwezo wake wa kuwaza, kufikiri na kuchambua mambo mwenyewe kutegemea (mis)information alizonazo na mazingira yaliyomzunguka.

Kumuachia jukumu hili mtu mwingine ina maana ame-outsource ubongo wake. Bodly, hana tofauti na robot.

Wewe unaona lengo la mtu kuishi liwe determined na nani? Na kwa nini?
Mimi ni mdau wa kuamini Mungu!
Hivyo alietuumba ndie anaepaswa kudetermine lengo la kutumba kwake!
Hiyo itasimama kama general rule, exceptions zitakuwepo ktk mambo yaliyoruhusiwa kuchagua!

Nadhani hata wewe hauishi kama utakavyo! You have to abide with some rules whether state rules, customary, or even moral rules! = hauwezi kutekeleza interests zako zote bila ya kuafectiwa whether by relious rules or any other rules!
Sema wewe kwa vile umeamua kutofata lolote kuhusiana na dini ndio unajiuna uko huru sana kitu ambacho sio kweli!
Ni ngumu kujua nini kitatokea. A happy world? I don't know. Inategemea na malengo ya watu binafsi ambayo siyajui.
nadhani hapa ndio unathibitisha kwamba haiwezekani mtu kufanya atakalo! Na akifanya vyombo vya dola vitamdhibiti!

Mwisho wa siku tunapata jibu kuwa, vyovyote utakavyoishi ni lazima uendane na sheria na sio kujiamulia mwenyewe! Hii inamaana kitendo cha kuchagua uishi utakavyo kimeekewa mipaka!

No, I don't.
Hahahahahahaaa! Nilistukia hili kutokana na maelezo yako!
 
Huyo aliyetupangia kufa na kutuahidi kulata mito ya asali mbinguni ametukataza tusitamani kufa wala tusijiuwe kwa mikono yetu
bakar faki, ni sawa na umwambie mwanao akisoma kwa bidii na akifaulu utamnunulia zawadi ya gari, lakini haruhusiwi kuitamani hio gari! Lazima umchanganye aisee.

Sasa inaleta maana kweli kama tusitamani kufa wakati tujifa ndio tunaenda kuzuri zaidi?
 
Mimi ni mdau wa kuamini Mungu!
Hivyo alietuumba ndie anaepaswa kudetermine lengo la kutumba kwake!
Hiyo itasimama kama general rule, exceptions zitakuwepo ktk mambo yaliyoruhusiwa kuchagua!

Clearly hapa tunatofautiana kwa sababu mimi siamini mungu.

Pia unaongelea kuhusu intelligent design na uhuru wa kuchagua, vitu ambavyo haviwezi kumix. This is a debate for another time.

Nadhani hata wewe hauishi kama utakavyo!

Refer my response. Uhuru wa mtu kuishi kama atakavyo unategemea uwezo wake (iwe kifedha, akili, etc) na mazingira yanayomzunguka.

Kwa maana hiyo, mtu anaweza asiishi atakavyo. Lakini mtu anaweza kutambua limitations zilizopo na kuishi atakavyo katika mipaka ya hizo limitations. Au mtu anaweza kuamua kujiua kwa sababu hana uwezo au mazingira hayamruhusu kuishi atakavyo (haoni lengo na sababu ya kuendelea kuishi).

You have to abide with some rules whether state rules, customary, or even moral rules! = hauwezi kutekeleza interests zako zote bila ya kuafectiwa whether by relious rules or any other rules!

I prefer the use of "common sense" to rules.

Kwa mfano, naelewa nikikojoa mlangoni ni vibaya kwa sababu mlango huo ni njia na mkojo ni uchafu. Hivyo kufanya hivo ni vibaya. It's common sense, haihitaji mpaka mtu aandike "usikojoe hapa". Lakini pia inaweza kutokea mtu amebanwa kupita uwezo wake na akaamua kukojoa mlangoni. Akisafisha right after the act sioni kosa kwani it is explainable and excusable. The body failed him, but lawyer angesema angekojoa kabla hajatoka nyumbani 🙂

Hivyo common sense prevails and that's what I prefer kuliko kusema rules. Plus rules change. It was illegal to do certain things in the past, but with time, those same things are now legal.

Hivyo utaona laws/rules hazina consistency. Sadly common sense is not common.

Sema wewe kwa vile umeamua kutofata lolote kuhusiana na dini ndio unajiuna uko huru sana kitu ambacho sio kweli!

This is debatable. Mfano kwa trend ya majibu yaliyotolewa hapa inaonekana lengo la maisha ni kuserve yale mungu aliyosema. Wengine wanasema kuishi vile mungu atakavyo.

Kama mimi siamini huyo mungu nina uhuru wa kufanya mengine ambayo mungu hajasema. Vilevile nina uhuru wa kuishi kwa muono wangu mimi mwenyewe bila kanuni au sheria za mungu.

nadhani hapa ndio unathibitisha kwamba haiwezekani mtu kufanya atakalo! Na akifanya vyombo vya dola vitamdhibiti!

Kwa ulichosema hapo inaonyesha kwamba mtu kufanya kile atakacho, ni kufanya vitu ambavyo ni "morally" wrong.

Hiyo ni kusema kusingekuepo na mungu watu wangetenda mabaya. Kuonyesha kwamba bila mungu watu hawana common sense ya kutambua "zuri" na "baya" na kuishi pamoja bila kufanyiana "mabaya".

Note: Natumia "" kwenye suala la morality kwa sababu morality yenyewe ni debatable. IMO, moral absolutism is flawed. Sema wewe kwa kua unaamini mungu na kanuni zake unaona morality ni absolute kwa sababu imeandikwa katika kitabu kipi sawa na kipi si sawa.

Mwisho wa siku tunapata jibu kuwa, vyovyote utakavyoishi ni lazima uendane na sheria na sio kujiamulia mwenyewe! Hii inamaana kitendo cha kuchagua uishi utakavyo kimeekewa mipaka!

Nakubaliana na wewe kuhusu mipaka, refer jibu langu juu kuhusu kuishi nitakavyo. Mipaka hii inategemea uwezo na mazingira.

Pia mtu ana uwezo wa kujiamuliwa mwenyewe keeping in mind anajua consequences za kile anachoamua regardless ya rules kuwepo.

Hahahahahahaaa! Nilistukia hili kutokana na maelezo yako!

:A S-devil4:
 
Clearly hapa tunatofautiana kwa sababu mimi siamini mungu.
😛oa:
Pia unaongelea kuhusu intelligent design na uhuru wa kuchagua, vitu ambavyo haviwezi kumix. This is a debate for another time.
😛oa:
Refer my response. Uhuru wa mtu kuishi kama atakavyo unategemea uwezo wake (iwe kifedha, akili, etc) na mazingira yanayomzunguka.

Kwa maana hiyo, mtu anaweza asiishi atakavyo. Lakini mtu anaweza kutambua limitations zilizopo na kuishi atakavyo katika mipaka ya hizo limitations. Au mtu anaweza kuamua kujiua kwa sababu hana uwezo au mazingira hayamruhusu kuishi atakavyo (haoni lengo na sababu ya kuendelea kuishi).
Mkuu watu wanatofautiana kufikiri na nikubailiene na wewe kwamba uhuru wa mtu unategemea fedha akili etc! Hapo kwenye kutambua limitation zilizowekwa kwenye uhuru wa kuchagua nadhani umegeneralize sana coz (kuwa na) fedha na akili sometimes ndio source ya kukiuka hizo limitation!
I prefer the use of "common sense" to rules.

Kwa mfano, naelewa nikikojoa mlangoni ni vibaya kwa sababu mlango huo ni njia na mkojo ni uchafu. Hivyo kufanya hivo ni vibaya. It's common sense, haihitaji mpaka mtu aandike "usikojoe hapa". Lakini pia inaweza kutokea mtu amebanwa kupita uwezo wake na akaamua kukojoa mlangoni. Akisafisha right after the act sioni kosa kwani it is explainable and excusable. The body failed him, but lawyer angesema angekojoa kabla hajatoka nyumbani 🙂
Mkuu kusudio langu hapo ni kuwa, sometimes mtu mwenyeye anaingia conflict na interest zake pale anapokumbuka morality rule! Kwani mkuu haukumbuki kutaka kufanya kitu na ukajisuta au ukafeel sorry kwa ulichokifanya?
Hivyo common sense prevails and that's what I prefer kuliko kusema rules. Plus rules change. It was illegal to do certain things in the past, but with time, those same things are now legal.

Hivyo utaona laws/rules hazina consistency. Sadly common sense is not common.
😛oa: na ukumbuke hata akili, kipato na mazingira havina consistency, vyote viko subject to change!
This is debatable. Mfano kwa trend ya majibu yaliyotolewa hapa inaonekana lengo la maisha ni kuserve yale mungu aliyosema. Wengine wanasema kuishi vile mungu atakavyo.
😛oa: ingawa wengi (tunaoamini) tumekremu!
Kama mimi siamini huyo mungu nina uhuru wa kufanya mengine ambayo mungu hajasema. Vilevile nina uhuru wa kuishi kwa muono wangu mimi mwenyewe bila kanuni au sheria za mungu.
Hapo siwezi kukupinga!
What i believe is not what you believe! The accuracy of what we believe is nothing rather than politics!!! Yes! Ni si siasa tu! Coz wewe unamaelezo, hoja na maswali ambayo sitoweza kukujibu na mimi ninavitu ambavyo hautaweza kunijibu! Kama sio siasa ni nini hiko?
Kwa ulichosema hapo inaonyesha kwamba mtu kufanya kile atakacho, ni kufanya vitu ambavyo ni "morally" wrong.
Yap! But sio perfect! Ukumbuke mwanadamu ni mchoyo na ni kiumbe mpiganaji kiasili!
Hiyo ni kusema kusingekuepo na mungu watu wangetenda mabaya. Kuonyesha kwamba bila mungu watu hawana common sense ya kutambua "zuri" na "baya" na kuishi pamoja bila kufanyiana "mabaya".
No!
Note: Natumia "" kwenye suala la morality kwa sababu morality yenyewe ni debatable. IMO, moral absolutism is flawed. Sema wewe kwa kua unaamini mungu na kanuni zake unaona morality ni absolute kwa sababu imeandikwa katika kitabu kipi sawa na kipi si sawa.
Mkuu mimi sijakremu!
natambua religious moral, universal na hata subjective moral! Na zaidi nakubali moral is subjective rather than religion and universe! Yap! What is moral to me is not moral to you!

Nakubaliana na wewe kuhusu mipaka, refer jibu langu juu kuhusu kuishi nitakavyo. Mipaka hii inategemea uwezo na mazingira.

Pia mtu ana uwezo wa kujiamuliwa mwenyewe keeping in mind anajua consequences za kile anachoamua regardless ya rules kuwepo.
😛oa:
:A S-devil4:
 
Tangu mwanzo(Kabla ya anguko la Adamu na Hawa) Mungu alikusudia kuishi na Wanadamu duniani milele!,kifo na uharibifu wa kila namna vilikuja baada ya anguko.Tangu hapo dunia ikawa haisapoti umilele tena,hata hivyo Mungu wetu kwa wingi wa rehema na fadhili zake alimtoa kwetu mwanae wa pekee(Yesu Kristo) ili kila atakayemwamini awe na Tumaini la uzima wa milele moyoni mwake ambao utatimilizwa atakapokuja mara ya pili kuwachukua wamwaninio ambapo watavaa miili isiyoharibika(kama ya malaika) na kuishi pamoja nae mbinguni(kwa sababu dunia imekwisha haribiwa hivyo haisapoti umilele,ingawa ukweli ni kwamba,tangu mwanzo Mungu alikusudia kuishi na wanadamu duniani milele na sio mbinguni!)
 
maisha ni vita ya kiroho sisi ni wanajeshi kuna waasi na wazalendo tafuta ushindi BE A GREAT THINKER Cc juve2012

Baada ya tukio la uasi wa malaika mbinguni,uasi wa binadamu na malaika pale Eden,uasi wa malaika mara ya pili pale Hermon,uasi wa binadamu pale babylon,kifo cha Yesu pale Golgota,tuko katika plan B ambayo tukiiweza tutarudi Plan A in future times.Lakini ifahamike kwamba wokovu hauji bila ule ukengeufu kuja kwanza.Mungu anachuja viumbe wake.Halel ameachwa purposely,kuonyesha kama uasi dhidi ya Mungu ni jambo jema au baya.Na sasa umefika wakati wake wa kuachiwa.Anaivuruga sana dunia na ataendelea kuivuruga sana.This is satanic golden age,the age of aquaria,the age of satanic civilization,lakini kwa sababu uasi dhidi ya Mungu ni uovu,na mwisho wa uovu ni maangamizi,civilization hii imekuja na uharibifu.Mwisho wa uasi hauko mbali.Hii scenario ndio inayofanya watu washindwe kujua kwa nini wapo duniani.Ni kwa sababu hawajui kwa nini dunia iko hivi.Nawaomba waumize vichwa vyao kujua jibu la hilo swali la mwisho,kwa nini dunia iko hivi?imetoka wapi,then watajua ilipaswa kuwaje,na hivyo watajua wao ni nani na wana sehemu gani katika urithi huu,but look around you,billions of people around the world,hivi huyu aliyeumba wote hawa kawaumba ili walete chaos zote hizi?kwa nini hatufurahii maisha haya ya chaos?je,tuko peke yetu duniani?tusije tukawa tunafanya makosa kwa kudhani tuko peke yetu na hivyo kujipachika liabilities kwa kila kiendeleacho duniani na kumbe kukawa na viumbe wengine wenye influence kubwa katika hali iliyopo,wanaotupeleka wanakotaka wao,wanaotuondoa katika asili yetu na hivyo kuharibu uhusiano wetu na chanzo chetu.Thanks to God there is always whistleblowers.Historia ni whistleblower wetu.Mto wa maji ukishachafuka,then ukitaka maji masafi kwenye mto huo huo inabidi uufuatilie ulikoanzia,pale kwenye chemchemi yake,utapata maji safi,na pia ukikuta maji ya mto ni machafu kabisa,ukaufuatilia hadi unapoanzia na kukuta chemchemi inatoa maji machafu,ujue huo ni mto wa maji machafu,usiseme umechafuka,sema mto wa maji machafu,na kama unatafuta maji masafi,tafuta mto mwingine.Lakini kile unachoita wewe uchafu,mwingine atasema ni aina ya maji,akaipenda.Huenda mto huo unatoka katika ufa wenye volcanic activities,maji yamejaa sumu tangu mwanzo,ukajua ukauacha,mtu mwingine akapenda rangi ya maji,ukamtahadharisha,akakupuuza,akavutiwa na rangi,akanywa,tukamzika,sie tukaendelea kutafuta mto uliochafuliwa,na sio mto mchafu,wengine njiani wakaanza kupiga mayowe,jamani eeh,hii safari haiishi,tumechoka bwana,mito yote michafu tu,hakuna maana ya safari yetu(maisha),bora tungebaki misri kwa farao,tuendelee kula kitimoto,huku tukicheza ngoma ya zomari na nyoka!na mayowe haya ni mengi kweli siku hizi,ndipo hapo Halel anapataka ili apoteze kabisa mioyo hii rahisi,na ndipo hapo Elohi anapataka,aithibitishe imani ya wanaostahili kuendelea na safari,hao wanastahili kuishi.ni ukweli mchungu kumeza but ni mchungu kwa sababu katika ages zote hizi,tumeishi kwa kudanganywa,uongo ule wa Eden,tena siku hizi umepamba moto kweli, kwamba utakuwa kama Mungu,ukijua mema na mabaya,ila hakusema consequences za kujua mabaya.Sasa tukiwa tunalalamika kwa kuujua ubaya, amerudi tena,full of lies,unaweza kumwona hata humu Jf,na doctrine yake ile ile,akiwaambia mtakuwa kama Mungu..binadamu ni mungu,hakuna mungu zaidi ya binadamu mwenyewe,hakuna aliye juu yake,fanyeni meditation,mjitambue,msikie inner voice,mkutane na ascended (descended) masters,wawaongoze kufikia uungu wenu,mfikie viwango vya juu vya ufahamu etc etc...haya ni mafundisho ya kichawi yanayoenea toka enzi za babylon hadi leo..chaldean witchcraft,brought down to the world by the watchers,angelic beings called grigori,the fallen angels.Halel himself want to be like God,he is so obssesed with that,to the extent of talking a lot about it,spreading that lie everywhere he goes.beware,it's the age of aquarius,new age,age of deception,age of destruction.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaa haaaa
Yaaani Imebidi nicheke tu
Hajui mambo ya Mungu hayachunguziki mkuu

Umeona eee bana kuna siku washkaji walikuwa na mjadala kuhusu Mungu alianzaje? Basi chalii mmoja akajibu Mungu alitokana na power, mwingne akaulza hiyo pawa iliundwa na nani? Jibu likatoka ni nature, swal jngne likaulzwa hiyo nature iliundwa nani? Jamaa mmoja akawakata maini kwa kuwajibu vitu vyote viliumbwa na Mungu, na Mungu alitokeaga ghafla. Mjadala ukawa kama vile umekufa, lakini bila kutegemea chalii mmoja tena akaulza kabla Mungu hajatokea ghafla kulikuwepo na nini? Jibu likawa kulikuwa na utupu. Swali tena Utupu uliundwa na nani? Mie nikaona hii topic ni infinity bora nisepe tu make mwngne anaweza kujbu utupu ulitokea kama upepo naye ataulizwa upepo uliumbwa na nani? Akjibu jiwe atabandkwa tena swal jiwe liliumbwa na nani? Maswali yatakuwa endelevu bila mwisho. Kwa hiyo jibu zuri ni lile la kwenye bibilia kwamba ''Mungu alikuwepo toka awali hakuanza na wala hana mwisho''
 
Tatizo watu wanamfikiria Mungu kibinadamu.wanamcontain katika maumbile wakati yeye si kiumbe.we only know kwamba viumbe ndivyo vyenye mwanzo na mwisho,we don't know everything kuhusu Mungu,yeye si kiumbe,ukitaka kujifunza kuhusu yeye,you have to think outside the box,prepare yourself for the unknown,mambo ya ajabu kwako,na bado brain yako itakuwa na limitation katika tafsiri.
 
Binadamu wa ajabu sana maswali mgumu ya kutafuta majibu yakiwashinda wanakimbilia kusema mambo ya mungu hayo lakini tukumbuke hata gono lilikuwa halina dawa watu wakatafuta majibu wakayapata.sasa wacha kusingizia mungu chekechecha bongo.
 
Tatizo watu wanamfikiria Mungu kibinadamu.wanamcontain katika maumbile wakati yeye si kiumbe.we only know kwamba viumbe ndivyo vyenye mwanzo na mwisho,we don't know everything kuhusu Mungu,yeye si kiumbe,ukitaka kujifunza kuhusu yeye,you have to think outside the box,prepare yourself for the unknown,mambo ya ajabu kwako,na bado brain yako itakuwa na limitation katika tafsiri.

peke yako jf nzima ndo tuna the same idea and which is a real key i appreciate Great thinkers like you ,nakumbuka when i was young niliandika kitabu changu kinaitwa TEARS OF WISE HUMANITY ,watu wanapotea reli,watu hawajitambui,hawaelewi tupo kwenye battle ,wanasahau asili,hawafikiri zaidi ,dunia ni uwanja wa mapambano tena very serious ,watu wanadhani hell ni jambo la kufikirika hawajui soma hata ishara juve2012
 
Last edited by a moderator:
Ni Mungu pekee anayejua madhumuni ya kutuumba sisi binadamu na kutuleta duniani na kutufanya tuishi kwa kipindi fulani.

Hata hivyo ninachojua Mungu ametuwekea 'speed governer' katika ubongo wetu, ambapo ametuwekea 'limit' ya upeo wa kujua mambo ya Mungu.

Mfano utacrack kichwa chako kutaka kujua inakuwaje Mungu awe Alpha na Omega hutapata majibu.

Vile vile ukitafakari wakati wa uumbaji wake wa dunia na vyote vilivyomo duniani pamoja na sayari zote zinazozunguuka dunia, 'material' ya kuumbia sayari hizi, hutapata majibu, na badala yake utaumiza kichwa tu.

Ukitaka kuthibitisha ukuu wa Mungu ni kuwa hata maScientists, ambao wamekuwa 'wagumu' wa kukiri uwepo wa Mungu, lakini hata wao wanakiri kuwa dunia na vyote vilivyomo duniani na sayari zinazoizunguka, havikuja 'vyenyewe' tu, bali lazima kuna aliyeviumba, yaani CREATOR!!

Kwa hiyo sisi bibadamu tunapowaza maajabu ya Mungu ya uumbaji, tunaishia kutojua zaidi kutokana na Mungu kutuwekea 'speed governer' kwenye bongo zetu na hatimaye tunaishia tu kujisemea kimoyo moyo kuwa, mwacheni Mungu aitwe Mungu!!!!!!!!!!!

Mkuu hapo kwenye material,nikushangaze zaidi,scientific researchers wamegundua kuwa ni material moja tu iliyoumba vitu tofauti vilivyojaa kwenye universe,nayo ni energy.wamegundua ndani ya kila kitu kuna energy,iliyo katika mfumo wa mtetemo(vibrations) na vibration hizo zinajipanga kihisabati ili kuipa mada aina yake,ukichunguza jiwe,maji,mbao,mchanga,etc kila kitu kinakuwa na mtetemo wake tofauti na vya aina nyingine.na hata ukichukua mawe ya aina tofauti,utakuta yana pattern tofauti katika vibration zake,meaning kwamba kinachosababisha mtetemo huo ndio kinaamua hatma ya mada inayotokana na mtetemo husika.Hisabati inayotumika kuzalisha vibration hizo remains a mystery!what it means ni kwamba something so big and complex is causing these vibrations.there is one energy which disintergrated to cause all of what we have today and it is still playing it's mathematical music to hold all creation together and according to the command which give them their type.wakagundua pia kwamba wakati wa big bang jinsi mlipuko ulivyotokea,kiwango cha kutanuka ulimwengu kilikuwa na mpangilio maalum ulioleta initial conditions ambazo ni favourable kwa existence ya ulimwengu na yaliyomo.kama kiwango cha kutanuka ulimwengu sekunde moja tu baada ya mlipuko ule kingechelewa just for one part among milions in a millions,ulimwengu ungecollapse into a fireball.Gravity force ingepungua just for one part in ten thousands,ulimwengu usingeweza kuwa na mazingira yanayoruhusu uhai.kihisabati,kuna karibu 50 quantities and constants zilizojitokeza wakati wa big bang ambazo ilikuwa lazima ziwe balanced kama zilivyokuwa ili ulimwengu uruhusu uhai.na sio tu kwamba ilikuwa lazima kubalance kila quantity tu,bali pia uhusiano wa quantity moja na nyingine ilikuwa lazima uwe balanced.So improbability is multiplied by improbability by improbability untill our minds are reeling in incomprehensible numbers.Hakuna ajuae ni kwa nini constants na quantities hizo zimebeba value zile zilizo nazo.Mwanasayansi Fred Hoyle anasema,"a common sense interpretation of the facts suggests that a superintellect has monkeyed with physics."Robert Jastrow,mkuu wa NASA's Gordad institute for space studies,anasema "this is the most powerful evidence for the existence of God ever to come out of science".Hizi facts wanazogundua wanasayansi sasa zinaprove kwamba ulimwengu haukuja by chance,bali by design.big bang inaprove kwamba ulimwengu ulikuwa na mwanzo,sasa kama kuna kitu kimeanzisha space and time,then kitu hicho lazima kiwe timeless,changeless,uncaused,immaterial being of unimaginable power.Na pia lazima kiwe personal.Lazima kiwe personal na akili za maamuzi,inawezekana vipi source ambayo ni timeless ikasababisha jambo bila kuwa na akili ya maamuzi?kama mwanzo wa ulimwengu ni jambo ambalo limejitokea tu kimazingira,how come mazingira hayo yabadilike ghafla tu at a point na kuumbika kwa mpangilio wa hali ya juu hivi wakati yapo enzi na enzi?kama cause ipo enzi na enzi basi na effect ingekuwepo enzi na enzi, kitu ambacho si sahihi kwa facts zilizopo.njia pekee ya cause kuwepo timelessly na effect kuanza kwa wakati na design ya kiwango hiki ni hiyo cause kuwa personal agent mwenye akili yenye maamuzi yenye kuleta effect at any point in time without any prior dertemining conditions.kwa hiyo ulimwengu si tu kwamba una mwanzo bali pia mwanzo huo ni personal Creator.Kuna mtu mmoja anaitwa kahtaan humu aliwahi kusema,upungufu wa elimu ndio unawafanya watu waamini hakuna Mungu.Kahtaan una maudhi mengi lakini kwa hili,nitakuheshimu sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom