Bingwa wa 'software' anahitajika

Bingwa wa 'software' anahitajika

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Habari wakuu?

Nahitaji mtu anayeweza kutengeneza software ya 'animation', yaani ya kutengeneza 'video' za katuni.

Hiyo 'programme' iwe na angalau sifa hizi:-​
  • Iwe ni rahisi kutumia​
  • Iweze kutumia lugha mbili kiingereza/kiswahili​
  • Iweze kutengeneza 'character' wa aina yoyote​
  • 'Back ground' iwe inabadilishika, iendane na mtumiaji​
  • Isiwe na mavitu mengi ya kuchanganya​
  • Pia, uwe tayari kutoa mafunzo kwa watumiaji​
Kwa wale watundu wa mambo ya 'software' kazi kwenu; dau langu ni milioni mbili, iko mfuko wa shati.

Tupige kazi.​
 
Ya video za 2D au 3D? Hii system ni kubwa mnoo millioni 2 ni budget ndogo sana, na kwa ninavowajua developers wa bongo wakiweza niite mbwa nimekaa palee!!😅 Sio kama hawajui ila uvivu na wanahitaji usimamizi wa hali ya juu.
 
Kuna watu mnachekesha kweli, Hiyo project ya Adobe yenyewe imecost millions of dollars wewe unazungumzia developer wa bongo akutengenezee?? Hizo ni software kubwa mno sio Tanzania tu hata Afrika bado hatuna hao wataalam
 
Sasa, chuo wanaenda kusoma nini?
 
sijasomea hiyo kitu kabisa, lakini ukitaka tu website yenye database ndani yake inagonga huko. na hapa ndio napata mashaka ya budget yako.
 
2D mkuu; wengi wana maneno, kazi kidogo
2D ni nyepesi zaidi, Nadhani wanaweza! Sema cha kukushauri kwa budget ya milioni 2 ni ndogo, ukienda kwenye firm za IT watakwambia hata 50mils, ila nisikukatishe tamaa assemble team ya madogo walioko mtaani, jobless, njaa kali uwape ofa hio, wahudumie, wasimamie I believe watatoa kitu.
 
Kuna watu mnachekesha kweli, Hiyo project ya Adobe yenyewe imecost millions of dollars wewe unazungumzia developer wa bongo akutengenezee?? Hizo ni software kubwa mno sio Tanzania tu hata Afrika bado hatuna hao wataalam
Hapana IT sio space science kwamba washindwe mimi sio developer, sijasoma IT ila najua inawezekana. Kimachofanya watu wengine washindwe kutengeneza ni kwamba watamuuzia nani ila si kwamba haiwezekani
 
2D ni nyepesi zaidi, Nadhani wanaweza! Sema cha kukushauri kwa budget ya milioni 2 ni ndogo, ukienda kwenye firm za IT watakwambia hata 50mils, ila nisikukatishe tamaa assemble team ya madogo walioko mtaani, jobless, njaa kali uwape ofa hio, wahudumie, wasimamie I believe watatoa kitu.
Watu wanalalamika ajira hakuna; hii sasa imekuja, wenye ujuzi wajitokeze.
 
Hapana IT sio space science kwamba washindwe mimi sio developer, sijasoma IT ila najua inawezekana. Kimachofanya watu wengine washindwe kutengeneza ni kwamba watamuuzia nani ila si kwamba haiwezekani
Fursa imewaangukia sasa, inawezekana kupitia kazi hii, ikawa mwanzo wa kuendelea kupata masoko zaidi
 
Ila Developers wabongo kuna mahala wanakwama.......
Field kibao naliona Gap lao ( kama huku Kwenye Survey & Engineering ) wana nafasi kubwa sana.....
Toeni hata Copy za Autocad addins basi wakuu, kama Autocad ni gharama ( hapa mtaeleweka)
Addins kibao tunanua kwa bei kubwa ila najua wabongo mnaweza tengeneza.

Kama hampati mawazo mnitafute mie niwape basi.
 
Inawezekana elimu ikawa kwenye cheti tu; ila kiuhalisia hakuna ujuzi alioupata huko masomoni.
 
Ya video za 2D au 3D? Hii system ni kubwa mnoo millioni 2 ni budget ndogo sana, na kwa ninavowajua developers wa bongo wakiweza niite mbwa nimekaa palee!!😅 Sio kama hawajui ila uvivu na wanahitaji usimamizi wa hali ya juu.
Sio developers wa bongo ila ni pesa ndogo sana kwa developer yoyote dunia nzima.
Hiyo siyo kazi ya kitoto kama kutengeneza kiwebsite. Ona tu dau walilitoa adobe kuinunua figma wakati hata sio platform ya animation
 
Back
Top Bottom