Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Mkazi wa Magoweko wilayani Goweko mkoani Morogoro, Secilia Ching’unyau (22) amenusurika kifo akijaribu kujiua kwa kunywa sumu ya kuhifadhia mahindi aliyoichanganya na pombe aina ya Vodka-Cuca kwa madai ya wazazi kutaka kuvunja mahusiano kati yake na mpenzi wake.
Akizungumzia tukio hilo leo Januari 27, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, (SACP) Fortunatus Muslim, amesema tukio hilo limetokea katika mtaa wa Magoweko Tarafa na Wilaya ya Gairo, ambapo alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ya kuhifadhia mahindi aina ya Acteric, huku kiini cha tukio hilo kikiwa ni wivu wa kimapenzi kuwa wazazi wanaingilia kuvunja mahusiano na mpenzi wake.
“Inaelezwa mtuhumiwa alikunywa sumu hiyo kwa kuchanganya na pombe aina ya Vodka-cuca, ambapo alikutwa amelewa na kupoteza kumbukumbu huku akiwa ameegemea ukuta wa nyumba na pembeni yake kukiwa na vikopo viwili vya pombe aina ya Vodka/cuca vikiwa vimeshatumika na vikopo viwili vyenye kuhifadhia mahindi aina ya Acteric ambavyo vilikuwa bado havijatumika.
“Mtuhumiwa amelazwa katika Kituo cha Afya Gairo akiendelea na matibabu na kwamba hali yake inaendelea vizuri,” amesema Kamanda Muslim.