Mkuu kuna mawili sema watoto wakishapenda ni hatari sana,katika makubalianao yenu hapo naona kama jamaa hajazama sana kwa binti yako au binti ameonesha mapenzi yaliyopitiliza ndo maana kagomea mahali ya 500,000/=
Kwa mtazamo wangu nadhani kama jamaa angekuwa na nia thabiti na mapenzi ya dhati angejivuta japo hata kwa milioni moja,kwa uwiano wa 2M na 500K naona kabisa jamaa hana nia ya dhati,lakini hakuna namna maana binti kesha penda.
Nakumbuka wakati naenda kumtolea mahari mke wangu,malengo ambayo Mimi nilikuwa nimejiwekea nilikuwa ni Milioni moja na ikizidi sana ni 1.2M,tulipofika ukweni nikiwa na rafiki Yangu ,wakwe zangu walianza na mahali ya 2.5M ,tulibembeleza na mwisho wakakatalia 1.6M na kwa vile sikuwa na namna na binti nilimpenda ikanibidi nikubali,sikuwa na namna.
Sasa kama jamaa kakomalia 500K napata wasi wasi sana, lakini hakuna namna maana binti kesha zama,waache wkajenge familia.maana mahari si kipimo thabiti cha mapenzi
Sent from my TECNO KB7j using
JamiiForums mobile app