Binti aliyebebeshwa dawa za kulevya na mchumba wake wakati wa safari ya kwenda kutambulishwa ukweni

Binti aliyebebeshwa dawa za kulevya na mchumba wake wakati wa safari ya kwenda kutambulishwa ukweni

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,261
Reaction score
9,733
Jumapili nilikuwa nasikiliza kipindi cha njia panda cha Clouds nikasikia story yam dada flani anayeitwa Mansura.

Mansura ni mwenyeji wa Moshi, alikuja kuishi Dar mwaka 2013 wakati alipojiunga na chuo cha Bandari. Kama mnavyojua mabinti wa chuo, Manstura alikuwa ni sista du wa ukweli.

Siku moja akiwa Mlimani City kwenye Birthday ya rafiki yake, akakutana na jamaa flani. Anadai jamaa alikuwa kamzidi sana maana yeye kwa kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 23. Jamaa wakabadilishana namba wakacheza mziki na baada ya hapo wakawa karibu.

Jamaa akamwambia kuwa yeye ni raia wa Sierra Leone na dada kusikia kuwa siyo Mtanzania basi akasema huyu ndiye mwenyewe. Kama mnavyojua mabinti wa Kitanzania wanapenda foreigners wakidai kwamba sisi wanaume wa Kibongo ni waongo na hatujui mapenzi. Haijalishi ni foreigner wa wapi ili mradi foreigner tu.

Manstura na jamaa wakawa wapenzi, jamaa anamhudumia maana alikuwa na pesa na alimwambia Manstura kuwa yeye ni mfanyabiashara. Maisha yakaenda, bata ikaliwa kwa kama miezi 8.

Muda huo wote, Manstura hakwahi kumwambia dada yake kuwa yuko kwenye mahusiano. Aliyekuwa anajua ni mke wa kaka yake ambaye anaishi Moshi.

Anadai kwamba alikuwa akiongea na ndugu wa jamaa kupitia simu. Ikafika kipindi mwaka 2014, jamaa akamwambia anataka akamtambulishe kwao. Wakakubaliana kwamba wataondoka pasipo Manstrua kuaga na watakaa wiki arudi pasipo kwao kufahamu kwamba kasafiri.

Basi mipango ikapangwa ikapangika. Jamaa akamwambia kwamba kakosa tiketi Dar, hivyo itabidi wapande ndege kupitia KIA.

Basi wakasafiri mpaka Moshi. Manstura akaenda kumwambia huyo wifi yake kuwa yeye anasfiri anaenda kutambulishwa kwa wake. Lakini akamwomba asimwambie mtu. Wifi akawa na hofu itakuaje wakija kufahamu na wakafahamu kuwa yeye alijua na hakusema. Manstura akamtoa hofu kwamba itakuwa ni wiki tu atakuwa karudi.

Baadae jamaa akamwambia kuwa kakosi tiketi ya watu wawili, hivyo itabidi Manstura atangulie na mizigo atapokelewa na ndugu zake na yeye atafuata nyuma. Basi jamaa na Mansura wakapanga mabegi. Siku ya safari ikafika Mansura akiwa na mabegi matatu, huku jamaa akisindikiza wakakodi tax mpaka Airport –KIA.

Walipofika, jamaa akaanza piga simu akidai anampigia Manstura mtu atakayemsaidia process za kucheck in. Simu ikawa haipokelewi. Jamaa akamwambia Manstura asonge tu atafanya process mwenyewe. Manstura akasonga kama kawaida. Alipofika sehemu ya kucheck mizigo, wakaweka begi la kwanza likapita vizuri, begi la pili likapita vizuri, begi la tatu likapita, wakalirudisha mara ya pili likapita, wakalirudisha mara ya tatu lipatishwa. Askari akamuuliza, dada hili begi la kwako. Manstura akajibu, Ndiyo. Akamuuliza umelipanga mwenyewe? Manstura akajibu ndiyo. Akamwambia alifungue. Manstura akalifungua wakalipitisha tena. Wakamwambia kuna kitu wanakiona hakiko sawa kwenye hilo begi.

Wakamwambia unaturuhusu tulichane. Manstura akakubari. Wakachukua kisu wakachana pembeni. Ile kuchana tu, unga ukamwagika. Askari akasema, Yani mdada mrembo kama wewe unabeba dawa za kulevya. Manstura akasema mdawa gani. Askari akamjibu ina maana huna macho huoni huu unga. Manstura ndipo kustuka akajua sasa nimekwisha nguvu zikamwishia. Kumbe lile bag lilkuwa limetengenezwa kwa style maalum. Yani bag ndongo limeungwa na bag kubwa Halafu katikati wamejaza dawa.

Basi wakamwondoa kwenye mstari wakampeleka na kumfungia kwenye chumba pale KIA. Kumbe muda wote huo, mpopo alikuwa hajaondoka airport alikuwa nje kwenye tax anapiga simu kujua kama Manstura kafanikiwa kuvuka. Lakini simu ilikuwa ishachukuliwa na haipokelewi.

Baadae Manstura akachukuliwa, na kuanza kufanyiwa mahojiano. Akawambia kuwa lile begi aliletewana boyfriend wake. Akawaeleza kisa chote. Sasa mpopo baada ya kuona Manstura hapokei simu, akamtuma dereva tax akaangalie kuna nini. Dereva tax akaingia uwanjani, wakati anashangaa shangaa askari akamwona na kumfuata.

Akamuuliza unatafuta nini, akamwambia kuwa kuna mtu kamtuma acheck kama mpenzi wake keshaondoka. Askari akamwambia yuko wapi? Jamaa akasema yuko kwenye gari. Askari akamwita askari asiye na uniform aongozane na dereva tax, wakaenda na kumnasa.

Wakamleta alipo Manstura na kumuuliza kama namfahamu. Jamaa akaitika kuwa anamfahamu ni mchumba wake. Basi wote wakaungwa na kupelekwa kituoni.

To cut the story short, Manstura alikamatwa tarehe 12 Feb 2014, amekaa ndani kesi ikiendelea kwa miaka kadhaa. Katoka mwaka huu tarehe 12 Feb. Jamaa amehukumiwa kifungo cha maisha.

Manstura amekaa ndani hadi alikuwa Nyampara.

Ila amshukuru Mungu kuwa alikamatiwa hapa hapa TZ, angekamatwa huko mbele angesahau kutoka.

Wapopo na watu wa west Afrika madada mnawapenda ila si wakuaminika.
 
Hatari sana hii kuamini watu hovyo Kuna kipindi huonyeshwa national geographic kuhusu Hawa wadada wanavodaganyika na kuishia kukamatwa na kuteseka huwa kina funzo zuri sana. Siku moja nilikuwa airport nikashangaa wamekuja wakaka wananiomba niwasaidie mzigo wao mdogo eti kwa uzito umezidi nikikumbuka matukio ya watu kubebeshwa madawa bila kujua nikashtuka sana
 
Walitaka wakubebeshe mzigo. Hakuna kumwamini mtu ukiwa safarini maana unaweza kujikuta uko kwenye matatizo makubwa
 
Jumapili nilikuwa nasikiliza kipindi cha njia panda cha Clouds nikasikia story yam dada flani anayeitwa Mansura.

Mansura ni mwenyeji wa Moshi, alikuja kuishi Dar mwaka 2013 wakati alipojiunga na chuo cha Bandari. Kama mnavyojua mabinti wa chuo, Manstura alikuwa ni sista du wa ukweli.
Wadada Tz wengi warembo wanavyopenda maisha mazuri na ya mteremko, ni rahisi sana kwa Tz kumdanganya mdada asiyejua kwamba mambo kama haya yapo duniani. Ukiangalia vipindi kama "Banged Up Abroad" cha NatGeo channel wanaelezea matukio kama haya yaliyowapata real people. Binafsi huwa nawashauri wale ninaowafahamu sababu mambo kama haya yanatokea sana na mbele ya hela bahati mbaya ni rahisi mtu kudanganyika. Mungu awalinde wadogo zetu Tz kwa kweli.
 
Wapopo waliumiza sana wadada wa Kizungu. Wanakwenda club za vijijini huko na limousine. Wamepiga pamba designer kuanzia juu mpaka chini.

Wana target wadada naive, wakishawachukua wanawapeleks kwenye limousine wanawaambia wanarudi hotelini kulala, baada ya bata hili mdada anaambiwa tunakwenda holiday. Akijua maisha ndiyo ameyapatia kumbe yeye ni container.

Wanajua wadada wa Kizungu wanaweza kuzunguka dunia kwasababu ya passport zao, nchi nyingi wanapata visa unapoingia.
 
Hatari sana hii kuamini watu hovyo Kuna kipindi huonyeshwa national geographic kuhusu Hawa wadada wanavodaganyika na kuishia kukamatwa na kuteseka huwa kina funzo zuri sana. Siku moja nilikuwa airport nikashangaa wamekuja wakaka wananiomba niwasaidie mzigo wao mdogo eti kwa uzito umezidi nikikumbuka matukio ya watu kubebeshwa madawa bila kujua nikashtuka sana
Kuna safari nilijikuta namsaidia Mzee Mmoja mzigo wake airport kisa tulikua tu Watanzania nikajikuta namsaidia nikapita nao hadi kukaguliwa cha kushukuru Mungu hakua na madawa ila that was a stupidest thing nimefanya. Baada ya kuona zile shows za watu wanavyobebeshwa madawa bila kujua, kamwe usimsaidie mtu mzigo airport.
 
Hata awe mjanzito acha asaidiwe na wahudumu. Eti nikusaidie mzigo thubutu
 
Wapopo waliumiza sana wadada wa Kizungu. Wanakwenda club za vijijini huko na limousine. Wamepiga pamba designer kuanzia juu mpaka chini.

Wana target wadada naive, wakishawachukua wanawapeleks kwenye limousine wanawaambia wanarudi hotelini kulala, baada ya bata hili mdada anaambiwa tunakwenda holiday. Akijua maisha ndiyo ameyapatia kumbe yeye ni container.

Wanajua wadada wa Kizungu wanaweza kuzunguka dunia kwasababu ya passport zao, nchi nyingi wanapata visa unapoingia.
Duuuh, na mitoto ya kizungu inavyojifanyaga much know haishauriki acha wawatumie.
 
Back
Top Bottom