Binti aliyebebeshwa dawa za kulevya na mchumba wake wakati wa safari ya kwenda kutambulishwa ukweni

Binti aliyebebeshwa dawa za kulevya na mchumba wake wakati wa safari ya kwenda kutambulishwa ukweni

Angalia muda ambao wamedumu kwenye mahusiano na ndiyo utakubaliana na mimi kuiwa binti alikuwa anajua dili. Asingekuwa anajua, asingefungwa!
Madada unawajia unawaskia. Ukiwa na pesa hata ndani ya week unaweza mpeleka dsda kokote. Wana roho ngumu sana.
Kama dada unakutana naye mtandaoni hakujui unamwita kwako anakuja peke yake, si roho ngumu hiyo.
 
Hatari sana hii kuamini watu hovyo Kuna kipindi huonyeshwa national geographic kuhusu Hawa wadada wanavodaganyika na kuishia kukamatwa na kuteseka huwa kina funzo zuri sana. Siku moja nilikuwa airport nikashangaa wamekuja wakaka wananiomba niwasaidie mzigo wao mdogo eti kwa uzito umezidi nikikumbuka matukio ya watu kubebeshwa madawa bila kujua nikashtuka sana
Sometimes akili inakuwa kama imefungwa,unakuja kushtuka too late.
 
Kama alikuwa anaenda Moshi why asitumie private transport au hata Basi akaamua kutake risk ya kutumia Ndege wakati anaenda hapa hapa TZ huku akiwa amembebesha mwenzake madawa?hapa naomba ufafanuzi
Hapana hajaenda Moshi kwa ndege. Ticket za kwenda huko walikokuwa wanaenda, Dar hazikuwepo, ila zilikuwepo KIA kwa hiyo ili wakapandie huko. Wewe ulishawahi kuona kitu kama hiki wakati huu wa utandawazi? Walienda Moshi kwa usafiri gani, hilo halijasemwa. Hawa watu walikuwa kwenye dili na binti alikuwa anajua, hakubebeshwa!
 
Mkuu mimi nimesunnerize story maana nisingeweza kuandika kila kitu story kahadithia kipindi chote cha saa 2 nisingeweza kuandika kila detail.
Kahadithia mpaka maisha ya jela, wakili wake kamtaja jina, mahakimu wote walioendesha kesi, wa kwanza aliondoka akaikamata mwingine ndiye aliiendesha mpera mpera mpaka akatoka.
Mwaka 2018, mwendesha mashitaka alisema hana nia ya kuendelea na hiyo kesi akaachiwa, ile anafika nje akadakwa kumbe waliifunga na kuifungua tena upya.
Kuna mambo mengi sana alihadithia
 
Nimesoma na mtu anaitwa mastura abdul probably Ni yeye kwa kuwa amesema alisoma arusha namfahamau vzr huyu mtoto
 
Madada unawajia unawaskia. Ukiwa na pesa hata ndani ya week unaweza mpeleka dsda kokote. Wana roho ngumu sana.
Kama dada unakutana naye mtandaoni hakujui unamwita kwako anakuja peke yake, si roho ngumu hiyo.
Hahaha hii kweli kabisa hawa watu wanakua na ujasiri wa hali ya juu sana, hakujui wala hajawahi kukuona lakini anakuja mafichoni bila chembe ya hofu kama mmejuana miaka 5 iliyopita.
 
Alivokuja peke yake ukamfanyaje?
 
Hahaha hii kweli kabisa hawa watu wanakua na ujasiri wa hali ya juu sana, hakujui wala hajawahi kukuona lakini anakuja mafichoni bila chembe ya hofu kama mmejuana miaka 5 iliyopita.
Wana ujasiri wa hali ya juu na hasa wakiona pesa. Kuna mke wa jamaa yangu ananiambiaga kipindi ameanza date na rafiki yangu alikuwa anahisi anauza unga kwasababu alikuwa mara nyingi anamkuta ana bag la pesa kwenye gari halafu anaenda badilisha hilo bag na watu flani au anapokea bag la pesa toka kwa mtu kwenye parking.
Lakini na kuona hayo yote hakuwa na wazo la kujiepusha naye, kisa alikuwa anamhudumia
 
Huwa nakitizama hicho kipindi. Kuna kingine kinaitwa "Airport Sericuty". Akina dada wanaingizwa mkenge kwa jina la mapenzi. Wengine wanakubali kubeba lakini pia wapo wanaowekewa katika suitcase bila kujua.
Hatari sana hii kuamini watu hovyo Kuna kipindi huonyeshwa national geographic kuhusu Hawa wadada wanavodaganyika na kuishia kukamatwa na kuteseka huwa kina funzo zuri sana. Siku moja nilikuwa airport nikashangaa wamekuja wakaka wananiomba niwasaidie mzigo wao mdogo eti kwa uzito umezidi nikikumbuka matukio ya watu kubebeshwa madawa bila kujua nikashtuka sana
 
Jumapili nilikuwa nasikiliza kipindi cha njia panda cha Clouds nikasikia story yam dada flani anayeitwa Mansura.

Mansura ni mwenyeji wa Moshi, alikuja kuishi Dar mwaka 2013 wakati alipojiunga na chuo cha Bandari. Kama mnavyojua mabinti wa chuo, Manstura alikuwa ni sista du wa ukweli.

Siku moja akiwa Mlimani City kwenye Birthday ya rafiki yake, akakutana na jamaa flani. Anadai jamaa alikuwa kamzidi sana maana yeye kwa kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 23. Jamaa wakabadilishana namba wakacheza mziki na baada ya hapo wakawa karibu.

Jamaa akamwambia kuwa yeye ni raia wa Sierra Leone na dada kusikia kuwa siyo Mtanzania basi akasema huyu ndiye mwenyewe. Kama mnavyojua mabinti wa Kitanzania wanapenda foreigners wakidai kwamba sisi wanaume wa Kibongo ni waongo na hatujui mapenzi. Haijalishi ni foreigner wa wapi ili mradi foreigner tu.

Manstura na jamaa wakawa wapenzi, jamaa anamhudumia maana alikuwa na pesa na alimwambia Manstura kuwa yeye ni mfanyabiashara. Maisha yakaenda, bata ikaliwa kwa kama miezi 8.

Muda huo wote, Manstura hakwahi kumwambia dada yake kuwa yuko kwenye mahusiano. Aliyekuwa anajua ni mke wa kaka yake ambaye anaishi Moshi.

Anadai kwamba alikuwa akiongea na ndugu wa jamaa kupitia simu. Ikafika kipindi mwaka 2014, jamaa akamwambia anataka akamtambulishe kwao. Wakakubaliana kwamba wataondoka pasipo Manstrua kuaga na watakaa wiki arudi pasipo kwao kufahamu kwamba kasafiri.

Basi mipango ikapangwa ikapangika. Jamaa akamwambia kwamba kakosa tiketi Dar, hivyo itabidi wapande ndege kupitia KIA.

Basi wakasafiri mpaka Moshi. Manstura akaenda kumwambia huyo wifi yake kuwa yeye anasfiri anaenda kutambulishwa kwa wake. Lakini akamwomba asimwambie mtu. Wifi akawa na hofu itakuaje wakija kufahamu na wakafahamu kuwa yeye alijua na hakusema. Manstura akamtoa hofu kwamba itakuwa ni wiki tu atakuwa karudi.

Baadae jamaa akamwambia kuwa kakosi tiketi ya watu wawili, hivyo itabidi Manstura atangulie na mizigo atapokelewa na ndugu zake na yeye atafuata nyuma. Basi jamaa na Mansura wakapanga mabegi. Siku ya safari ikafika Mansura akiwa na mabegi matatu, huku jamaa akisindikiza wakakodi tax mpaka Airport –KIA.

Walipofika, jamaa akaanza piga simu akidai anampigia Manstura mtu atakayemsaidia process za kucheck in. Simu ikawa haipokelewi. Jamaa akamwambia Manstura asonge tu atafanya process mwenyewe. Manstura akasonga kama kawaida. Alipofika sehemu ya kucheck mizigo, wakaweka begi la kwanza likapita vizuri, begi la pili likapita vizuri, begi la tatu likapita, wakalirudisha mara ya pili likapita, wakalirudisha mara ya tatu lipatishwa. Askari akamuuliza, dada hili begi la kwako. Manstura akajibu, Ndiyo. Akamuuliza umelipanga mwenyewe? Manstura akajibu ndiyo. Akamwambia alifungue. Manstura akalifungua wakalipitisha tena. Wakamwambia kuna kitu wanakiona hakiko sawa kwenye hilo begi.

Wakamwambia unaturuhusu tulichane. Manstura akakubari. Wakachukua kisu wakachana pembeni. Ile kuchana tu, unga ukamwagika. Askari akasema, Yani mdada mrembo kama wewe unabeba dawa za kulevya. Manstura akasema mdawa gani. Askari akamjibu ina maana huna macho huoni huu unga. Manstura ndipo kustuka akajua sasa nimekwisha nguvu zikamwishia. Kumbe lile bag lilkuwa limetengenezwa kwa style maalum. Yani bag ndongo limeungwa na bag kubwa Halafu katikati wamejaza dawa.

Basi wakamwondoa kwenye mstari wakampeleka na kumfungia kwenye chumba pale KIA. Kumbe muda wote huo, mpopo alikuwa hajaondoka airport alikuwa nje kwenye tax anapiga simu kujua kama Manstura kafanikiwa kuvuka. Lakini simu ilikuwa ishachukuliwa na haipokelewi.

Baadae Manstura akachukuliwa, na kuanza kufanyiwa mahojiano. Akawambia kuwa lile begi aliletewana boyfriend wake. Akawaeleza kisa chote. Sasa mpopo baada ya kuona Manstura hapokei simu, akamtuma dereva tax akaangalie kuna nini. Dereva tax akaingia uwanjani, wakati anashangaa shangaa askari akamwona na kumfuata.

Akamuuliza unatafuta nini, akamwambia kuwa kuna mtu kamtuma acheck kama mpenzi wake keshaondoka. Askari akamwambia yuko wapi? Jamaa akasema yuko kwenye gari. Askari akamwita askari asiye na uniform aongozane na dereva tax, wakaenda na kumnasa.

Wakamleta alipo Manstura na kumuuliza kama namfahamu. Jamaa akaitika kuwa anamfahamu ni mchumba wake. Basi wote wakaungwa na kupelekwa kituoni.

To cut the story short, Manstura alikamatwa tarehe 12 Feb 2014, amekaa ndani kesi ikiendelea kwa miaka kadhaa. Katoka mwaka huu tarehe 12 Feb. Jamaa amehukumiwa kifungo cha maisha.

Manstura amekaa ndani hadi alikuwa Nyampara.

Ila amshukuru Mungu kuwa alikamatiwa hapa hapa TZ, angekamatwa huko mbele angesahau kutoka.

Wapopo na watu wa west Afrika madada mnawapenda ila si wakuaminika.
Kuna masista du wengine nilisoma nao chuo back n days, wapo India wanatumikia miaka yao, mabinti wa kibongo wanapenda shortcuts sana, mimi kuna msenge nliwahi mnunulia iPhone 8 enzi hizo penzi bado la moto na sina majukumu baadae akapata foreigner akamdanganya anafanya kazi ubalozi fulani, akampangishia nyumba nzima ushuani Dar na mtaji wa duka milioni 17 akampatia, mm kuona vile nikakaa pembeni japo alinisihi nisifanye hivyo kwa kua kule alifuata pesa akataka niendelee kuichakata, kwa kua nami mambo yangu yalikua fresh nikamshit, maana siwezi share penzi kwa kufahamu kabisa, otherwise niwe sijui, nikatafuta chimbo jipya, nimekutana nae juzi mjini hata haelewi kama Msimbazi iko kariakoo, ananisimulia story ndeeeefu ambayo haina impact kwangu, inshort alikamatika baadae hajui anaanzia wapi
 
Wapopo siyo watu wazuri. Ni hatari sana mkuu tamaa zitawaua.
 
Mwanza airport wapo na ndoo za plastic za fillet za sato. Huwa nakataa. Unaweza kuishia kunyongwa for nothing. Wema wa airport wa kuchukuwa mzigo wa mtu ni wema wa kijinga.
Kuna safari nilijikuta namsaidia Mzee Mmoja mzigo wake airport kisa tulikua tu Watanzania nikajikuta namsaidia nikapita nao hadi kukaguliwa cha kushukuru Mungu hakua na madawa ila that was a stupidest thing nimefanya. Baada ya kuona zile shows za watu wanavyobebeshwa madawa bila kujua, kamwe usimsaidie mtu mzigo airport.
 
Huwa nakitizama hicho kipindi. Kuna kingine kinaitwa "Airport Sericuty". Akina dada wanaingizwa mkenge kwa jina la mapenzi. Wengine wanakubali kubeba lakini pia wapo wanaowekewa katika suitcase bila kujua.
Ni kweli wanawake huwa ni victims huingiliwa kwa gear ya mapenzi, au wengine huwekewa bila wao kujua Matokeo yake huwa ni kudakwa hasa wale walinzi wakibadilishwa. So vipindi ka hivo vinaelimisha sema watu hawavipendi wanapenda miziki
 
Walitaka wakubebeshe mzigo. Hakuna kumwamini mtu ukiwa safarini maana unaweza kujikuta uko kwenye matatizo makubwa
Yani na tulikuwa watu wengi wakanifata Mimi eti niwasaidie wamezidiwa woooi nilivokumbuka hicho kipindi cha national geographic nikasema shindwa shetani hunipati ng'o nikakataa
 
Back
Top Bottom