Binti aliyebebeshwa dawa za kulevya na mchumba wake wakati wa safari ya kwenda kutambulishwa ukweni

Binti aliyebebeshwa dawa za kulevya na mchumba wake wakati wa safari ya kwenda kutambulishwa ukweni

Kuna safari nilijikuta namsaidia Mzee Mmoja mzigo wake airport kisa tulikua tu Watanzania nikajikuta namsaidia nikapita nao hadi kukaguliwa cha kushukuru Mungu hakua na madawa ila that was a stupidest thing nimefanya. Baada ya kuona zile shows za watu wanavyobebeshwa madawa bila kujua, kamwe usimsaidie mtu mzigo airport.
Una bahati angekuwa na mzigo ungedakwa wewe na ingekuwa bongo ni kifungo Cha maisha hicho
 
Yani na tulikuwa watu wengi wakanifata Mimi eti niwasaidie wamezidiwa woooi nilivokumbuka hicho kipindi cha national geographic nikasema shindwa shetani hunipati ng'o nikakataa
Binadamu, na sasa ukamatwe nchi kama china
 
Yes mkuu, aliingia 12 feb katoka 12 feb yani tarehe ile ile.
Anajuta chuo hakumaliza, katoka gerezani akiwa na elimu ya ujasiriamali na anatengeneza sabuni za maji sasa.
Anasema anataka baadae arudi chuo ila kwa sasa akili yake anahisi haijawa tayari
Nikikumbuka Hamisa alivyomegwa na yule bonge nyanya na huko mitandaoni sie wakibongo tukaonekana si kitu.. Nadhani kuna masomo inabidi tuwafunze wadogo zetu
 
Camera za airport zilikuwa zimekwisha wanasa pamoja. Kilichomsaidia dada ni kuwa jamaa alizubaa airport baada ya simu kutokupokelewa. Machale yangemcheza na kuondoka moja kwa moja, huyo dada kifungo hicho cha maisha kingemhusu yeye.
Sema jamaa naye alikuwa mwaminifu, hakumkana alipoulizwa uhusiano wake na mdada. (Ila inawezekanaje jamaa akubali kumfahamu mdada kwa situation kama ile!?!?! Najiuliza).

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Nikikumbuka Hamisa alivyomegwa na yule bonge nyanya na huko mitandaoni sie wakibongo tukaonekana si kitu.. Nadhani kuna masomo inabidi tuwafunze wadogo zetu
Mabinti wanaangalia pesa tu. Wana wa miss use kama public funds
 
Yanatokea. Angalia "Banged up abroad" na "Airport security" kwenye National Geographic. Sehemu ambayo siamini ni pale kwa jamaa kupiga simu, haipokelewi, halafu anatuma taxi driver kwenda kuchungulia. Wauza unga huwa wana machale sana. Simu kama haipokelewi, wanapotea mara moja hata kwa miguu.
Sijui kwanini sijaiamini hii storeee
 
Kuna masista du wengine nilisoma nao chuo back n days, wapo India wanatumikia miaka yao, mabinti wa kibongo wanapenda shortcuts sana, mimi kuna msenge nliwahi mnunulia iPhone 8 enzi hizo penzi bado la moto na sina majukumu baadae akapata foreigner akamdanganya anafanya kazi ubalozi fulani, akampangishia nyumba nzima ushuani Dar na mtaji wa duka milioni 17 akampatia, mm kuona vile nikakaa pembeni japo alinisihi nisifanye hivyo kwa kua kule alifuata pesa akataka niendelee kuichakata, kwa kua nami mambo yangu yalikua fresh nikamshit, maana siwezi share penzi kwa kufahamu kabisa, otherwise niwe sijui, nikatafuta chimbo jipya, nimekutana nae juzi mjini hata haelewi kama Msimbazi iko kariakoo, ananisimulia story ndeeeefu ambayo haina impact kwangu, inshort alikamatika baadae hajui anaanzia wapi
Hahaha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]



Yaan haelewi msimbazi iko wapi na kakulia dar? Haahaahaa

Mkuu elezea kidogo alifanyaje kwani?
 
Jumapili nilikuwa nasikiliza kipindi cha njia panda cha Clouds nikasikia story yam dada flani anayeitwa Mansura.

Mansura ni mwenyeji wa Moshi, alikuja kuishi Dar mwaka 2013 wakati alipojiunga na chuo cha Bandari. Kama mnavyojua mabinti wa chuo, Manstura alikuwa ni sista du wa ukweli.

Siku moja akiwa Mlimani City kwenye Birthday ya rafiki yake, akakutana na jamaa flani. Anadai jamaa alikuwa kamzidi sana maana yeye kwa kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 23. Jamaa wakabadilishana namba wakacheza mziki na baada ya hapo wakawa karibu.

Jamaa akamwambia kuwa yeye ni raia wa Sierra Leone na dada kusikia kuwa siyo Mtanzania basi akasema huyu ndiye mwenyewe. Kama mnavyojua mabinti wa Kitanzania wanapenda foreigners wakidai kwamba sisi wanaume wa Kibongo ni waongo na hatujui mapenzi. Haijalishi ni foreigner wa wapi ili mradi foreigner tu.

Manstura na jamaa wakawa wapenzi, jamaa anamhudumia maana alikuwa na pesa na alimwambia Manstura kuwa yeye ni mfanyabiashara. Maisha yakaenda, bata ikaliwa kwa kama miezi 8.

Muda huo wote, Manstura hakwahi kumwambia dada yake kuwa yuko kwenye mahusiano. Aliyekuwa anajua ni mke wa kaka yake ambaye anaishi Moshi.

Anadai kwamba alikuwa akiongea na ndugu wa jamaa kupitia simu. Ikafika kipindi mwaka 2014, jamaa akamwambia anataka akamtambulishe kwao. Wakakubaliana kwamba wataondoka pasipo Manstrua kuaga na watakaa wiki arudi pasipo kwao kufahamu kwamba kasafiri.

Basi mipango ikapangwa ikapangika. Jamaa akamwambia kwamba kakosa tiketi Dar, hivyo itabidi wapande ndege kupitia KIA.

Basi wakasafiri mpaka Moshi. Manstura akaenda kumwambia huyo wifi yake kuwa yeye anasfiri anaenda kutambulishwa kwa wake. Lakini akamwomba asimwambie mtu. Wifi akawa na hofu itakuaje wakija kufahamu na wakafahamu kuwa yeye alijua na hakusema. Manstura akamtoa hofu kwamba itakuwa ni wiki tu atakuwa karudi.

Baadae jamaa akamwambia kuwa kakosi tiketi ya watu wawili, hivyo itabidi Manstura atangulie na mizigo atapokelewa na ndugu zake na yeye atafuata nyuma. Basi jamaa na Mansura wakapanga mabegi. Siku ya safari ikafika Mansura akiwa na mabegi matatu, huku jamaa akisindikiza wakakodi tax mpaka Airport –KIA.

Walipofika, jamaa akaanza piga simu akidai anampigia Manstura mtu atakayemsaidia process za kucheck in. Simu ikawa haipokelewi. Jamaa akamwambia Manstura asonge tu atafanya process mwenyewe. Manstura akasonga kama kawaida. Alipofika sehemu ya kucheck mizigo, wakaweka begi la kwanza likapita vizuri, begi la pili likapita vizuri, begi la tatu likapita, wakalirudisha mara ya pili likapita, wakalirudisha mara ya tatu lipatishwa. Askari akamuuliza, dada hili begi la kwako. Manstura akajibu, Ndiyo. Akamuuliza umelipanga mwenyewe? Manstura akajibu ndiyo. Akamwambia alifungue. Manstura akalifungua wakalipitisha tena. Wakamwambia kuna kitu wanakiona hakiko sawa kwenye hilo begi.

Wakamwambia unaturuhusu tulichane. Manstura akakubari. Wakachukua kisu wakachana pembeni. Ile kuchana tu, unga ukamwagika. Askari akasema, Yani mdada mrembo kama wewe unabeba dawa za kulevya. Manstura akasema mdawa gani. Askari akamjibu ina maana huna macho huoni huu unga. Manstura ndipo kustuka akajua sasa nimekwisha nguvu zikamwishia. Kumbe lile bag lilkuwa limetengenezwa kwa style maalum. Yani bag ndongo limeungwa na bag kubwa Halafu katikati wamejaza dawa.

Basi wakamwondoa kwenye mstari wakampeleka na kumfungia kwenye chumba pale KIA. Kumbe muda wote huo, mpopo alikuwa hajaondoka airport alikuwa nje kwenye tax anapiga simu kujua kama Manstura kafanikiwa kuvuka. Lakini simu ilikuwa ishachukuliwa na haipokelewi.

Baadae Manstura akachukuliwa, na kuanza kufanyiwa mahojiano. Akawambia kuwa lile begi aliletewana boyfriend wake. Akawaeleza kisa chote. Sasa mpopo baada ya kuona Manstura hapokei simu, akamtuma dereva tax akaangalie kuna nini. Dereva tax akaingia uwanjani, wakati anashangaa shangaa askari akamwona na kumfuata.

Akamuuliza unatafuta nini, akamwambia kuwa kuna mtu kamtuma acheck kama mpenzi wake keshaondoka. Askari akamwambia yuko wapi? Jamaa akasema yuko kwenye gari. Askari akamwita askari asiye na uniform aongozane na dereva tax, wakaenda na kumnasa.

Wakamleta alipo Manstura na kumuuliza kama namfahamu. Jamaa akaitika kuwa anamfahamu ni mchumba wake. Basi wote wakaungwa na kupelekwa kituoni.

To cut the story short, Manstura alikamatwa tarehe 12 Feb 2014, amekaa ndani kesi ikiendelea kwa miaka kadhaa. Katoka mwaka huu tarehe 12 Feb. Jamaa amehukumiwa kifungo cha maisha.

Manstura amekaa ndani hadi alikuwa Nyampara.

Ila amshukuru Mungu kuwa alikamatiwa hapa hapa TZ, angekamatwa huko mbele angesahau kutoka.

Wapopo na watu wa west Afrika madada mnawapenda ila si wakuaminika.
Wasichana wengi wanapenda watu wa nje wakidanganywa kidogo wanaamini huyo atakuwa kapata fundisho na chuo hakumaliza na kwasasa anajutia tamaa zake za pesa
 
Kama haukumwelewa mwandishi, sijui kama kuna mtu anaweza kukuelewesha!!
Kama alikuwa anaenda Moshi why asitumie private transport au hata Basi akaamua kutake risk ya kutumia Ndege wakati anaenda hapa hapa TZ huku akiwa amembebesha mwenzake madawa?hapa naomba ufafanuzi
 
Yanatokea. Angalia "Banged up abroad" na "Airport security" kwenye National Geographic. Sehemu ambayo siamini ni pale kwa jamaa kupiga simu, haipokelewi, halafu anatuma taxi driver kwenda kuchungulia. Wauza unga huwa wana machale sana. Simu kama haipokelewi, wanapotea mara moja hata kwa miguu.
Exactly mkuu...kipengele hicho cha kumtuma dereva tax akachungulie ndo nimeona nimepata wenge...

Airport security nakifatilia sana, pale ndo utajua watu wanajua kujilipua hasa wachina na wamexico
 
Kwani Huyo Dada alihukumiwa au alikua rumande tu?
 
Nadhani jamaa anachouliza ni hiki walipanda ndege kwenda moshi au walitumia usafiri WA gari, kama walipanda ndege walifanikiwa vipi kupita airport JKN
Hujaelewa walienda mosh then KIA kwa ajaili ya safari ya kwenda huko west africa. Airport KIA alikamatwa akiwa anaenda kukwea pipa to Sierra Leone
 
Mwanza airport wapo na ndoo za plastic za fillet za sato. Huwa nakataa. Unaweza kuishia kunyongwa for nothing. Wema wa airport wa kuchukuwa mzigo wa mtu ni wema wa kijinga.
Hakika kuna binti wa Australia alipewa toy tu na rafiki yake wakiwa airport Mexico akalibeba kupita nalo kumbe ndani lina ngada. Alikaa miaka 16 ndani pasi na kutegemea
 
Camera za airport zilikuwa zimekwisha wanasa pamoja. Kilichomsaidia dada ni kuwa jamaa alizubaa airport baada ya simu kutokupokelewa. Machale yangemcheza na kuondoka moja kwa moja, huyo dada kifungo hicho cha maisha kingemhusu yeye.
drug delar hatakiwi kuukimbia msala kama jambazi maana ana dili na mzigo ule wa Uga ana takiwa asolve kwa means yeyote mzigo uende ndio maana alikwama
 
Back
Top Bottom