Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Kwema Wakuu!

Hii inavunja moyo kwa wanaume walioamua kuoa single Mothersl.
Haiwezekani binti umelelewa tangu ukiwa mtoto, ukasomeshwa na Baba mlezi(wakambo) ukamaliza mpaka chuo cha usimamizi wa fedha.

Miaka yote huyo Babaako mzazi hakuwepo. Hakujua unakula nini wala unavaa níni. Wala hakuonyesha kujali,

Umefikisha miaka 25 ndio anajitokeza.
Siku ya harusi unampa heshima kipaombele huku ukimpuuza baba wa kambo aliyekulea.

Nimeumia sana. Hii sherehe imefanyika jana jioni.
Mzee wa Watu katia huruma kweli. Mama mtu naye ni kama hakuonyesha kujali zaidi ya kufurahia sherehe ya binti yake huku aliyemlea sura yake ikiwa haina furaha.

Hata kutambulishwa tuu.

Aiseeh!

Hata kula sikula nilirudi kula makande yangu.

Hekima ni kitu muhimu sana.

Jioni njema
We umejudge kwa situation moja tu,ila jua familia zina siri nyingi,kuanzia mtoto mpaka binti anakuwa kiasi cha kuolewa ni miaka mingi,wat if kama baba mzazi alikuwa anahudumia,wat if kama baba mlezi kuna vitu alifanya vya kumkosea heshima binti,wat if baba mlezi alimwonyesha binti anambagua waziwazi,kiuhalisia ni ngum sana mtoto wa kike ukamlea kama binti yako mpaka anakua alafu akaja kukutosa cku ya harusi,na kama hicho kitu kimetokea kweli (coz binadam hawatabiriki pia) basi we pray karma ichukue nafasi yake.
 
Back
Top Bottom