Binti Ana Ujauzito wa Miezi 3, Sasa Wazazi Wake Wanataka Nikae Naye—Lakini Bado Sijajipanga

Binti Ana Ujauzito wa Miezi 3, Sasa Wazazi Wake Wanataka Nikae Naye—Lakini Bado Sijajipanga

Usifanye jambo hilo la kutoa mimba. Mchukue binti. Hiyo ndiyo maana ya upendo. Usimpende wakati wa starehe tu. Umaweza kuwa na mashaka mengi lakini ukianza maisha yawezekana ukashangaa maisha yanaenda.

Mambo ya kitoa mimba, waweza kuishia kufanya mauaji ya watu wawili, mama na mtoto. Mtoto huyo atakapokuwa mkubwa unaweza kujishangaa kwa nini ulifikiria kumwua. Sahizi humwoni, unaweza usiwe na uchungu naye, lakini akishakua, anaweza kuwa chanzo cha firaha yako. Yapokeeyote kwa moyo wa upendo, trna wala usioneshe kama vilr unalazimishwa.
Well said. Nilikuwa namjaribu tu mleta mada.
 
Mkuu,

Anza mkakati wa malezi mapema, nsikufiche mkuu muhindi anapesa zetu nyingi sana, mwendo ni odd mbili mbili kwa siku
Kila stake weka 100k, utashangaa ndani ya week mbili hiyo sio changamoto tena, sasa akili itaanza kuwaza kuhusu uridhi
 
Kwamba hilo jambo limekuja ghafla?
 
Una makosa wajibika.

lakini sijui nani ongee na mabinti kuhusu hili jamani.

Hutakiwi mbebea mimba mtu ikiwa hamjapanga.
 
Habari za muda huu wakuu mimi ni kijana wa kiume
Miez minne iliyopita nilianza uhusiano na binti mmoja jirani na ofisini kwangu. Ni binti mdogo miaka 22 na bado anaishi na wazazi wake.
Ishu ikatokea binti nimempa ujauzito na sasa una miezi mitatu juzi nimeitwa kwao mama yake anataka kunikabdhi binti nikakae nae kwangu hapa anasubiliwa baba yake ambae yupo safarini kikazi arudi mchakato uanze.

Sasa ndugu zangu mimi bado sijajipanga kuowa mshahara wangu ni laki 6 tu na sina kitega uchumi kingine naishi kwenye chumba kimoja tena kisela sina kijiko wala kikombe. Ntawezaje kujivika majukumu ya kuishi na mtu nawaza malengo yangu yatatimia kweli je siku nikikosa kazi na tayari nina familia inanitegemea. Ushauri wenu ndugu zagu hapa nimeshaambiwa na mama mkwe inabidi tuanze kliniki nachoka ndugu zangu. Naombeni ushauri ni kipi nifanye hapa au wenzangu mliopitia hali kama hii mliwezaje kusarvive.
Ingekuwa binti yangu hadi saivi free melancholic zingekuwa za kutosha tu
 
Hivi unamfahamu hao walinzi unaowaona na ma uniform mishahara yao Huwa haizidi laki tatu na Wana famili Tena kubwa tu
Acha woga mtoto wa kiume ukishaweza kutia mimba manake umekua na kuhudumia utaweza tu
 
Back
Top Bottom