mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Habari za jioni wakuu mabibi na mabwana
Huyu binti namfahamu tangu akiwa mtoto. Anatoka kwenye mazingira magumu kuliko ngumu wenyewe.
Hamjui baba yake mzazi, hajawahi kumsikia wala kumuona.
Mazingira ambayo mama yake hawezi kumiliki hata simu ya elfu20, hawezi lipa kodi vyumba2 vya elfu 60 uswahilini kwetu huku, hana uhakika wa kulisha watoto wake milo miwili kwa siku lakini amepambana hadi binti kafika kidato cha sita kwa msaada wa serikali na amepata hayo matokeo hapo.
Alipofaulu kidato cha nne kwenda kidato cha tano mkoani hata nauli wachana na Ile ada ya elfu70 ya Magufuli ilikua shughuli kubwa. Wakati wa kufunga shule ndio ilikua hadi walimu wapige simu kwa namba atakazowapa za ndugu na jamaa ndio arudi njiani. Yaani kwa kifupi amekua kwenye mazingira magumu nyakati zote shuleni na nyumbani
Pamoja na kuwa amesoma shule zetu za serikali tangu chekechea hadi kidato cha sita na matokeo yake ni hayo hapo, amejitahidi kadri ya uwezo wake kwa lengo la kuja kusomea masomo ya utabibu kama udaktari au maana ya lakini leo nimeumia kidogo baada ya kumkuta kajikunyata kwa huzuni baada ya kukosa ufadhili au mkopo wa serikali kwa kozi hizo ambazo ada zake zipo juu
Nimewaza nikaona nije hapa jukwaani kwa wajuzi wa mambo maana najua hapa kuna wazoefu, walimu, wasomi, washauri, wazazi wenye mapenzi mema labda Huyu binti anaweza saidika
Mtoto wa mwenzio no mtoto wako, natanguliza shukrani
Nawasilisha🤝
Cc Dada Ummy Wizara ya Afya Tanzania