Mashisha haya wanayovuta watoto wa kike siku hizi sio salama sijui kwann wanayapenda.
Kuna jambo ambalo naona ni changamoto sana na jamii inatakiwa kulitafakari upya.
Vijana wengi wanakutwa na umri wa kuanza mahusiano wakiwa kwa wazazi. Shinikizo la wazazi linakuwa ni kwamba mapenzi ni kitu haramu na hutakiwi kuyaingia hadi umalize shule.
Ule muda wa kumaliza shule ni mrefu na hapo katikati vishawishi ni vingi. Vijana na mabinti wengi wanapotea eneo hilo na kuharibu future zao za kimahusiano sababu ya kusubiria wakati rasmi ambao huwa ni miaka mingi mbele.
Matokeo ndio kama hivi, vijana na mabinti wanakuwa na shughuli za kimahusiano zisizo rasmi na wazazi hawajui lolote.