Binti ninayemtongoza anataka nimuazime Tsh. 100,000/-

Binti ninayemtongoza anataka nimuazime Tsh. 100,000/-

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,479
Reaction score
1,348
Wakuu habari za muda huu,

Nisiwachoshe na mambo mengi ngoja nije moja kwa moja kwenye mada. Wiki iliyopita katika harakati zangu za kutafuta nilikutana na binti mrembo kiasi.

Kama mjuavyo hulka ya mwanaume anapokutana na pisi lazima utesti mambo. Kwangu pia ilikua hivi toka siku nilipokutana na huyo mrembo niakaaza kumtongoza kwa sababu tayari nilishachukua namba yake licha ya yeye kuto toa jibu la kunikubalia.

Leo kanitumia meseji ya kuniomba shilingi 100,000 kwa masharti ya kumuazima na atarudisha baadae ya wiki 2 Mara baada ya kupokea mshahara kwa kuwa ni mfanyakazi.

Binafsi sijamjibu na sijajua mpaka sasa namjibu nini, nimeamua kuandika hapa ili kuomba ushauri kwamba pisi unayoitokea inapokuomba uiazime pesa itaweza kurejesha kweli? Lakini pia kama ikitokea nikamwazima hiyo pesa ataweka uzito wa kuirejesha kweli?
 
Kama huna achana naye.

Ila kama mkwanja unao why not? Mpe tu, usipomtumia hupati mzigo.

Kama vipi mueleze tu mfanye biashara.
 
Wanawake wa siku hizi wanna akili saana kuliko wa zamani

Zamani binti kama hakutaki alikuwa hataki hata kukutana na wewe
Hawa awamu hii wakakaa kikao wakajadili kwamba kumwambia mtu mzima mwenzio kwamba sikutaki siyo ustarabu

Wengi wao wakaona iwe fursa yaani ukiona mtu hujamwelewa lakini yeye kang'ang'ana wewe shusha nyavu zako vua kadri ya uwezo wako
Vijana wengi mmejikuta mko njia panda kwa kukosa maarifa

"MWANAMKE MWENYE NIA NZURI HAKUOMBI HELA"
Labda awe amebanwa kwelikweli

100000 kwa hapa uswahilini kwetu ni kodi ya miezi 5
 
Back
Top Bottom