Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Hapa watakwambia umechanganyikiwa! Mtu anasoma masters mpaka PhD anavuka na border, anarudi Tanzania kuuza makande. Pathetic.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha Aise
l8klTYmW1T6EBH-13qFYiZBlj6Z3EseHRtozcuQZfS5IefpyoP4ZGyuqTZQpBwrR-19dPjoX_wAKlv2M7r7ihCBcL64HH...jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli umeongea point ya maana lakin walio wengi humu Kwa unafki wao hatokosa sababu ya kupinga hoja yako ila kiukweli mitaji ndio inawakwamisha sana vijana katika kufikia malengo
Kwani biashara ya makande inahitaji mtaji kiasi gani
 
Ukitaka watu wakupigie makofi basi wape wazo lako la kuendelea kuwa ndani ya Confort zone hapo utashangiliwa sana.

Dada wa MWANZA angekuja na Idea ya Kufungua Duka kali la Urembo angeshangiliwa sana, Duka la Nguoa watu wangeshangilia mno, Salooni kari ya kike watu wangeshangilia sana, Baa tungeshangilia sana.

Tungeshangilia kwa sababu ni vitu vya Confort zone zetu.


Ukitaka ukamwe basi waso lako la nje kabisa ya Confort zone wapelekee watu wa ndani ya Confort zone. Hahaaa hapo unakamwa milele

DADA MWENYE BIASHARA YA KANDE MWANZA nazani aliomba ushauri kutoka kwa watu wa walio kwisha toka kabisa nje ya Confort zone zao. la sivyo asingefanya ile biashara. yaani angeomba ushauri kutoka kwa watu kama sisi tungeishia kumwambia anajiabisha.


Nisha wahi kuleta Habari ya Dasa muuza Uji anaye soma Chuo watu waliponda sana wanaponda kwa sababu dada katoka nje ya Confort zone na si vinginevyo.


Wanao pondea Dada wa Mwanza ni kwa sababu yule Dada katoka nje ya Confort zone walizo zizoea wao. sasa hii ni tatizo kwetu watu wa Confort zone.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro Sometimes unachemka sana,yani mtu asome hadi PhD ya injiniaring halafu aje kuuza kande kweli? haya ni matumizi mabaya ya elimu,wenzetu wanatumia elimu zao kigundua vitu vya maana sie twauzia kande hahahaha halafu na wewe unasifia eti yuko nje ya konfoti zoni daah....aibu sana Afrika....
 
Huyu binti ni wakumweka ndani

Sema ni upuuzi wa kiwango cha juu mtu unasoma hadi masters then unarudi mtaani kuuza mahindi...sasa unatofauti gani na aliyefeli darasa la saba

Hizi nchi zetu maskini za kiafrika ngumu sana..

Nanaa
 
NGOJA NAMI NICHANGIE KIDOGO...
Tusipende sana wasomi kufanya mambo tofauti na carrier zao...
AFRIKA NI MASIKINI KWA SABABU WASOMI WENGI HAWAFANYI VILE WALIVYOSOMEA.. UNAKUTA KASOMEA IT LKN ANAUZA NGUO...
TUKUBALI KUWA TUMEPOTEA....
KAMA ALISOMEA UJASIRIAMALI BASI AMEPATIA SANA NA ANAFANYA KILE AMBACHO ANAPASWA KUFANYA ILA KAMA KASOMEA TOFAUTI NA HAPO YUKO WRONG NA HII NI KWA SABABU YA UMASIKINI WETU.
WASOMI WETU WAANGALIWE VIZURI NA KAMA NCHI LAZIMA TUWE NA SERA MADHUBUTI ZA KUWAWEZESHA HAWA WASOMI... TUSICHEKELEE UPUUZI HUU.. MTU KATUMIA GHARAMA KUBWA AFU ETI UNAMSIFIA KUUZA KANDE?? SI BORA ANGEANZA KUUZA TANGIA ZAMANI?? HAKUNA MWENYE KUSOMA AKAWAZA HAYO MAMBO.. ALWAYS HUTOKEA MARA BAADA YA KUSHINDWA KWA SERA ZETU ZA KUIINUA WASOMI WETU...
NCHI YA HOVYO SANA HII.. NA NI AIBU KWA TAIFA KWA WATU KUFANYA VITU AMBAVYO HAWANA UTAALAMU NAVYO..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulianza vizuri lakini na wewe ni chenga tu ka wengine wasioelewa.
Lazima ujue sifa za mjasiriamali na mweke huyo dada ndo utajua pumba uliyoandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida nnayoiona hapa ni kulinganisha nadharia na uhalisia.

Nadharia msomi anatarajiwa afanye mambo makubwa na awe na kipato kikubwa.

Uhalisia msomi hana mtaji wa kujiajiri wala elimu yake haikumuandaa hata kwa interview ya kazi na akirudi mtaani ajikomboe kimaisha anaonekana pathetic.

It was once said, life is never fair.

Live today that’s all you have, tomorrow is not in your capacity rather than probability.

Naona nilipitwa na habari ya mdada naungaunga tuu hapa degree PhD na makande wapi na wapi..... sijui nani anisimulie.

Pia nahisi story imekuwa hivi sababu ni mdada, Je angekuwa mwanaume.... bado angeshangawa au ndo ingesemwa mwanaume kupambana kutafuta hela hakuna kuchagua kazi??..

Nimekumbuka kitu kingine, unakuta mzazi anamsomesha mwanae shule nzuri kuanzia primary ada Tsh milioni tatu kwa mwaka kwa miaka 7, kumla Tsh milioni 21.

Sekondari ada Tsh milioni 2 kwa mwaka kwa miaka 4 jumla Tsh milioni 8.

A level ada Tsh milioni 3 kwa mwaka kwa miaka 2 jumla tsh milioni 6. Chuo anamsomesha hapa nchini analipia miaka 3 kila mwaka Tsh a milioni 3 jumla Tsh milioni 9. Masters anaenda kufanyia Uganda au South Africa achia wa uingereza au marekani, hapo kwa miaka 2 mzazi zinamtoka milioni 10 kwa kiwango cha chini.
Haya ni makadirio ya chini maana hapo gharama nyingine sijaziweka.

Halafu ukute mzazi ana watoto 4 wote wapitie mkondo huo huo.... kisha mtoto akimaliza masters aje kuajiriwa TRA au benki mshahara Tsh milioni 2 kwa mwezi, huo ndo wa kiwango cha juu wengine wanalipwa hadi milioni 1 au laki 8.

Well, elimu / ujuzi hauna expire date ila gharama alizowekeza mzazi na kipato au return anayopata mtoto ni sawa na sifuri.

Inabaki kuwa mapenzi kwa mzazi kuhakikisha mwanae amepata elimu nzuri ili morrow nae aje kumsomesha mwanae.

Uwekezaji kwenye elimu ukikokotoa ije ikulipe kama sio kibosile unaweza piga mbiu wa chini yako wasipoteze muda na hela kusoma na kusubiri ajira.

Kasie.
 
Back
Top Bottom