Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Kiukweli umeongea point ya maana lakin walio wengi humu Kwa unafki wao hatokosa sababu ya kupinga hoja yako ila kiukweli mitaji ndio inawakwamisha sana vijana katika kufikia malengo
Kwani biashara ya makande inahitaji mtaji kiasi gani
 
Bro Sometimes unachemka sana,yani mtu asome hadi PhD ya injiniaring halafu aje kuuza kande kweli? haya ni matumizi mabaya ya elimu,wenzetu wanatumia elimu zao kigundua vitu vya maana sie twauzia kande hahahaha halafu na wewe unasifia eti yuko nje ya konfoti zoni daah....aibu sana Afrika....
 
Huyu binti ni wakumweka ndani

Sema ni upuuzi wa kiwango cha juu mtu unasoma hadi masters then unarudi mtaani kuuza mahindi...sasa unatofauti gani na aliyefeli darasa la saba

Hizi nchi zetu maskini za kiafrika ngumu sana..

Nanaa
 
Ulianza vizuri lakini na wewe ni chenga tu ka wengine wasioelewa.
Lazima ujue sifa za mjasiriamali na mweke huyo dada ndo utajua pumba uliyoandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida nnayoiona hapa ni kulinganisha nadharia na uhalisia.

Nadharia msomi anatarajiwa afanye mambo makubwa na awe na kipato kikubwa.

Uhalisia msomi hana mtaji wa kujiajiri wala elimu yake haikumuandaa hata kwa interview ya kazi na akirudi mtaani ajikomboe kimaisha anaonekana pathetic.

It was once said, life is never fair.

Live today that’s all you have, tomorrow is not in your capacity rather than probability.

Naona nilipitwa na habari ya mdada naungaunga tuu hapa degree PhD na makande wapi na wapi..... sijui nani anisimulie.

Pia nahisi story imekuwa hivi sababu ni mdada, Je angekuwa mwanaume.... bado angeshangawa au ndo ingesemwa mwanaume kupambana kutafuta hela hakuna kuchagua kazi??..

Nimekumbuka kitu kingine, unakuta mzazi anamsomesha mwanae shule nzuri kuanzia primary ada Tsh milioni tatu kwa mwaka kwa miaka 7, kumla Tsh milioni 21.

Sekondari ada Tsh milioni 2 kwa mwaka kwa miaka 4 jumla Tsh milioni 8.

A level ada Tsh milioni 3 kwa mwaka kwa miaka 2 jumla tsh milioni 6. Chuo anamsomesha hapa nchini analipia miaka 3 kila mwaka Tsh a milioni 3 jumla Tsh milioni 9. Masters anaenda kufanyia Uganda au South Africa achia wa uingereza au marekani, hapo kwa miaka 2 mzazi zinamtoka milioni 10 kwa kiwango cha chini.
Haya ni makadirio ya chini maana hapo gharama nyingine sijaziweka.

Halafu ukute mzazi ana watoto 4 wote wapitie mkondo huo huo.... kisha mtoto akimaliza masters aje kuajiriwa TRA au benki mshahara Tsh milioni 2 kwa mwezi, huo ndo wa kiwango cha juu wengine wanalipwa hadi milioni 1 au laki 8.

Well, elimu / ujuzi hauna expire date ila gharama alizowekeza mzazi na kipato au return anayopata mtoto ni sawa na sifuri.

Inabaki kuwa mapenzi kwa mzazi kuhakikisha mwanae amepata elimu nzuri ili morrow nae aje kumsomesha mwanae.

Uwekezaji kwenye elimu ukikokotoa ije ikulipe kama sio kibosile unaweza piga mbiu wa chini yako wasipoteze muda na hela kusoma na kusubiri ajira.

Kasie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…