Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Acheni unafiki ndugu zangu! Angalia tu jiko lake lilivyo, ni kwamba ana mtaji wa kutosha na amewezeshwa huo mtaji! We tengeneza makande kwenye kibanda kama cha Mama Ntilie uone kama utakuwa umefuata nyayo zake!


Point za wengi wetu humu ni hamna kitu kama ule mkumbo wa vijana kulima matikiti maji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wameandika katika hii mada wakisukumwa na wivu, kinyongo au chuki. Tuwe wakweli tu, huyo Nancy anapaswa kupongezwa, tena kupongezwa mnoo, kwa sababu ameweza kuvuka eneo ambalo 99% ya wasomi wa kitanzania wameshindwa.
Nancy pamoja na usomi wake au urembo wake ameweza kukubali kuwa mama ntilie, huku akiifurahia kazi yake, akivuna pesa na hapo hapo ameweza kuajiri wengine.

Sasa tujiulize tu, ni wasomi wangapi wameweza kutumia upeo wao mbadala kuweza kujiajiri mbali na vyeti vyao baada ya soko la kuajiriwa kushindwa kuwachukua?

Kisingizio cha wasomi wengi watakwambia ni mtaji, lakini hapo hapo utaona msomi huyo huyo anamiliki simu ya kisasa ya laki Tano, na kila siku anatumia karibu shilingi 3000 kununua bundle la kuchat umbeya instagram, facebook na whatsapp. Mtaji wa kwanza wa mtu kuweza kujiajiri ni Mawazo yake na Uthubutu wake. Nancy aliwaza kupika makande na akathubutu, leo hii anasonga mbele.
 
Ndugu yangu ameangalia mambo kwa jicho la chuki na wivu mtupu.

Nancy amesema hapo ni kwao, ametumia mazingira yale yale ya nyumbani kwao kuanzisha biashara. Ametumia kilichopo katika mazingira yake ili kuvuna pesa. Ajabu iko wapi?

Wakati huo huo kuna wasomi kibao wanatumia mazingira ya nyumbani kwao kupigia picha ili kujitafutia followers wa umbeya mitandaoni.
 
Yes, hilo ndio lengo la Nancy, na ameweza kulifanikisha. Amejitangaza. Sasa sijui tulitakaje? Yeye kama mjasiriamali ulitaka atumie akili na mbinu zipi kujitangaza? Ulitaka ujifiche? Ulitaka iwe siri yake?
Nadhani katika hilo tulipaswa kumpongeza. Ni jambo jema na lenye kutumia Akili.

Sasa jiulize tu, ni wasomi wangapi wa level ya Nancy wasio na ajira, wanaweza kuwa na ujasiri wa kufanya hicho alichokifanya Nancy cha kuweza kujitangaza hivyo?
 
Wewe ulitaka mtu akisoma Marekani basi arudi Tanzania kufanya nini?
Kwani kusoma Marekani kunakufanya usiwe mama Lishe? Wasomi wa kitanzania wamekaririshwa mnoo.

Mimi ninavyojua, usomi wowote ni bure kabisa kama utashindwa kumkomboa muhusika. Kama utasomea kutengeneza ndege Marekani halafu ukarudi Tanzania ukakosa ajira ya kutengeneza ndege, basi weka pembeni hivyo vyeti na huo utaalamu wa kutengeneza ndege, tumia upeo wako ulioupata katika maisha yako ya kawaida ya kielimu kufanya jambo lingine lolote litakalokufanya kupata pesa na kuishi. Na hicho ndio ambacho amekifanya huyo binti anayeuza Makande.
 
Kweli mkuu, mimi siamini hii masters ya huyu binti
Kama unashindwa kuamini masters ya huyo binti ambaye ameweza kujiajiri na kuweza kuajiri watu wengine watano, basi anza kuamini elimu ya Professor Usorro ya kutulisha upepo watanzania kuwa tutavuna kila mtu Noah yake kwa matrilioni hewa ya makinikia.
 
Mkuu usitake kuiga au kufananisha hicho anachokifanya huyo binti na mazingira uliyopo wewe. Jaribu kujifunza kwa huyo binti na utaelewa. Tusipende sana kutafuta visingizio ili kuhalalisha kushindwa kwetu. Watanzania tumejaa sana woga na hatutaki kufikiri kwa akili zetu. Hakuna siku mazingira yatakuwa rafiki, katikati ya mazingira magumu ndipo wajanja wanatoboa kiuchumi.

Tafakari kwanza ubunifu wake, ujasiri wake na uthubutu wake.
 
h
huyo yuko vizur sana...Yupo mwanza sehem gani na mimi niende kupata Menu hapo!! napenda kula sehemu safi safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…