Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

hili sikubaliani nalo kabisa hizo kande anazouza zina utofauti gani na tunazopika majumbani kwetu?huyu anaitaji maombi
 
Habari wadau...

Nimekutana na habari ya Nancy Lema wa Mwanza nikaona ku-share nanyi wadau mtoe maoni.. je binti yupo sahihi au wrong?

Kafanya Shahada yake St Marys University of Minnesota na masters university of Minnesota huko USA.

Baada ya kumaliza masomo yake akaamua kurudi nyumbani kujiajiri kwa kuuza makande kisasa na kwao ni mambo safi hasa hasa...

Nawaza tu why dada zetu maskini hawapendi kujishughulisha huku washua hawachagui kazi.

Nimemkumbuka na Mercy Kitomari Nelwa Gelato naye ana degree ya U.K ila amerudi Tanzania anauza ice cream tu kisasa

Binafsi, nimempenda bure huyu dada Nancy.....normally kitu anachokifanya, kimewashinda wenzake wengi sana. So anahitaji kupongezwa na kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa sana...ili aendelee kuwa icon kwa vijana wengine wa kitanzania.

All the best Nancy....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu pengine ile comment unaona kwako ni ujinga ni comment wengine ambao ni wasomi wa hali ya juu wanaona hio ndio point safi, in short intelligence is relative sir, be wise
Usomi wa hali ya juu ni kitu gani? Kuna wenye vyeti hakuna wasomi hapa
 
hili sikubaliani nalo kabisa hizo kande anazouza zina utofauti gani na tunazopika majumbani kwetu?huyu anaitaji maombi
Huwezi kufahamu utofauti buku hujazitumia kiongozi,lakini angalia hizo kande bei yake nafikiri utaona utofauti.
 
Huyo hajakataa mshahara muongo, sema asingeweza kuendelea kuishi USA kama mhamiaji haramu, baada ya kumaliza shule. Huyu binti kasema ukweli, karudi nyumbani kwa sababu USA asingependa kuendelea kuishi huko bila makaratasi, baada ya student visa kuisha.
Lakini hiyo kampuni iliyotaka kumuajiri ingeweza kumuombea kupata kibali cha kuishi na kufanya kazi Marekani.( Hapa nazungumzia huyo jamaa aliekataa mshahara wa zaidi ya mil 300)
 
Lakini hiyo kampuni iliyotaka kumuajiri ingeweza kumuombea kupata kibali cha kuishi na kufanya kazi Marekani.( Hapa nazungumzia huyo jamaa aliekataa mshahara wa zaidi ya mil 300
Uhamiaji wangeiuliza kampuni mmekosa mzawa mwenye hizo sifa?Nani asiependa kufanya kazi marekani?????Mnadanywa tu. Huyo mhindi makaratasi ya uanafunzi yaliisha akawa hana jinsi na ikabidi arudi nyumbani. Hiyo sijui ya kukaataa kuajiriwa marekani ni strategy tu ili mumuone yeye ni hot cake.Na kweli kafanikiwa wewe ukiwa mmojawapo umemuamini.
 
unaijua nala app yake.. unajua imeshazoa award ngapi na hela milioni ngapi ameshashinda... mshahara wa milioni 300 alioukataa marekani ni kwa mwaka sio kwa mwezi..

usa mishahara wanapigaga kwa mwaka.. nimeshawai fanya kazi ubalozi wao dar... hata unavyoajiriwa mshahara unaambiwa kwa mwaka ni kaisi flani.. kisha wanaugawanyisha kwa kila baada ya wiki mbili unakuwa unalipwa...

yule fernandez hela alizoshinda tu baada ya kurudi tz zimezidi milion 300 alizokataa marekani...

huyu wa makande sawa naweza kubali... ila yule fernandez ni jembe sana la kupiga hela

sio wa kutegemea ajira yule
 
Uhamiaji wangeiuliza kampuni mmekosa mzawa mwenye hizo sifa?Nani asiependa kufanya kazi marekani?????Mnadanywa tu. Huyo mhindi makaratasi ya uanafunzi yaliisha akawa hana jinsi na ikabidi arudi nyumbani. Hiyo sijui ya kukaataa kuajiriwa marekani ni strategy tu ili mumuone yeye ni hot cake.Na kweli kafanikiwa wewe ukiwa mmojawapo umemuamini.
Nakubaliana na hoja yako kiasi ila sidhani kama kampuni iliyotaka kumuajiri haikujua taratibu zote hizo kuhusu raia wa kigeni kufanya kazi nchini kwao. Kwa maelezo yake yeye ni kwamba alishapatiwa ajira kabisa ila akaikataa that means alikua na vigezo vyote vya kuanza kazi ila ni yeye tu kwa utashi wake akakataa hiyo ajira
 
Kinachokushangaza nini hapo?marekani?makande?mtoto wa kishua?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeuliza kwahiyo watoto wote wakishua wauze makande?.

Nikakuuliza pia nani kasema wauze makande?.

Hakuna jambo linalo nishangaza kiongozi maana jamaa mleta mada katoa mfano wa biashara anayofanya huyo anaemwita mtoto wakishua, jambo lamsingi nilivoelewa nikuwa nawatu wengine wajiongeze kwa namna wanavyoona inafaa.
 
Kiukweli umeongea point ya maana lakin walio wengi humu Kwa unafki wao hatokosa sababu ya kupinga hoja yako ila kiukweli mitaji ndio inawakwamisha sana vijana katika kufikia malengo
Zamani sanaaa nilikuwa namawazo kama haya. Kwamba mtaji ni tatizo... Lakini huyo MTU anayelalamika mtaji hata ukimuuliza anataka mtaji kiasi gani hajui, na mtaji anataka ili aanzishe biashara gani ataanza kujing'ata tu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom