Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Mimi nna degree ya SAUT nachoma mahindi hapa darajani hapa Mbeya.Huyo hafanyi biashara anajitangaza,tupo wengi huku tunatokea kwenye familia maskini mnoooo nadhani ndiyo maana hamtutangazi.....HAKUNA MTU HAPENDI KUFANYA KAZI,HAKUNA MTU ANAPENDA KULA BURE,SHIDA NI MTAJI NA KUPATA KAZI YENYEWE.
Ili uwe mtaji inatakiwa iwe sh ngapi?
 
Huko ni kujipa matumaini tu kwa kiwango cha kipuuzi kabisa. Huko ni kwa mtu alieshindwa kutumia nafasi na fursa aliyoipata vizuri.Kama hachagui kazi huo msemo ilitakiwa aitumie akiwa marekani. Kule kuna kazi nyingi za kwenye mashoprite ya kupanga mabox tu,hata kama unasoma,una uwezo wa kutengeneza hela,tena hela sio hizi. Kule unalipwa kwa masaa. Nina mifano miiiiiingi isiyo idadi. Nina familia jirani,huyo mama ni mzee sasa ana watoto wa4,mkubwa yuko uingereza,ndie alianza kwenda kama kusoma,lakini akaanza na kazi hizo za kwenye mashoprite kupanga mabox,baadae alivyomaliza masomo akatafuta kazi huko huko. Kifupi kwenda kusoma ilikuwa gear tu. Baada ya kuseto akampigia pande mdogoake akaenda,akampa michongo mizima. Dogo baada ya muda pale UK,akasepa uswiswi,nae akamvuta dogo mwingine,huyo dogo wa 3 baada ya muda akasepa marekani,baada ya muda nae akamvuta wa 4. Wa 4 yuko Canada. Familia iko njema sana. Mama akiamua kuzunguka kote kwa wanae. Kazi walizoanza nazo ni hizo ambazo wazungu hawazitaki za kupanga mabox wanaziona ni za chini. Lakini zina mshahara wa kukufikisha ukawa milionea ukija huku kwetu. Hata ufanye ndani ya miaka 10 tu wewe ni bilionea ili mradi uwe na malengo,achana na statehe za kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe nadhani hujawahi kutoka hata nje ya hicho kijiji chenu. Ungewahi kuishi kidogo tu marekani au uingereza usingeandika upuuzi huu huu hapa. Tanzania maisha ni rahisi sana na opportunity ni nyingi kuliko huko marekani na ulaya unaposema. Wacheni ndoto vijana.
 
Ficha ujinga wako unamshamgaa mtu anauza makande mbona humshangai bakhresa anauza chapati na maandazi?
Kweli mkuu wabongo wana visingizio tena vya kijinga. Eti mtu kasoma marekani,halafu anakuja kubana nafasi za akina mama wauza kande eti wanamsifia badala kumpatia shule upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sa
Huko ni kujipa matumaini tu kwa kiwango cha kipuuzi kabisa. Huko ni kwa mtu alieshindwa kutumia nafasi na fursa aliyoipata vizuri.Kama hachagui kazi huo msemo ilitakiwa aitumie akiwa marekani. Kule kuna kazi nyingi za kwenye mashoprite ya kupanga mabox tu,hata kama unasoma,una uwezo wa kutengeneza hela,tena hela sio hizi. Kule unalipwa kwa masaa. Nina mifano miiiiiingi isiyo idadi. Nina familia jirani,huyo mama ni mzee sasa ana watoto wa4,mkubwa yuko uingereza,ndie alianza kwenda kama kusoma,lakini akaanza na kazi hizo za kwenye mashoprite kupanga mabox,baadae alivyomaliza masomo akatafuta kazi huko huko. Kifupi kwenda kusoma ilikuwa gear tu. Baada ya kuseto akampigia pande mdogoake akaenda,akampa michongo mizima. Dogo baada ya muda pale UK,akasepa uswiswi,nae akamvuta dogo mwingine,huyo dogo wa 3 baada ya muda akasepa marekani,baada ya muda nae akamvuta wa 4. Wa 4 yuko Canada. Familia iko njema sana. Mama akiamua kuzunguka kote kwa wanae. Kazi walizoanza nazo ni hizo ambazo wazungu hawazitaki za kupanga mabox wanaziona ni za chini. Lakini zina mshahara wa kukufikisha ukawa milionea ukija huku kwetu. Hata ufanye ndani ya miaka 10 tu wewe ni bilionea ili mradi uwe na malengo,achana na statehe za kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Safiri na kufanya kazi na kulipa bills kwenye hizo nchi unazosema ndiyo unaweza ukapata picha kwanini kaamua kurudi na kuanzisha biashara yake ya chakula.
 
Mkuu Freelancer unakosea!

Hapa wadau hatutaelewa popoma ni nani kati ya wanaomsifia au wanaomkosoa,wewe unaona yupo sahihi kwa elimu yake hiyo kufanya biashala ya chakula?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Biashala = biashara

Mtu mwenyewe hata kuandika hujui sasa unajua nini?
 
Uza karanga
Hivi kwanini watu mliofanikiwa kupata kitu fulani kwenye maisha huwa mnakosa akili na busara? Wengine tulienda shule ili tusiwe wauza karanga au wachoma mahindi,tungetaka kuchoma mahindi au kuuza karanga tungeishia kidato cha nne na kuanza kuuza karanga.....hizi kejeri mnamezeshwa na serikali yenu ya CCM kuwa vijana wajiajiri,mmeshindwa kuzalisha ajira na mmeshindwa kuwawezesha vijana kujiajiri kwa mali au hali,MSITAKE VIJANA TUONEKANE WAVIVU WAKATI TUMEWAKABIDHI HII NCHI ILI MTENGENEZE MWANGA WA MAISHA YA WATANZANIA....narudia tena HAKUNA ASIYEPENDA KUFANYA KAZI WA KULA BURE.
 
Lengo lake kubwa ni kujulikana tu kama kwao mboga nane matunda kibao juice na vyoda, lakini anauza makande na ame somea marekani hilo ndo lengo lake. Hakuna cha makande ya kisasa wala nini kande ni kande tu hakuna kisasa wala nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha upopoma wewe kande za kisasa na kande za kawaida zinatofauti ushazoea zile za kuchanganya na mchicha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka lakini ulivyosema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa alikataa mshahara wa USA akarudi bongo akafungua ofisi mwaka jana ofisi yake ikashirikia shindano ikashinda zaidi ya 200M.

Huyu dada, Degree na Master ya Nje. Anauza makande.

Mimi sidhani kama mtu kufanya biz ya chini inatakiwa ihesabiwe kama inspiration kwa job seeker. Alitakiwa atuonyeshe tofauti yake kama huyo jamaa aliyekataa ule mshahara.

Hapa Tz tayari tuna degree holder anauza uji mwingine anauza mihogo. Yaani ni kwamba degree na master ya nje imewaza sawasawa na degree ya bongo jua kali.
Huyo hajakataa mshahara muongo, sema asingeweza kuendelea kuishi USA kama mhamiaji haramu, baada ya kumaliza shule. Huyu binti kasema ukweli, karudi nyumbani kwa sababu USA asingependa kuendelea kuishi huko bila makaratasi, baada ya student visa kuisha.
 
Huko ni kujipa matumaini tu kwa kiwango cha kipuuzi kabisa. Huko ni kwa mtu alieshindwa kutumia nafasi na fursa aliyoipata vizuri.Kama hachagui kazi huo msemo ilitakiwa aitumie akiwa marekani. Kule kuna kazi nyingi za kwenye mashoprite ya kupanga mabox tu,hata kama unasoma,una uwezo wa kutengeneza hela,tena hela sio hizi. Kule unalipwa kwa masaa. Nina mifano miiiiiingi isiyo idadi. Nina familia jirani,huyo mama ni mzee sasa ana watoto wa4,mkubwa yuko uingereza,ndie alianza kwenda kama kusoma,lakini akaanza na kazi hizo za kwenye mashoprite kupanga mabox,baadae alivyomaliza masomo akatafuta kazi huko huko. Kifupi kwenda kusoma ilikuwa gear tu. Baada ya kuseto akampigia pande mdogoake akaenda,akampa michongo mizima. Dogo baada ya muda pale UK,akasepa uswiswi,nae akamvuta dogo mwingine,huyo dogo wa 3 baada ya muda akasepa marekani,baada ya muda nae akamvuta wa 4. Wa 4 yuko Canada. Familia iko njema sana. Mama akiamua kuzunguka kote kwa wanae. Kazi walizoanza nazo ni hizo ambazo wazungu hawazitaki za kupanga mabox wanaziona ni za chini. Lakini zina mshahara wa kukufikisha ukawa milionea ukija huku kwetu. Hata ufanye ndani ya miaka 10 tu wewe ni bilionea ili mradi uwe na malengo,achana na statehe za kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiachana na hapo kwenye miaka 10 kuwa bilionea hapo kwenye kuvutana vutana hebu nieleweshe vizuri au kma ikibidi nipe mkanda mzima maana ninandugubyangu yupogo huko nashangaaa hanivuti mimi ndugu yake wakati kumbe uwezekano upo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nadhani hujawahi kutoka hata nje ya hicho kijiji chenu. Ungewahi kuishi kidogo tu marekani au uingereza usingeandika upuuzi huu huu hapa. Tanzania maisha ni rahisi sana na opportunity ni nyingi kuliko huko marekani na ulaya unaposema. Wacheni ndoto vijana.
Sawa mkuu. Naongea kitu ninachokifahamu wala sio hadithi,na sio hiyo familia tu,nina wengi wa kuwatolea mifano,na wala sio ndoto,ni ndoto kwenu nyie mkienda ulaya mnajifanya machinoo,mnaiga maisha wanayoishi wazungu. Na kuhusu kutembea,kuna uwezekano mimi nimetembea zaidi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa alikataa mshahara wa USA akarudi bongo akafungua ofisi mwaka jana ofisi yake ikashirikia shindano ikashinda zaidi ya 200M.

Huyu dada, Degree na Master ya Nje. Anauza makande.

Mimi sidhani kama mtu kufanya biz ya chini inatakiwa ihesabiwe kama inspiration kwa job seeker. Alitakiwa atuonyeshe tofauti yake kama huyo jamaa aliyekataa ule mshahara.

Hapa Tz tayari tuna degree holder anauza uji mwingine anauza mihogo. Yaani ni kwamba degree na master ya nje imewaza sawasawa na degree ya bongo jua kali.
She has a long way to go...

Kwani wangapi wanasoma huko huko na hata hicho kidogo hawana.

Akaze buti, akijibrand vizuri few years to come atakuwa mtu mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashala = biashara

Mtu mwenyewe hata kuandika hujui sasa unajua nini?
Sawa sawa baba mwanaidi nikupongeze wewe umesoma vizuri mimi nilikimbia shule kwa hiyo naomba kila utakapokuta humu jukwaani nimekosea unisahihishe kama ulivyofanya hapa na naahidi nitakuwa mwanafunzi bora.

Back
Top Bottom