Huko ni kujipa matumaini tu kwa kiwango cha kipuuzi kabisa. Huko ni kwa mtu alieshindwa kutumia nafasi na fursa aliyoipata vizuri.Kama hachagui kazi huo msemo ilitakiwa aitumie akiwa marekani. Kule kuna kazi nyingi za kwenye mashoprite ya kupanga mabox tu,hata kama unasoma,una uwezo wa kutengeneza hela,tena hela sio hizi. Kule unalipwa kwa masaa. Nina mifano miiiiiingi isiyo idadi. Nina familia jirani,huyo mama ni mzee sasa ana watoto wa4,mkubwa yuko uingereza,ndie alianza kwenda kama kusoma,lakini akaanza na kazi hizo za kwenye mashoprite kupanga mabox,baadae alivyomaliza masomo akatafuta kazi huko huko. Kifupi kwenda kusoma ilikuwa gear tu. Baada ya kuseto akampigia pande mdogoake akaenda,akampa michongo mizima. Dogo baada ya muda pale UK,akasepa uswiswi,nae akamvuta dogo mwingine,huyo dogo wa 3 baada ya muda akasepa marekani,baada ya muda nae akamvuta wa 4. Wa 4 yuko Canada. Familia iko njema sana. Mama akiamua kuzunguka kote kwa wanae. Kazi walizoanza nazo ni hizo ambazo wazungu hawazitaki za kupanga mabox wanaziona ni za chini. Lakini zina mshahara wa kukufikisha ukawa milionea ukija huku kwetu. Hata ufanye ndani ya miaka 10 tu wewe ni bilionea ili mradi uwe na malengo,achana na statehe za kwao
Sent using
Jamii Forums mobile app