Binti yangu; ukiona Dalili hizi kwa Mchumba anayetaka Kukuoa kimbia haraka Sana

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
BINTI YANGU; UKIONA DALILI HIZI KWA MCHUMBA ANAYETAKA KUKUOA KIMBIA HARAKA SANA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwanza nilikuambia unatakiwa ujitegemee na uweze kujimudu mahitaji yako ya msingi. Huo ndio UTU wako. Na hiyo ni Moja ya sifa kuu ya Mwanamke Bora atakayekuwa Mama Bora na Mke Bora kwa mumewe.
Huwezi kuwa Mke na mama Bora ikiwa wewe ni tegemezi. Hiyo haijawahi kutokea.

Kuzaa hata Wanyama wanazaa. Kuzaa hakukufanyi uwe mama na Mke Bora.
Zaa lakini Hakikisha uwe na uwezo wa kujitunza na kutunza watoto wako.
Kushindwa kujitunza na kutunza watoto uliowazaa Mwenyewe NI kujishushia thamani yako ya kiutu.

Ni Bora Mnyama anayeweza kujitegemea kuliko mtu mzima mwenye afya tegemezi.

Na ndio maana Binti yangu kila siku ninakuambia Fanya Kazi za uzalishaji uweze kujitegemea. Mawazo ya kumtegemea mwanaume wanayo wanawake Watumwa, Maskini na ambao hawana tofauti na Makahaba.
Binti za Tibeli hawako hivyo.
Huwezi kujivunia kumtegemea mtu mwingine ilhali wewe ni mtu mzima. Hiyo ni dalili ya utumwa.

Ukishakuwa na mtazamo wa Watibeli Basi zifuatazo ni dalili ambazo ukiziona kwa mwanaume ambaye ni mpenzi au Mchumba wako anayetaka kukuoa, Basi Mkimbie HARAKA Sana;

1. Hawezi kujidhibiti hasa Mihemko yake(anaongozwa na hisia)
Mwanaume yeyote ambaye anaongozwa na Mihemko/hisia zake huyo hawezi kukupa furaha kama Binti za Tibeli.
Mwanaume asiyeweza kujidhibiti hisia zako ni hakika Hana uwezo wa kukutawala na kukufanya uwe Mkewe.
a) Hasirahasira za kijinga.
Mwanaume hapaswi kukasirika hovyohovyo. Kitu kidogo hasira. Kitu kidogo anataka kukupiga au anakupiga. Hapo hamna kitu.
KIMBIA HARAKA. Na usiwe na Muda wa kumbadilisha mtu. Muda ni mchache Sana.

b) Wivu wa kijinga.
Wivu ni sehemu ya Mihemko. Mwanaume asiyeweza kudhibiti Wivu wake huyo Hana uwezo wa kukupa mapenzi yenye furaha. Hajakomaa.
Wivu wa kijinga ni pale ambapo mwanaume anakudharau na kukuona wewe huna tofauti na Malaya wengine. Wewe ni mwanamke rahisi unayeweza kuchukuliwa kirahisi rahisi na mtu yeyote.
Ndio maana ukienda gengeni anakufuatilia, barabarani hataki usalimiane na watu.
Hataki ufanye Kazi kwa Wivu. Ni kwamba anakuona wewe ni Maji maramoja.
Watibeli hatuko hivyo.

2. Anathamini Pesa kuliko UTU.
Watibeli hatuko hivyo. Hata Binti zetu hawako hivyo. Ndio maana Binti ya Tibeli pisikali, inakipato, imesoma lakini inaweza Kuolewa na mwanaume wa kawaida na Binti huyo akawa anamheshimu Sana mumewe.

Mwanaume yeyote anayethamini pesa kuliko UTU huyo kuna mawili aidha akuue wewe au umuue yeye.
Huwezi furahia maisha ya ndoa na mtu anayethamini Pesa kuliko UTU.
Ndoa nyingi zipo kwenye mapito magumu kwa Sababu kuna mmojawapo anathamini Pesa kuliko UTU. Au wote wanathamini pesa kuliko UTU.

3. Hawezi kujidhibiti tamaa yake.
Akiona mwanamke Mzuri anashindwa kujizuia anatumia jitihada za Ziada Kupata ngono ili atimize tamaa yake.
KIMBIA

4. Anakuhonga(wengi huita kuhudumia )wakati hajakuoa Wala hamuishi Wote.
Mwanamke anayekupa pesa wakati hajakuoa Wala hamuishi Wote tafsiri yake hata akikuoa kuna wanawake Nje atakuwa anawahonga kama alivyokuwa anakuhonga wewe.
Zawadi ni Sawa akupe lakini kuhudumia wakati hajakuoa Wala hamuishi pamoja hiyo ni dalili mbaya. KIMBIA.

Elewa kama anakupa pesa wewe kirahisi na hajakuoa na hamuishi pamoja nini kitamzuia kuhonga wanawake wengine siku ikitokea amekuoa?
Binti yangu, Moja ya mambo yanayoumiza wanawake wengi Duniani ni pamoja na kusikia waume Zao wanatoa pesa Nje kwa Wanawake wengine.
Mwanamke hupata uchungu kama uchungu wa fumanizi asikiapo mumewe anatoa pesa Nje.

Weka akilini hii, usije ukafikiri hayo ni Mapenzi na anakupenda kweli ndio maana anakuhonga. Kumbuka Mapenzi lazima yafuatane na Akili ili yaitwe mapenzi ya dhati(kweli).
Mapenzi Bila Akili hayaitwi mapenzi ya dhati kwa Sababu lazima madhara yajitokeze.

Katika hoja hii ndio maana nilikuambia lazima ujitegemee. Ufanye Kazi ili usiwe wale wanawake wajinga ambao kwao kuwa na mwanaume ni kuwa na Mradi.

5. Mwanaume ambaye hakupi Kipaombele.
Huyo ni mwanaume ambaye bado hajawa tayari kuwa Mume na kuwa Baba.
Moja ya ishara ya Mwanaume ambaye yupo tayari kuanzisha familia yake, kuwa Mume na kuwa Baba ni kukupa Kipaombele.
Kama hafanyi hivyo KIMBIA HARAKA.
Hamtajenga familia na mtu ambaye hajui maana ya familia na hayuko tayari kuwa na familia.

Mwanaume anayetanguliza Wazazi wake mbele kuliko wewe mkewe Mtarajiwa huyo Mkimbie HARAKA. Hajui nini anataka. Hajui anajiingiza kwenye kitu gani.
Anachotaka wewe uwe mashine yake ya kumzalia watoto.
Ninakuhakikishia hiyo ndoa utaikimbia au atakufukuza. Na kama utakomaa utateseka Sana.

Mwanaume anayewapa ndugu zake na rafiki zake kipaombele huyo bado hajafikia kiwango cha kuwa Mume au Baba. KIMBIA HARAKA tafuta mwingine.
Hata hivyo Binti za Tibeli nanyi mnajua ya kuwa hata ninyi lazima muwape waume zenu kipaombele. Mkipeana wote kipaombele hakuna kitakacho haribika.

6. Mwanaume ambaye Hana Maamuzi
Yeye ni bendera fuata upepo. Akija Mamaake anafuata. Akija Dadaake anafuata. Akija rafikiake anafuata. Akija sijui nani Ake anafuata.
Hapo hamna kitu. KIMBIA HARAKA.
Mwanaume lazima awe na maamuzi yake binafsi na maamuzi hayo lazima yatangulize mbele familia yenu. Yaani wewe na yeye. Hii ni kumaanisha hata mkiwa Mke na Mume na mkazaa watoto unajua fika kuwa Mumeo anamaamuzi ambayo yanazingatia ustawi wa familia yenu.

Jitu Halina maamuzi halitakufikisha popote. Lipo tayari kuvunja familia yake mwenyewe kisa familia ya ndugu zake au wazazi wake. Hapo hamna kitu.

7. Mwanaume anayefuatilia Maisha ya Watu wengine.
Mwanaume Mbeambea. Kazi majungu na kufuatilia maisha ya watu. Yeye ukikaa naye Kazi kusengenya wengine na kueleza habari za wengine au kutaka kujua ya wengine. Hamna kitu hapo. KIMBIA HARAKA

Mwanaume ambaye anapenda kuingilia mambo yasiyomhusu, kuingilia familia za watu na kujipa umuhimu. Huyo KIMBIA hakuna kitu hapo.

8. Mwanaume ambaye hawezi kuchuja taarifa.
Limepewa taarifa huko hata halijafuatilia vizuri Linakurupuka kupayuka au kutaka kupigana. KIMBIA HARAKA hakuna kitu hapo.
Mwanaume lazima awe na uwezo wa kiintelejensia. Ndio maana pale juu nilikuambia asiendeshwe na Mihemko.

Wanaume wengi ambao wamegombanishwa na wazazi au ndugu au wake Zao, wengi wao walikurupuka ingawaje wao wenyewe huwatupia lawama wanawake ni wachonganishi na wagombanishi wa ndugu lakini kimsingi wao ndio wenye matatizo.

Wanawake kisaikolojia wao ni watu wenye mdomo na mafriji Yao hayaganishi, wanaongozwa na Mihemko. Yeye akisikia taarifa huko anakuletea kama ilivyo na kuongeza chumvi sasa ni jukumu Lako mwanaume kupembua chuya na Mchele.

Sio nawe uwe kama mwanamke.

9. Mwanaume anayependa kujionyesha yeye ni mwanaume.
KIMBIA Sana. Huko ni kutokujiamini.
Mara nyingi wenye Tabia hii hujikuta wakipigana pigana, wakigombana na watu.
Wakipunwa pesa na wanawake wajanja.
Mfano, kuna wale wanawake anaweza kukukuta kwa Mangi unashangaa na anakuambia Fulani ninunulie Soda.
Wanaume wengi hujikuta kwenye tabu hata kama hataki, analazimika kununua hiyo soda ili asionekane sio Mwanaume.
Na kama usiponunua mwanamke atakuambia mwanaume gani unakosa miatano ya soda.

Mwanaume wa hivyo Mkimbie. Sifa za kijingajinga zisizo na Tija.

Pasaka Njema!
Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
TAIKON Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
"wivu wa kijinga"hii ni silaha ambayo wanawake wanatumia ku silence mwanaume pale unapoanza kishtukia nyendo zisizo na afya lakini pia ni njia nzuri pale wanapoamua kumuacha "ana wivu wa kijinga"
 
OG
 
Aisee one of the best content 2025, uko sahihi 100%, But wasio na uwezo mzuri wa kiakili watukupinga na kukutukana.
 
Somo zuri,

Namuwekea binti yangu akikua asome aelewe, maanaa vijana WA ovyo ni wengi kuliko vijana wema
 
Mniue tu , lakini wazazi wangu ni kipaumbele 😂😂
Na nimeoa, mke wangu nampenda na hana baya ! na ndoa nimefunga na mtoto tumepata na tunaishi vizuri.

Lakini nafasi ya wazazi isipuuzwe !
Kila mtu atafiti kwenye vipaumbele vyake panapohitajika wazazi kuwa wa kwanza (kipaumbele) watakua wa kwanza !!
Mke wangu akihitajika kuwa wa kwanza atapewa pia kipaumbele pia.

Maisha ya ndoa hayana jibu la ndio au hapana ila kinachoangaliwa ni situation.

Wazazi ni watu ambao hawajawahi kunikatia tamaa mpaka hapa nilipo ni wao kuanzia tabia , mafanikio hadi mwenendo mimi ni image ya wazazi kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufinyanga hivi nilivyo !!
Na mabinti niwape ronja ukiona mumeo mtarajiwa hapendi au hajali kuhusu wazazi wake shtuka.
 
Kuna vitu hujazingatia kwenye andiko lako umeshindwa kuelewa kuwa binadamu tunatofautiana naona umempa wema zaidi mwanamke umeshindwa kuelewa jambazi hazaliwi ila anatengenezwa kuwa jambazi, mwanamme mwenye wivu na tabia nyingine unazo sema mbovu kwa kiasi kikubwa vinasababishwa na wanawake hao hao mwanamke hata awe mkamilifu kivipi lakini bado yupo kwenye point ile ile kuwa ni mwanadamu mwenye tamaa pia unaposema kujari pesa kuliko mke hapo uchaguzi ni wako jari mke upoteze pesa na mke au jari pesa ili upate pesa na mke!
 
Suala la kumpa kipaumbele mke au wazazi na ndugu itafuatana na mazingira na situation itakayo kuwepo kwa wakati huo, kwa sababu kila mtu ana nafasi yake kwenye maisha yako na kati ya hao hakuna anaye weza kukava nafasi ya mwenzie.
Mke hawezi kuziba nafasi ya wazazi wangu pia na wazazi na ndugu zangu hawawezi kuziba nafasi ya mke wangu.
Hutakiwi kufanya maamuzi kwa kumpa mtu fulani kipaumbele bali unatakiwa kuamua kutokana na ninani mwenye haki na ninani mwenye makosa kwa wakati huo.
Mkeo hawezi kuwakosea heshima wazazi na ndugu zako alafu umchekee eti kwa sababu ndo kipaumbele kwenye maisha yako.
Au mama yako hawezi kuja nyumbani kwako kuwatembelea au kuishi alafu majukumu ya ndani ya nyumba ukamnyanganya mkeo na kumkabidhi mama eti kwa sabababu mama yako ndo kipaumbele chako utakuwa mpumbavu.
Kiufupi kila mtu asimame kwenye nafasi yake.
 
BINTI YANGU; UKIONA DALILI HIZI KWA MCHUMBA ANAYETAKA KUKUOA KIMBIA HARAKA SANA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwanza nilikuambia unatakiwa ujitegemee na uweze kujimudu mahitaji yako ya msingi. Huo ndio UTU wako. Na hiyo ni Moja ya sifa kuu ya Mwanamke Bora atakayekuwa Mama Bora na Mke Bora kwa mumewe.
Huwezi kuwa Mke na mama Bora ikiwa wewe ni tegemezi. Hiyo haijawahi kutokea.

Kuzaa hata Wanyama wanazaa. Kuzaa hakukufanyi uwe mama na Mke Bora.
Zaa lakini Hakikisha uwe na uwezo wa kujitunza na kutunza watoto wako.
Kushindwa kujitunza na kutunza watoto uliowazaa Mwenyewe NI kujishushia thamani yako ya kiutu.

Ni Bora Mnyama anayeweza kujitegemea kuliko mtu mzima mwenye afya tegemezi.

Na ndio maana Binti yangu kila siku ninakuambia Fanya Kazi za uzalishaji uweze kujitegemea. Mawazo ya kumtegemea mwanaume wanayo wanawake Watumwa, Maskini na ambao hawana tofauti na Makahaba.
Binti za Tibeli hawako hivyo.
Huwezi kujivunia kumtegemea mtu mwingine ilhali wewe ni mtu mzima. Hiyo ni dalili ya utumwa.

Ukishakuwa na mtazamo wa Watibeli Basi zifuatazo ni dalili ambazo ukiziona kwa mwanaume ambaye ni mpenzi au Mchumba wako anayetaka kukuoa, Basi Mkimbie HARAKA Sana;

1. Hawezi kujidhibiti hasa Mihemko yake(anaongozwa na hisia)
Mwanaume yeyote ambaye anaongozwa na Mihemko/hisia zake huyo hawezi kukupa furaha kama Binti za Tibeli.
Mwanaume asiyeweza kujidhibiti hisia zako ni hakika Hana uwezo wa kukutawala na kukufanya uwe Mkewe.
a) Hasirahasira za kijinga.
Mwanaume hapaswi kukasirika hovyohovyo. Kitu kidogo hasira. Kitu kidogo anataka kukupiga au anakupiga. Hapo hamna kitu.
KIMBIA HARAKA. Na usiwe na Muda wa kumbadilisha mtu. Muda ni mchache Sana.

b) Wivu wa kijinga.
Wivu ni sehemu ya Mihemko. Mwanaume asiyeweza kudhibiti Wivu wake huyo Hana uwezo wa kukupa mapenzi yenye furaha. Hajakomaa.
Wivu wa kijinga ni pale ambapo mwanaume anakudharau na kukuona wewe huna tofauti na Malaya wengine. Wewe ni mwanamke rahisi unayeweza kuchukuliwa kirahisi rahisi na mtu yeyote.
Ndio maana ukienda gengeni anakufuatilia, barabarani hataki usalimiane na watu.
Hataki ufanye Kazi kwa Wivu. Ni kwamba anakuona wewe ni Maji maramoja.
Watibeli hatuko hivyo.

2. Anathamini Pesa kuliko UTU.
Watibeli hatuko hivyo. Hata Binti zetu hawako hivyo. Ndio maana Binti ya Tibeli pisikali, inakipato, imesoma lakini inaweza Kuolewa na mwanaume wa kawaida na Binti huyo akawa anamheshimu Sana mumewe.

Mwanaume yeyote anayethamini pesa kuliko UTU huyo kuna mawili aidha akuue wewe au umuue yeye.
Huwezi furahia maisha ya ndoa na mtu anayethamini Pesa kuliko UTU.
Ndoa nyingi zipo kwenye mapito magumu kwa Sababu kuna mmojawapo anathamini Pesa kuliko UTU. Au wote wanathamini pesa kuliko UTU.

3. Hawezi kujidhibiti tamaa yake.
Akiona mwanamke Mzuri anashindwa kujizuia anatumia jitihada za Ziada Kupata ngono ili atimize tamaa yake.
KIMBIA

4. Anakuhonga(wengi huita kuhudumia )wakati hajakuoa Wala hamuishi Wote.
Mwanamke anayekupa pesa wakati hajakuoa Wala hamuishi Wote tafsiri yake hata akikuoa kuna wanawake Nje atakuwa anawahonga kama alivyokuwa anakuhonga wewe.
Zawadi ni Sawa akupe lakini kuhudumia wakati hajakuoa Wala hamuishi pamoja hiyo ni dalili mbaya. KIMBIA.

Elewa kama anakupa pesa wewe kirahisi na hajakuoa na hamuishi pamoja nini kitamzuia kuhonga wanawake wengine siku ikitokea amekuoa?
Binti yangu, Moja ya mambo yanayoumiza wanawake wengi Duniani ni pamoja na kusikia waume Zao wanatoa pesa Nje kwa Wanawake wengine.
Mwanamke hupata uchungu kama uchungu wa fumanizi asikiapo mumewe anatoa pesa Nje.

Weka akilini hii, usije ukafikiri hayo ni Mapenzi na anakupenda kweli ndio maana anakuhonga. Kumbuka Mapenzi lazima yafuatane na Akili ili yaitwe mapenzi ya dhati(kweli).
Mapenzi Bila Akili hayaitwi mapenzi ya dhati kwa Sababu lazima madhara yajitokeze.

Katika hoja hii ndio maana nilikuambia lazima ujitegemee. Ufanye Kazi ili usiwe wale wanawake wajinga ambao kwao kuwa na mwanaume ni kuwa na Mradi.

5. Mwanaume ambaye hakupi Kipaombele.
Huyo ni mwanaume ambaye bado hajawa tayari kuwa Mume na kuwa Baba.
Moja ya ishara ya Mwanaume ambaye yupo tayari kuanzisha familia yake, kuwa Mume na kuwa Baba ni kukupa Kipaombele.
Kama hafanyi hivyo KIMBIA HARAKA.
Hamtajenga familia na mtu ambaye hajui maana ya familia na hayuko tayari kuwa na familia.

Mwanaume anayetanguliza Wazazi wake mbele kuliko wewe mkewe Mtarajiwa huyo Mkimbie HARAKA. Hajui nini anataka. Hajui anajiingiza kwenye kitu gani.
Anachotaka wewe uwe mashine yake ya kumzalia watoto.
Ninakuhakikishia hiyo ndoa utaikimbia au atakufukuza. Na kama utakomaa utateseka Sana.

Mwanaume anayewapa ndugu zake na rafiki zake kipaombele huyo bado hajafikia kiwango cha kuwa Mume au Baba. KIMBIA HARAKA tafuta mwingine.
Hata hivyo Binti za Tibeli nanyi mnajua ya kuwa hata ninyi lazima muwape waume zenu kipaombele. Mkipeana wote kipaombele hakuna kitakacho haribika.

6. Mwanaume ambaye Hana Maamuzi
Yeye ni bendera fuata upepo. Akija Mamaake anafuata. Akija Dadaake anafuata. Akija rafikiake anafuata. Akija sijui nani Ake anafuata.
Hapo hamna kitu. KIMBIA HARAKA.
Mwanaume lazima awe na maamuzi yake binafsi na maamuzi hayo lazima yatangulize mbele familia yenu. Yaani wewe na yeye. Hii ni kumaanisha hata mkiwa Mke na Mume na mkazaa watoto unajua fika kuwa Mumeo anamaamuzi ambayo yanazingatia ustawi wa familia yenu.

Jitu Halina maamuzi halitakufikisha popote. Lipo tayari kuvunja familia yake mwenyewe kisa familia ya ndugu zake au wazazi wake. Hapo hamna kitu.

7. Mwanaume anayefuatilia Maisha ya Watu wengine.
Mwanaume Mbeambea. Kazi majungu na kufuatilia maisha ya watu. Yeye ukikaa naye Kazi kusengenya wengine na kueleza habari za wengine au kutaka kujua ya wengine. Hamna kitu hapo. KIMBIA HARAKA

Mwanaume ambaye anapenda kuingilia mambo yasiyomhusu, kuingilia familia za watu na kujipa umuhimu. Huyo KIMBIA hakuna kitu hapo.

8. Mwanaume ambaye hawezi kuchuja taarifa.
Limepewa taarifa huko hata halijafuatilia vizuri Linakurupuka kupayuka au kutaka kupigana. KIMBIA HARAKA hakuna kitu hapo.
Mwanaume lazima awe na uwezo wa kiintelejensia. Ndio maana pale juu nilikuambia asiendeshwe na Mihemko.

Wanaume wengi ambao wamegombanishwa na wazazi au ndugu au wake Zao, wengi wao walikurupuka ingawaje wao wenyewe huwatupia lawama wanawake ni wachonganishi na wagombanishi wa ndugu lakini kimsingi wao ndio wenye matatizo.

Wanawake kisaikolojia wao ni watu wenye mdomo na mafriji Yao hayaganishi, wanaongozwa na Mihemko. Yeye akisikia taarifa huko anakuletea kama ilivyo na kuongeza chumvi sasa ni jukumu Lako mwanaume kupembua chuya na Mchele.

Sio nawe uwe kama mwanamke.

9. Mwanaume anayependa kujionyesha yeye ni mwanaume.
KIMBIA Sana. Huko ni kutokujiamini.
Mara nyingi wenye Tabia hii hujikuta wakipigana pigana, wakigombana na watu.
Wakipunwa pesa na wanawake wajanja.
Mfano, kuna wale wanawake anaweza kukukuta kwa Mangi unashangaa na anakuambia Fulani ninunulie Soda.
Wanaume wengi hujikuta kwenye tabu hata kama hataki, analazimika kununua hiyo soda ili asionekane sio Mwanaume.
Na kama usiponunua mwanamke atakuambia mwanaume gani unakosa miatano ya soda.

Mwanaume wa hivyo Mkimbie. Sifa za kijingajinga zisizo na Tija.

Pasaka Njema!
Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
TAIKON Master
Kwa sasa Dar es salaam
Perfect
 
📌
 
Anakuhonga(wengi huita kuhudumia )wakati hajakuoa Wala hamuishi Wote.
Mwanamke anayekupa pesa wakati hajakuoa Wala hamuishi Wote tafsiri yake hata akikuoa kuna wanawake Nje atakuwa anawahonga kama alivyokuwa anakuhonga wewe.
Zawadi ni Sawa akupe lakini kuhudumia wakati hajakuoa Wala hamuishi pamoja hiyo ni dalili mbaya. KIMBIA.
Zote nimeunga mkono ila sababu namba 4 ina ukakasi.
 
Back
Top Bottom