Mimi nafikiri kuwe na clear separation kati ya mali binafsi na mali za kanisa, misikiti, madhehebu yote.
Sadaka, dhaka,michango inawekwa kwenye account ya kanisa.
Kwamba mchungaji analipwa mshahara, anauza vitabu vyake binafsi hivyo viwekwe kwenye account binafsi.
Ila tufanye hivyo hivyo kwa makanisa yote, misikiti yote, madhehebu yote, dini zote.
KKKT, RC, Sunni, Shia, Hindu, Sikh, kwa Wakristo na Waislamu na wengine wote. Sheria hizo hizo zitumike Tanzania nzima bara na visiwani, dini zote, NGO zote.
CAG aangalie hesabu zao.
Zisilenge watu fulani, wachache, kuwanyamazisha wale wenye maoni tofauti na Serikali kwenye issue fulani, kusiwe na upendeleo wowote kidini, kimadhehebu.
TCRA, TRA visitumike kuwa vyombo vya kuthibiti maoni mbadala.