butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Utajiri una historia ndugu yangu,matajiri wa Bongo wengi wasanii na wezi na ndiyo maana fedha zao wanaficha nje ya nchi.Kwa mfano JK utajiri alionao kautoa wapi na kwao hawana Historia ya utajiri!!Punguza dharau zisizokuwa na maana Mbona jamaa katoa maoni kwa hekima kwamba Rugemalira aliamua kupoteza yote maana alishapanga kila kitu nyumbani kuhusu mali halafu wewe kwa dharau zako unaita porojo.
Umelishwa akili mbaya kwamba kila mwenye pesa ni mpigaji. Yani hakuna tajiri Tanzania mwenye uwezo wa kuwa na pesa zake bila kuitwa mpigaji.?.
Halafu Sasa hivi kila kitu mnamwangushia jk kana kwamba yeye kila ubaya ni wake. Wakati wa Magufuli mlimsema Sana na kumdharilisha mkidhani Magufuli ataishi milele.
Tuheshimu maoni ya wengine Kama unavyotaka maoni yako yaheshimiwe.
Fuatilia mahojiano ya Mawaziri wateule wa Kenya na kamati ya uteuzi ya Bunge lao,watu wapo wazi wanataja utajiri wao na walivyoupata,sasa Bongo kiongozi gani atakwambia kwa uwazi utajiri alionao kautoa wapi!