Biswalo Mganga hana makosa. Plea bargaining ni kwa mujibu wa sheria. Hakuna pesa iliyoingia mfukoni kwa mtu. Zitto ni mpenda sifa za kijinga

Biswalo Mganga hana makosa. Plea bargaining ni kwa mujibu wa sheria. Hakuna pesa iliyoingia mfukoni kwa mtu. Zitto ni mpenda sifa za kijinga

Hivi ungekuwa wewe unapewa kesi isiyo na kichwa wala miguu ya uhujumu au utakatishaji pesa ambayo haina dhamana kisha unakaa gerezani miaka minne upelelezi haujakamilika utafanya nini? Utachanganyikiwa.
Sasa Biswalo na timu yake kumbe muda wote huo wanachunguza fedha ngapi unazo, majumba mangapi au viwanja prime area unamiliki.

Unafuatwa gerezani kila siku na hata ndugu zako wanafuatwa usaini plea bargain uachiwe kwa kulipa bilioni moja na nyumba 2 au 3 uachie. Ukikumbuka hiyo miaka 4 watoto wameathirika, ndugu wamekufa, mkeo anaanza kukosa msimamo na wewe uko matesoni unajiuliza mali na pesa ni nini zaidi ya uhuru wako?

Una saini uporaji huo, na kumbe haziendi serikalini bali Biswalo na nduguze na marafiki wanagawana.
Halafu Nyankurungu2020 anatoka atokako anamtetea!
Ule ulikuwa ni ushenzi na usheteni kabisa
 
Acha porojo, yaani Mzee avumilie mateso ili mali zake zisalimike na mtu wa umri mdogo ukubali kupoteza mali zako,kweli?
Wale wote walikuwa wapigaji tu,sema kwa sasa timu Msoga imerejea basi wanataka waendelee kutafuna nchi.

Punguza dharau zisizokuwa na maana Mbona jamaa katoa maoni kwa hekima kwamba Rugemalira aliamua kupoteza yote maana alishapanga kila kitu nyumbani kuhusu mali halafu wewe kwa dharau zako unaita porojo.

Umelishwa akili mbaya kwamba kila mwenye pesa ni mpigaji. Yani hakuna tajiri Tanzania mwenye uwezo wa kuwa na pesa zake bila kuitwa mpigaji.?.

Halafu Sasa hivi kila kitu mnamwangushia jk kana kwamba yeye kila ubaya ni wake. Wakati wa Magufuli mlimsema Sana na kumdharilisha mkidhani Magufuli ataishi milele.

Tuheshimu maoni ya wengine Kama unavyotaka maoni yako yaheshimiwe.
 
Utawala uliopo ndio unamtuma kupitia mgongo wa nyuma, lengo ni kuwadhalilidha viongozi wote waliokuwa wameteuliwa na JPM na wadhamini ni wafanyabiashara......................kuna siku mpira utapungwa kinyumenyume ambapo mtaziona sura halisi ni akina nani wako nyuma ya hao jamaa.................ndio mpaka sasa kila kukicha wanamzushiwa skendo kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ambaye ndiye anawabana ipasavyo viongozi wa michongo na wabadhirifu wa mali za umma.

Nani huyo anamzushia?. Usitukane mamba kabla hujavuka mto. Tatizo watu wa Magufuli mlidhalilisha Sana kikwete mkidhani mtatawala milele ila Sasa ndio mnalia kuwa mnadhalilishwa
 
Huna akili
Watu hawalalamikii plea bargain kama plea bargain wanacholakamikia ni namna sheria ilivyotekelezwa
kumbuka
1. kuna watu walilipa zaidi ya wengine wakati wako kwenye kesi moja, hili halikuwepo kwenye sheria

2. Utaratibu wa kuwalipisha watu hela ulianza hata kabla ya kutungwa kwa Sheria?

3. Kuna tuhuma pia mchakato kughubikwa na rushwa.

Hizo ndo hoja , hoja sio kwamba hakukuwa na Sheria
Tulia basi huo uchunguzi ukifanyika na ripoti ikitoka ndo utoe hilo POVU

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Hilo kundi haramu la sukuma gang chini ya dhalimu lilifanya mambo mabaya sana ikiwemo kuteka, kuua,na kupora wetu fedha zao. Nakumbuka huu uhayawani ulifanyika hadi kwenye mabureau de change. Kisha wakawa wanatunga sheria mbaya kama enzi za wakoloni ili kuhalalisha unyama wao.
Wewe unajulikana.
 
"Mzigo utaenda serikalini", maana yake nini eti? That is general statement. You have to be specific. "Ulienda serikalini" kwenye Bank Account ipi...???

Maana ukisema "mzigo ulienda serikalini", unasahau kwamba, hata Magufuli na huyu Biswalo ndio waliojifanya wao ndiyo "absolute government"..

Na kwa maana hiyo, wasemao kuwa "mzigo wa Plea Bargaining" ulikwenda kwenye mifuko ya jamaa hawa waliojifanya wao ndiyo serikali kwa hakika wanakuwa HAWAKOSEI...!

Wewe uliyeshindwa kuichambua vyema sheria hiyo ya P.B na kisha unakimbilia haraka haraka kuwaita wenzio washamba, wewe uitweje sasa...?

Obviously, wewe utakuwa mshamba+++!!
Mavi yako mbwa wewe.
Screenshot_20221017-152057.jpg
 
We umejuaje? Punguza kiherehere hakuna jiwe litakalo salia juu ya jiwe....

Heri achekaye mwisho maana hucheka milele....

Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake....

Mngezijua siku zaja za kulia na kusaga meno hakika msingetamani zile karamu Za ubatili na makufuru za fashisti KAYAFA!!
Kwa hiyo umekomaa kana kwamba kuna hoja yenye mashiko!!??
Upuuzi huo ..
Labda nikukumbushe kila kitu kilifanyika kwa mujibu wa sheria na pesa ziliingia kwenye akanti za serekali. Umeelewa ww kilaza!
 
Ule uchunguzi wa pesa zilizopotea benki kuu wakati wa msiba wa Magufuli mpaka leo sijawahi kuona majibu yake, sina imani na hao jamaa.

Kitu kinachofanyika kwa idhini ya mahakama hakiwezi kuhojiwa na kubatilishwa nje ya mahamaka.

Nionavyo mimi, hili ni swala la kifedha (fedha ya umma) ambalo linaangukia kwenye himaya ya CAG. Tukitaka kila mmoja wetu awe CAG hapa, nchi itakwenda ubenibeni!
 
Magufuli alikuwa Msanii

Wizi sio mzuri hata siku 1


Haki itendeke .
 
Kwa hiyo umekomaa kana kwamba kuna hoja yenye mashiko!!??
Upuuzi huo ..
Labda nikukumbushe kila kitu kilifanyika kwa mujibu wa sheria na pesa ziliingia kwenye akanti za serekali. Umeelewa ww kilaza!
"Pesa ziliingia Akaunti ya serikali"

Akaunti gani na ipo benki ipi?

Hata hao jamaa waliopiga hela hizo walikuwa wanajiita "serikali"

Kama una maana ya kuingia mifukoni mwao, you might be right..!
 
"Pesa ziliingia Akaunti ya serikali"

Akaunti gani na ipo benki ipi?

Hata hao jamaa waliopiga hela hizo walikuwa wanajiita "serikali"

Kama una maana ya kuingia mifukoni mwao, you might be right..!
Wajinga mpo wengi sana na story zenu za Mwananyamala Kidile
 
Back
Top Bottom