Hivi ungekuwa wewe unapewa kesi isiyo na kichwa wala miguu ya uhujumu au utakatishaji pesa ambayo haina dhamana kisha unakaa gerezani miaka minne upelelezi haujakamilika utafanya nini? Utachanganyikiwa.
Sasa Biswalo na timu yake kumbe muda wote huo wanachunguza fedha ngapi unazo, majumba mangapi au viwanja prime area unamiliki.
Unafuatwa gerezani kila siku na hata ndugu zako wanafuatwa usaini plea bargain uachiwe kwa kulipa bilioni moja na nyumba 2 au 3 uachie. Ukikumbuka hiyo miaka 4 watoto wameathirika, ndugu wamekufa, mkeo anaanza kukosa msimamo na wewe uko matesoni unajiuliza mali na pesa ni nini zaidi ya uhuru wako?
Una saini uporaji huo, na kumbe haziendi serikalini bali Biswalo na nduguze na marafiki wanagawana.
Halafu
Nyankurungu2020 anatoka atokako anamtetea!