BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

Ooh...mbaya sana hiyo!Ni bora wayaache tu nyumbani na kubadili matumizi yawe mabanda ya kufugia kuku.Chicken coops!
Ni ngumu kuyaacha nyumbani maana wanapoyapeleka gereji wanaaminishwa kua tatizo ni dogo tu, kikipatikana kifaa flani gari itaingia road.

Ndipo wanaposhangaa miaka na miaka gari inafia gereji na kila kifaa wanachoweka kinakua magumashi. Fundi kila siku saundi nyingi za matumaini!

Ndio hivyo wanaishia kuyasusa, madogo saidia fundi wanayafanya magofu ya kuvutia bange na kugeuza kua gesti bubu za kugongea wauza misosi!!!
 
Loooh!Hatari sana.Na kila mtu ajifunze kumiliki idadi ya ng'ombe anaoweza kuwaswaga machungoni wale washibe bila usumbufu.
 
We unazungumza mambo ya kuimpress mlinzi???

Mtu anaenda kuomba deals kwenye kampuni mlinzi anamtolea nje kuingia ndani sababu tu amekuja ya mguu au na bodaboda.

Yaani ukose deals kwa sababu za kipuuzi. Ujinga huo.

Kuna kitu wanashindwa kukuelewa ila kuna mazingira bila Gari unaonekana useless kabisa

Natamani kutoa mfano lakini naona mazingira magumu so far umezungumza point muhimu sana dunia ya leo ni mtu kitu sasa ukitaka kuongezewa kitu lazima uwe na kitu usipo kuwa na hata mfano wa kitu mambo huwa magumu sana.
 
Ndugu umefafanua vizuri sana , Gari zote za ulaya ni bora mno na nirahisi kutengeza japo zina ugharama kidogo kwa sababu spare zake sio nyingi mtaani yaani spare za kukata sio nyingi , hatuna mafundi, hata hao maarufu wengi ni uzoefu tu ila sio kusomea automotive engineering , Mfano nina gari CLS 550 ilikushuka ikagoma kupanda kupeleka kwa mtaani kwa wasomali hapa nilipo nikaambiwa compressor imekufa , kupeleka kwa mtaalam wa kimexico kabadilisha fuse kitu kikapanda dola 200 tu ufundi na fuse , ningemsikiliza msomali litakiwa dola 4000
 
uko sahihi. Tanzania tuna tatizo la mafundi si magari yenyewe. Na ni Tz tu tulioingizwa kwenye maisha ya toyota mno tangia uwepo wetu. Hata Burundi wanatuzid kuyaelewa haya magari.
Lakin ukweli ni kuwa huwezi linganisha ubora na raha ya eurocars dhidi ya Toyota.
Nina kisa kama chako. Jamaa aliniuzia x3 m9 kisa haitengenezeki kwa tatizo la nguvu na dashboard inawaka kama yote. Fundi yule yule wa mazoea ya kifamilia.
Sasa nikahangaika nayo ikafkisha m4 nanunulishwa kila spare za kuagiza tena mwenyewe kila wakipima ni mfumo wa hewa mara air mass, mara censors, had nikajua kila part ya injini.
Ndipo fund wa 7 akaja kugundua ni exhaust tu zimeziba eneo la masega (haitumii unga). At 30km/h inazima. No power. Ndo ikapona kwa 120k nimeshatumia zaid ya 4m.
Ndo nikajua wap tunakwama. Mafund wetu si proffessional na hawana vitendea kaz vya kisasa kugundua hitilaf. Lakin kwa sasa kuna improvements.
Mwaka 2012 horn ya benz E class iliacha kufanya kazi niko mkoan. Pengine kote ikiwa nzima kabsa. Fund akaloop tu na ikapiga. Ajab gari haikutoka had leo. Haikuwaka had kustart. Inalia tu. Mara ooh control box imeshot. Mara censor ya mafuta inaachia yote. Ilipofika m3 nikaachana nayo mana nilishauriwa kuweka injini ingine au ya toyota 3s.
 
Fanya kuwapelekea BMW yako chief kisha ulete mrejesho hapa😊💰💰.
Mafundi wababaishaji hakuna ujuzi, wanachomoa vifaa ama kwa kusudi au kutokujua, hawarudishii, ukosefu wa spare parts na vitendea kazi / mazingira duni.
 
Duuh huyo itakuwa alishort circuit...!! Mafundi majangaa sanaaa... Ila hata gari za siku hizi jamani ni majangaa Betri ikakaa week hujapiga hata siku moja jiandaeeee nyingine kuwaka chap tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…