Shida sio umeme mwingi wala diagnosis.
Shida wamiliki wa hayo magari wabahili na hawana pesa ya kuhudumia hayo magari ya europe.
Garage za kizungu zipo hapa bongo ila wamiliki wa hizo BMW wanaziogopa hizo garage maana ni gharama.
BOSCH garage wana branch hapa bongo. Wana vifaa vyote na skills zote za kutengeneza hayo magari.
Mfano mwingine Bus za kisasa hizi Zhongtong, Yutong, scania G 7. Zina umeme mwingii kuliko hizo bmw , range ama discovery.
Pamoja na umeme wake wote bado diagnosis na hata matengenezo hizo bus zinafanyiwa hapa hapa bongo