BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

Hakuna wapumbavu kama Hawa Vijana wapima na machine, hawajui kutafsiri codes wanakubambikia ugonjwa Mkubwa katika Gari lako, Mimi walishaninunulisha turbo wakati Gari ilikuwa na shida ya nozzle, very useless
Injector? Yaani wanapima waonekane wana uwezo ilhali hawajui kutafsiri vipimo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hujielewi, ninayo Kama hiyo ilipata ajali mwezi baada ya kufika Tanzania, sitaki ipiga rangi, nangoja spare parts zake.

Kumbuka, wakati nangoja parts zake nina hardtop 1Hz, intercooler, kwa hiyo sio pressure wala kungoja hizo parts, na hakuna haraka.

Aliyepark hayo magari anaweza kuwa na uwezo mkuwa sana, au keshanunua au kulipwa na insurance, na Aliyepark hapo ni maskin kadunduliza kununua kwa 6m.
Masikini kumbe wapo wenye magari pia? Daah
 
Gari yoyote usipozingatia kanuni za service i.e wakati na vipuri sahihi lazima itakugharimu.

Pia umiliki wa gari lazima uendane na consistency ya kipato chako. Ukipata fedha nyingi ya ghafla halafu ukachukua european cars lazima itakushinda tu sababu huna flow ya pesa ya uhakika kuweza kuimantain hiyo gari. Tukumbuke pia european cars ni chache sana so automatically vipuri na mafundi lazima watakuwa wachache, simple economic principle, bei zitakuwa juu.

sisi wa uchumi wa kati daraja la chini, tukae tu kwenye Toyota.
 
Back
Top Bottom