BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

BMW SUV (X3,X5) zinatelekezwa garage

Niliwahi kuwaambia wenzangu maskani,hizo gari sasahivi Kila kijana analo lakini hawawezi maliza mwaka watayakimbia kwasababu service zake sio mwembeni,nilisimangwa na kijiwe kizima kwa hoja Mimi natumia caldina(Toyota) Sina uwezo lakini natamani,

Kumbe nilikua sahihi
 
Acha hizo kuna range rovers nyingi sana nimeziona gereji za mitaa ya kinondoni na sinza zimetelekezwa sijui kuna siri gani humo
Insurance zake zinakuwaje, siyo Comprehensive? Maana kumiliki gari kubwa hivyo bila bima kubwa nayo ni ujinga sana. Na kama zina bima kubwa je imeshindwa kufanyia ukarabati mpaka mmiliki kuamua kutelekeza?
 
Niliwahi kuta bei ya sensa moja ya gar ni milion 12. Dah nilipagawa kusikia hiyo bei
Ila aisee spea na service za magari kama huna helaa usijaribu kununua gari za mzunguu walahi... kuna audi niliona inauzwa mil 4 za kitanzania ila shida yake ni CARD ya kucontrol system nzima sijui... kuuliza mtu card inauzwa sh ngapi weeee mil 12+ hapo unaagiza toka nje.
 
Back
Top Bottom