F-22 raptor
Member
- Aug 24, 2023
- 42
- 96
Tatizo kubwa hapa bongo ni mafundi wanatuharibia magari.Wakuu nimeshuhudia hizi gari zikitelekezwa Garage kadhaa hapo Dar. Wamiliki wamechemsha kuzimaintain? Tuachane na kumiliki gari kwa kufuata mkumbo.
MC pilipili like X3 lake sijui kalificha wapi siku hizi
View attachment 2682010View attachment 2682011View attachment 2682012
Inaweza kuwa tatizo la umeme kwenye gari, labda sensor fulani au wiring tu, wao wanalitafsiri ni mechanical problem; wanabomoa injini au gearbox hapo ndo habari imekwisha huna gari.
Imeshawahi kunitokea ndo maana nasema haya, niliingizwa hasara ya kununua gear box nyingine kumbe tatizo halikuwa gearbox, niliyoitoa kumbe ilikuwa nzima,
Gari ilikuwa na tatizo la kushtuka na kuzima inapoingia speed ya 80km/h au wakati mwingine inapoingia speed ya 60km/h, inastuka wakati gear inaingia na inazima. Walibomoa gearbox wakairudidhia ndo ikafa mazima gari haisogei hata futi moja.
Nikanunua hiyo gearbox nyingine wakaweka gari ikarudi na tatizo lilelile inazima baada ya kufikia hizo speed.
Hapo nimeshatupa 2m imagine.
Sasa wakaanza kuisingizia injini nikawaambia acheni nikachukua gari yangu nikaenda nayo nyumbani kwa hasira.
Gari ukitembea speed chini ya 60 unaenda nayo popote haizimi.
Nikaanza kuhangaika mwenyewe utundu utundu wa kufunguafungua kidogo ninao na spanner ninazo kwa kazi zangu ninazofanya.na google pia inasaidia sana tusidharau ilimradi rugha iwe inapanda.
Baada ya kupata marekezo sababu zinazoweza kusababisha hiyo hali wakaziorodhesha, nikafata moja baada ya nyingine.
Nikafika kwenye crank shaft sensor hapo ndipo lilipokuwa tatizo, huwezi kuamini matatizo yote na kuhangaika kote ni hapo, kadude kadogo tu kama betri ya remote, hii gari hiyo sensor ipo chini ya injini imefichwa kidogo na bellhousing ilikuwa imejaa tope limeganda, nikaifungu nikaisafisha nikaifunga gari ikawa imepona inabadili gear vizuri haizimiki tena
Mafundi sina hamu nao.