TANZIA Bob Makani afariki dunia

TANZIA Bob Makani afariki dunia

Innalilah wainna Illahi Rajiun.

Poleni sana Familia ya Bob Makani, poleni sana Chadema.
 
kama ilivyo desturi ya mwanadam uzaliwa na ufa hakuna ajabu hapo heri umeenda mwenyekiti wangu mstaafu na kuiacha hii dunia hasa tanzania yenye matatizo lukuki tunasemaga r.i.p lakini hatuna uhakika tunabahatisha tu.
 
Poleni wakuu,tatizo lake lile lile au jingine? Maana nakumbuka kulikua na uzi alilazwa aghakan!!

cha maana ni kumuombea apumzike kwa amani na kuwaombea ndugu jamaa na marafiki na wapenda mabadiliko nguvu ya kupokea msiba huu mzito! wewe hata ukijua tatizo lililomnyakua kutoka ulimwengu huu itakusaidia nini?? au unataka kuanzisha majungu??
 
R.I.P kamanda wangu pumzika kwa amani! Nasikitika umeenda wakati chama ndio kinazidi kupata mafanikio na kukubalika kila kona ya nchi kamanda kwa nini hukusubiri ukashuhudia chama ulichokiasisi kikichukua madaraka hapo 2015? Jibu ni rahisi mungu amekupenda zaidi! Tutakosa busara na ushauri wako lakini kama kukuenzi tutazingatia yote mema uliyotuasa wakati wa uhai wako! Pumzika kwa amani kamanda!!
 
r.i.p bob..mzee alikuwa anapiga fegi balaa!poleni wapigania uhuru wote
Wakati wa msiba mzito kama huu hatutegemei mzaha! kama alikuwa anapiga fegi wewe inakuhusuje? Ndugu jamaa na marafiki wanatarajia maneno ya kuwafariji kipindi hiki kigumu! R.I.P Mwenyekiti mstaafu wa CDM!!
 
Ameitumia fursa ya maisha yake (1) kuamini alivyopenda (2) kuchagua utumishi aliopenda. Mchango wake katika nchi utapimwa, kukumbukwa na kusahaulika. Sasa amelala, hana ufahamu tena, hana furaha wala huzuni, hana uwezo kuzungumza, kuonya wala kuomba, kutubu wala kukemea... hadi siku Mungu atakapokuja kutowa hukumu ya haki kwa kila mmoja.

Poleni familia yake, poleni CDM, poleni watu wote walioguswa na msiba huu. Alitwaliwa kutoka katika mavumbi na huko amerudi tena, neno la Bwana limetimia.
 
RIP makani Mungu akutangulie sana hapa dunia tunapiata tu kazi ulifanya na misingi uliijenga kwa kuwa mzalendo wa nchi yako Mungu akulaze mahali pema peponi.
 
Unaleta siasa mpaka kwenye mambo ya misiba. Mtu kuuliza chanzo cha kifo kuna ubaya gani?

ndio tatizo letu eti mtu kauliza chanzo mtu anatokwa mapovu ya kutukana nakumuita mwenzake gamba, this is way too much.
 
Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi natoa rambirambi zangu kwa ndugu jamaa na marafiki,viongozi na wanachama wote wa Chadema...Mungu awatie nguvu na ujasiri katika hiki kipindi kigumu cha msiba...Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Pole sana familia ya Makani na Chadema kwakuondokewa na mpambanaji wa ukweli hakuna asiyemjua hasa kwa mapenzi yake aliyaonyesha kwa chama akiwa mwenyekiti.

Mungu ampe pumziko jema.
 
Confirmed!

Mohamed Nyanga (Bob) Makani is no more... Katutoka muda si mrefu


...............

Kumbe alikuwa Muislamu!!!

Chadema inaonewa jamani sasa mbona wanasema ni cha kidini kumbe waasisis walikuwa dini mchanganyiko!!!!

RIP Kamanda .......

Mwambie JK Nyerere kuwa chama alichokipenda sera zake ndicho kitatawala kuanzia 2015!

....
Mapambano yanaendelea!!
 
Wewe ulikuwa unajua mkristo hujui hata historia ya chama chako kweli wewe dot.Com
...............

Kumbe alikuwa Muislamu!!!

Chadema inaonewa jamani sasa mbona wanasema ni cha kidini kumbe waasisis walikuwa dini mchanganyiko!!!!

RIP Kamanda .......

Mwambie JK Nyerere kuwa chama alichokipenda sera zake ndicho kitatawala kuanzia 2015!

....
Mapambano yanaendelea!!
 
Aliitumikia Tanzania, akaijenga CDM na upinzani Tanzania, na sasa Mungu amemtanguliza mbele ya haki. R.I.P. Comrade Makani. Ukifika msalimie Nyerere, mweleze kuwa CDM itaichukua nchi 2015.
 
Back
Top Bottom