Amina. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
Yatasemwa mengi sana mazuri kuhusu Bob Makani katika medani ya siasa. Na yatakuwa ya kweli. Niongeze hili moja tu kuhusu Mzee Makani ambalo aliniambia akiwa katika ofisi yake eneo la Co-Cabs pale Kidongo Chekundu: kwamba siasa inahitaji Uvumilivu mkubwa sana.
Alisema hili akiwa katika shida kubwa sana kifedha, baada ya mapato yake binafsi kuyumba kwa sababu ya kuhujumiwa na waliotaka Chadema kuyumba miaka ya mwanzoni--yaani miaka ya 1993 - 96 hivi. Wateja wake wengi katika Practice yake ya Law walikuwa Wahindi.
Wahindi hao walipewa onyo na taasisi fulani za serikali kwamba wakiendelea kumtumia Mzee makani kama mwanasheria wao, basi taasisi hizo zingechukua hatua ambazo zingeathiri biashara za Wahindi wale, na wahindi wengi wakaondoa mahitaji yao ya huduma za kisheria kutoka kwa Mzee Makani na kusababisha njaa kubwa kwa mwanachadema huyu.
Shughuli nilizokuwa nikifanya wakati huo zilinileta karibu na Bob Makani kiasi cha kutosha akanisimulia habari hii kwa uchungu sana ofisini kwake; lakini alichokisema mwishoni kikawa kwamba Siasa hataiacha kwa sababu ya hujuma hiyo, kwa kuwa Tanzania ilihitaji mabadiliko.
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.