Kama kawaida yako unaandika takataka tu humu, kupoteza muda.kwanza kabisa ifahamike wazi kwamba vyombo vya kiuchunguzi vya ulinzi na usalama haviwezi hata siku moja kupuuzia taarifa zozote za kihalifu zinazoweza kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa wananchi lakini pia taarifa zinazoweza kutumika kukamilisha uchunguzi au kufanikisha kuwatia nguvuni wahalifu...zote hizo mitandaoni zinazongatiwa...
jambo la pili la maana zaidi ni kwamba, baada ya hatua za kiuchunguzi kukamilika, kule mahakamani hapataki mzaha, harakati, hisia au huruma...
panahitajika uthibitisho wa ushahidi usio na mashaka dhidi ya mashaka yaliyowasilishwa mbele ya pilato..
na mapilato wengi sasa hivi hawaburuzwi tena kama zamani, kila moja anataka kuweka yake records safi, kwamba atoe hukumu ya haki ya kihistoria amabayo hapo baadae itumike kama reference kuhukumu kesi nyingine au kama reference ya kufundishia vyuoni...
nitoe wito tu kwa ujumla,
kwamba pamoja na hizo picha za mitandaoni,
ikiwa kuna raia yeyote, anazo taarifa za kutosha kufanikisha uchunguzi au kutiwa nguvuni kwa wahalifu wa utekaji na wengineo, milango ya vyombo vya ulinzi na usalama iko wazi, ajitokeze ili kufanikisha upatikanaji wa haki kwa waliodhulimiwa...
samahani sana kwa maelezo marefu niko ambako siwezi kuandika vizur 🐒